Alhamisi, 22 Juni 2017

WAZIRI MAKAMBA:WAKULIMA MABONDENI(VINYUNGU)WASIBUGHUDHIWE NA NI MARUFUKU KATIKA MAENEO MAPYA

Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba

Wakuu wa wilaya za Iringa wakiwa katika kikao cha kazi Siasa ni Kilimo

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na miji Iringa.

Wabunge wa Mkoa wa Iringa wakiwa katika kikao kujua hatma ya kilimo mabondeni


Kikao cha kazi mkoani Iringa chini ya Waziri makamba



Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira January Makamba amewataka watendaji wa serikali katika halmashauri zote nchi kutowabughudhi wananchi wanatumia kilimo cha mabondeni maarufu kama vinyungu mpaka litakapotolewa tamuko rasmi litakalotokana na makubaliano ya viongozi ambapo ametoa muda wa miezi mitatu kukamilisha majadiliano yatakayolenga kutatua mkanganyiko uliopo.
Waziri makamba amesema hayo  hii leo mkoani Iringa wakati alipokutana na viongozi wa mkoa huo ili kutoa ufafanuzi juu ya suala la utunzaji wa mazingira kwa kufuata kanuni zilizopo kutokana na sintofahamu iliyowakumba wananchi la kuzuiwa kutumia kilimo cha mabondeni kwa lengo la kutunza vyanzo vya maji jambo linaloifanya serikali kuwataka wananchi waendelee na shughuli za kilimo katika maeneo waliyopo na kutoingia katika maeneo mapya.
“kumekuwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wetu huku vijijini ambao wamekuwa wakiwakamata na kuwatesa wananchi pale wanapowakuta wananchi wajishughulisha na kilimo huku wakitumia nafasi zao kwa madai kwamba kuna agizo limetolewa hayo siyo maagizo leo muwambie wananchi waendelee na shughuli zao katika maeneo waliyopo na siyo kuingia katika maeneo ambayo bado hayajaguswa”
Katika hatua nyingine Waziri makamba ameyataka makampuni na Taasisi zilizowekeza katika sekta ya misitu nchini kuona namna ya kuanza kuitoa miti isiyorafiki wa mazingira katika vyanzo vya maji na kupanda miti inayohifadhi na kutunza maji badala ya kuwatazama wananchi pekee kuwa ndiyo sababu ya uharibifu wa mazingira.
“kumekuwa na makampuni na Taasisi ambazo zimewekeza katika misitu na chain a zimepanda mazao hayo mpaka kwenye vyanzo vya maji tunajaribu kuona jinsi ya kukaa nao ili waweze kuitoa kusudi wapande miti rafiki na vyanzo vya maji badala ya kuwabana wakulima tu pekee yao ningependa ndani ya wiki tatu tuwe na mkutano wa viongozi wote tuone namna ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa iringa na mabonde yote kubaini hali ilivyo huko”alisema makamba
Cosato Chumi na Venance Mwamoto ni Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini alisema wabunge richa ya kupigia kelele bungeni agizo hilo la wananchi kutojihusisha na kilimo hicho walisema iwapo serikali isingelitazama jambo hilo lingekuwa na athari za kiuchumi na maisha ya wananchi kwaujumla hivyo wamewataka wananchi kuzingatia maagizo kwa kushiriki utunzaji wa mazingira kwa vitendo.
“unapo angali athari za kimazingira ni lazima uangalie pande zote maana usiangalie kuhifadhi mazingira wakati unaumiza wananchi lakini inategemea na maeneo ambayo hakuna ulazima wa kufanya hivyo ukuangali kwa wilaya mufindi na mkoa wa Iringa tayari wananchi wake wanatunza vyanzo vya maji na kilimo cha vinyungu ni sehemu ya maisha ya wananchi kwahiyo jambo la kuwaacha wakulima waendelee ni sawa na tunaamini watatunza zaidi vyanzo vya maji”alisema Chumi
Venance Mwamoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo kwa upande wake alisema changamoto iliyopo ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya utofautishaji wa neon chanzo cha maji serikali iliona vyema kupiga marufuku lakini najua mkoa wa iringa unaasilimi zaidi ya 70% ya wananchi wake wanategemea kilimo cha vinyungu tayari tungeanza kuona madhara kwenye masoko kukosekana kwa Mboga halmashauri zingeanza kukosa mapato kwahiyo tunashukuru kwa uamuzi huu unatupa nguvu ya kufanya ziara kwenye majimbo yetu”alisema Mwamoto
Kwa upande wao baadhi ya Madiwani wamepongeza jitihada zilizofanywa na serikali kwani wanasema kuzuiliwa kwa kilimo cha mabondeni kulikuwa na Athari za moja kwa moja kwa wananchi kwani wananchi kwa kiasi kikubwa wanategemea kilimo hicho kutokana na msimu wa mvua kuwa mmoja
Hivi karibuni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hasan aliunda kikosi kazi ili kufanya upembuzi juu ya kulinda na kuokoa mto ruaha mkuu unaoonekana kuathiriwa na shughuli za kijamii huku mkoa wa iringa ukitegemea kilimo cha mabondeni ili kuwatoshereza wananchi kupata kipato na chakula.

leo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni