Jumatatu, 3 Julai 2017

UJERUMANI MABINGWA KOMBE LA MABARA 1-0 DHIDI YA CHILE

media
Michuano ya kombe la Mabara imemalizika na Hatimaye Timu ya Soka ya Taifa ya Ujerumani imeibuka Bingwa mara baada ya kumtandika bao Moja kwa Sufuli timu ya Taifa ya Chile ambaye katika mchezo wao uliopita Chile vs Ujerumani walitoka sare ya bao moja kwa moja uliochezwa kwenye uwanja wa Kazan Arena huko Kazan, Urusi.

Jumapili usiku, Julai 2, kumefanyika mtanange wa mechi moja ya fainali, ambapo timu ya taifa ya Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia lililopita nchini Brazil ambapo kwa sasa chini ya Mwalimu Joachim Löw ambaye amekiandaa kikosi cha Ujerumani na kurudisha heshimaya Soka nchini Ujerumani.

Ujerumani iliingia uwanjani kwenye mchezo huo, ikiwa na historia nzuri ya kuanza vyema michuano ya mwaka huu mpaka kwenye hatua waliyofikia baada ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

Ujerumani imetengeneza Historia ya kuwa timu nyingine itakayofanikiwa kutwaa taji la michuano ya Ulaya baada ya lile la kombe la dunia kama ilivyowahi kufanya timu ya taifa ya Hispania, iliyotwaa kombe la dunia mwaka 2010 na kushinda taji la Ulaya mwaka 2012.

Jumapili, 2 Julai 2017

Ujerumani 1 vs 0 Chile katika Mechi ya fainali ya (Confederation Cup)


Michuano ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa (Confederation Cup)inaendelea ambapo timu ya taifa ya Ujerumani inakipiga na Chile katika hatua ya fainali.

Katika mchezo huo Ujerumani imejipatia bao la kuongoza katika dakika za kipindi cha kwanza bao linaloendelea kudumu hadi sasa mchezo huo upo dk ya 86

TAIFA STARS YASONGA NUSU FAINALI BAADA YA KUTOA DOZI YA GOLI 1-0 DHIDI YA AFRIKA KUSINI


Image result for kikosi cha taifa stars 2017
Timu ya Soka ya Tanzania Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0 thidi ya Afrika Kusini katika michuano ya Balaza la Soka katika nchi za kusini Mwa Africa COSAFA ambapo katika dk 18 mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Elius Mguli jezi nambali 12 mgongoni aliwainua mashabiki kwa kupachika Bao la kwanza na la Ushindi.
Taifa Stars ilifuzu kuingia katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya michuano ya COSAFA inayo endelea huko nchini Afrika Kusini baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Mauritius.
Huko Afrika kusini Timu yua Tanzania ikicheza na Wenyeji wa Mashindano hayo Afrika Kusini imekuwa ilicheza mchezo wa kuvutia kuonesha ukomavu wa soka huku timu ya wenyeji wakidharu mchezo huo ambapo imewagharimu na sasa watabaki kuwa watazamaji wa wa Mashindano hayo baada ya kutolewa kwa Goli moja kwa sufuli.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Mcheza Mhimu katika mchezo huo(MAN OF THE MARCH)Elius Maguli amesema walipata nafasi na wameitumia na kupata goal lililowapeleka kwenye Nusu Fainali
“tunashukuru tumetumia nafasi tuliyoipata tumeshinda cha msingi ni kujiandaa katika michezo mingine”alisema mchezaji huyo
Katika michuano hiyo Taifa Stars imekuwa ikionesha tofauti na Timu zingine kwani Hadi leo imepata nafasi ya kutoa Man Of The March kwa mara ya Nne mfurulizo
Sayari ya Habari inaitakia Taifa Stars Ushindi katika mechi zijazo.

TANZANI 1-AFRICA KUSINI 0 KIPINDI CHA KWANZA KATIKA MICHUANO YA COSAFA



Nahodha wa Taifa Stars Himid Mao amesema kufikia hatua ya robo fainali michuano ya Baraza la Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) kumewapa imani kubwa dhidi ya safari yao kuelekea mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Mao ameiambia Sayari ya Habari,  kama wataendeleza morali walionayo sasa wanaweza kufika mbali ikiwemo kuwatoa wenyeji Afrika Kusini leo.

Amesema kikubwa ni wachezaji kuendelea kujituma na kuisaidia timu kufikia malengo yake.

“Tunashukuru Mungu kwa kufikia hatua muhimu kama hii ya robo fainali, nategemea tukiendeleza juhudi tutafika mahali pazuri kuelekea safari yetu ya kutafuta nafasi ya kufuzu CHAN na ikiwezekana Afcon,”amesema.

Mao amesema kikubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri mchezo wa leo dhidi ya Afrika Kusini na kutoa picha kamili.

Amesema Afrika Kusini ni timu iliyoendelea na itawapa changamoto na kutoa tathmini juu ya safari yao ya Chan na Afcon.

Jumamosi, 1 Julai 2017

ZAIDI YA VIJANA 500 IRINGA WASHIRIKI KATIKA TAMASHA LA JPM STAR SEARCH

Displaying photo.jpgWasanii chipkizi mkoani iringa wamewalalamikia wasanii wakubwa kwa kushindwa kuwapa ushirikiano katika kazi mbalimbali za sanaa hali inayochelewesha wasanii wadogo kufikia mafanikio na hivyo kudumaza tasnia hiyo hapa  nchini

Wakizungumza katika uzinduzi wa Tamasha linalojulikana kwa Jina la JPM Starsuch lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Manispaa ya Iringa na kufanyika katika ukumbi wa Hall Fear mkoani hapa kwa lengo la kibua vipaji mbalimbali kwa vijana  walisema kumekuwa na ugumu kwa wasanii wa kubwa kuonesha ushirikiano kwa wasanii wachangajambo linalosababisha linayosababisha kushindwa kuwepo kwa ushindani katika tasnia ya film na muziki na kuleta Tija kwa Taifa.

De Money ni miongoni mwa wasani chipkizi wa Sanaa ya Muziki wa Bongo Freva aliiambia SAYARI YA HABARI kuwa richa ya vijanawasanii kujiytuma lakini bado wanahitaji Sapoti kutoka kwa wasanii wakubwa jambo ambalo lipo tofauti kwani baadhi ya wasnii wakubwa wamekuwa wakihitaji fedha nyingi ili kufanya nao Korabo(kushirikisha)katika nyimbo kwa kisisngizio kwamba wanawabeba

“tunatamani sana kufika mbali kwasababu kama masinii unapofanyakazi unakuwa na maono ya wapi unataka kufika lakini pia kama msanii unajaribu kuwatafuta wasanii waliotangulia angalau wanamajina lakini changamoto kubwa hawaoneshi ushirikiano wa moja kwa moja gharama inakuwa kubwa ukitaka umshirikishe katika nyimbo yako natamani tusaidiane tuitangaze sanaa yetu ya Muziki”alisema De Msanii huyo

Merina Mlowe pia ni miongoni mwa waigizaji walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha Hilo ambapo alisema kama wasanii wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa fedha kama mitaji kwaajili ya kufanyia kazi zao jambo linalokwamisha jitahada wanazozifanya katika kutengeneza Tamthilia zenye Ubora hivyo aliiomba serikali iwasaidie waweze kupata mitaji ili iwasaidie kuandaa kazi bora.

“kwa kweli tunatamani sana kufanya kazi kwa kiwango kikubwa lakini tunashindwa kutokana na uhaba wa fedha ila tunawapongeza UVCCM kwa kuona waanze kuuanda mikakati ya kuibua vipaji na kuikumbusha serikali wajibu wake katika kutuwezesha vijana tuweze kujiari”alisema Merina

Kwa upande wake  rais wa shirikisho la film Tanzania Simon Mwakifamba alisema wasanii wakubwa ili kuiinua sanaa Tanzania ni lazima wasanii wakubwa watumie nafasi zao kuwainua wasanii chipkizi  kwani ili sanaa iwe na Tija kwa Taifa ni lazima watu wengi wawekeze katika shughuli hiyo badala ya kuwakatisha tama na kushindwa kufanya kazi pamoja na wasanii hao wachanga.

“hii ni kiongoni mwa changamoto ambazo zipo pengine mi mi nisema ni vema sasa wasanii wakubwa wanajitambua tena kwa majina ifike wakati tuwaone wasanii wadogo ni sehemu yetu hawa wakikua watatusadai lakini pia niwatie shime hilo lisiwakatishe tamaa kuweni wabunifu fanyeni kazi”alisema

Alphonce Myinga ni Katibu wa UVCCM Manispaa ya Iringa alisema Mashindano  hayo richa ya kuibua vipaji lakini pia yalilenga kuwakutanisha vijana pamoja ili kuoneshana wapi zinapopatikana Fursa ili vijana waweze kuwa na mambo ya kufanya badala ya kubaki wakilalamika kuwa hakuna ajira ipo haja kwa vijana kuanzisha miradi yao ikiwa nai pamoja na kujiingiza kwenye sanaa ili waweze kuonesha vipaji vyao na kuitangaza nchi.

“kanuni za umoja wa vijana zinaniongoza mimi hasa nikiwa natekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini nimeandaa tamasha hili ili kuhakikisha tunawaunganisha vijana ili waepukane na matendo mabaya wawe na jambo la kufanya kwa sababu sanaa ni ajira wajibu wangu ni kuwa linda vijana ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.”alisema katibu UVCCM

Naye mkuu wa wilaya ya iringa Richard kasesela alisema ipo changamoto kwa baadhi ya wasanii ambao hutumia nafasi zao kwa kudharau wengine na kuona wamefanikiwa jambo linalorudisha Nyuma maendeleo hivyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza baadhi ya wasanii wenye nia ya kuwainua vijana wenzao ambapo kwa kwakufanya hivyo kunawafanya na wao kufanikiwa zaidi.

“niwakumbushe wasanii nchini upo ukomo wa kuwa msanii hebu tumieni nafasi zenu kuwainua wasanii wenzenu kwani njia hiyo ndiyo hutumiwa na nchi zilizoendelea wale waliofanikiwa wanatumia nafasi zao kuwasadia waliochini ili kuweka Chain ya Wasanii mmoja anaposhindwa Yule aliyeibuliwa anaendeleza pale pongezi nyingi kwa Diamond kwa kusaidia vijana wenzake.”alisema kasesela

Alhamisi, 29 Juni 2017

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA IRINGA ROSE TWEVE AENDELEA NA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI


Zaidi ya kata 107 za mkoa wa Iringa kuanzisha mifuko maalumu ya kuwezeshana kiuchumi kutokana na Fedha zinazochangiwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Rose Tweve ili kuwawezesha wanawake kujitegema na kufanya ujasiliamali pasipo kujali itikadi.

Kutokana na Mpango huo wa Mb Rose tayari Zaidi ya kata 40 za wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi zimekwishanufaika na mpango huo unaokiwezesha kikundi cha wanawake katika kila kata kupata Sh 600,000 ambazo hazirudishwi.

Akizungumza wakati akikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa vikundi vya kata za Nyololo na Malangali, Tweve alisema zoezi hilo litaendelea katika kata zingine zote zilizobaki zitakazokamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo ya kuunda uongozi wake na kufungua akaunti benki.

Tweve alisema kwa kupitia mifuko hiyo itakayojulikana kama mifuko ya Rose Tweve ya kila kata wanawake watajiwekea utaratibu wa kuweka na kukopa, kuinuana kimaendeleo na kubuni mambo mengine yatakayowazidishia kasi ya maendeleo yao.

“Wanawake tupo wengi sana, lakini tunakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoturudisha nyuma. Huu ndio muda wa kujipanga upya na kubadili maisha yetu kwa kutumia kauli mbiu ya rais wetu Dk John Magufuli ya Hapa Kazi tu,” alisema.

Alisema kutakuwepo na utaratibu wa kuvifanyia tathimini vikundi hivyo na vile vitakavyofanya vizuri vitapata nyongeza ya fedha kila mwaka kwa kupitia mpango huo.

“Nimeanzisha mpango huu kwa kutumia rasilimali zangu mwenyewe na kwangu mimi naona hili la kusaidia wanawake wenzangu kwa kutumia rasilimali zangu linawezekana,” alisema.

Alisema matokeo chanya yatakayojitokeza  katika vikundi hivyo yatamshawishi atafute wafadhili wengine wa ndani na nje ili wasaidie zaidi.

“Sitoi fedha hizi ili mgawane kwa matumizi yasiofaa, natoa kama jitihada zangu za kuwahamasisheni kuona haja ya kuwekeza kwa pamoja na kwa manufaa ya wote,” alisema.

Akishukuru kwa mchang huo, mmoja wa viongozi wa kikundi cha wanawake wa mfuko wa Rose Tweve wa kata ya Malangali, Judith Kisinini alisema wako katika mchakato wa kuanzisha duka la kuuza pembejeo za kilimo, hatua itakayowawezesha wanawake wakulima wa kata hiyo kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu.



“Fedha hizo pamoja na michango ukiwemo wa mheshimiwa mbunge na faida tutakayokuwa tunapata kutoka katika shughuli tutakazokubaliana kufanya zitatumika kuendeleza wanachama wote bila ubaguzi wowote,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Nyololo, Grace Mbembati alisema; “mchango waliopata kutoka kwa mbunge huyo utatuongezea kasi katika kutimiza wajibu wetu ili kufikia azma tuliyonayo katika kusaidiana kiuchumi.”

Jumatano, 28 Juni 2017

HALMASHAURI YA WILAYA KILOLO YADHAMILIA KUMALIZA KATIKA SEKTA YA AFYA KWA KUJENGA HOSPITALI YA KISASA

Baadhi ya Majengo ya Hospitali ya Kisasa ya Halmashauri ya wilaya ya Kilolo
Halmashauri ya wilaya kilolo imedhamilia kumaliza kero inazowakabili wananchi hususani katika sekta ya afya kutokana na mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya itakayowahudumia zaidi ya  kata 12 za wilaya hiyo kutokana na kuikosa huduma hiyo kwa muda mrefu na kulazimika kuitafuta katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa

Aloyce Kwezi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Aloisi Kwezi na Asiah Abdallah ni mkuu wa wilaya hiyo waliiambia SAYARI YA HABARI kuwa  halmashaurii hiyo inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya wilaya kwa kushirikliana na wakala wa Majengo nchini TBA ikiwa ni miongoni mwa miradi itakayo kuwa na Tija ya moja kwa moja kwa wanachi kutokana na adha waliyoipata ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa muda wa miezi 8 kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi ambapo mpaka hivi sasa imesalia miezi miezi 2 kumalizika kwa muda uliotengwa ili wananchi kuanza kuifurahia halmashauri yao.

Viongozi hao wa Halmashauri ya wilaya kilolo walisema kutokana na Jografia ya wilaya hiyo changamoto kubwa ni namna wananchi wanavyoweza kupata huduma za afya hususani wakazi wa vijiji vya Kiwalamo na Ruaha Mbuyuni ambapo walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kuitafuta huduma hiyo huku baadhi ya wananchi wakipoteza ndugu zao wakiwa njiani kufuata huduma za afya ambapo hivi karibuni itabaki historia.

“hapo awali wananchi wa kilolo wamepata shida sana pale wanapopata maradhi hasa wanawake wajawazito waliokuwa wanahitaji huduma ya dharura(upasuaji)kwa kuwa katika Halmashauri yetu hatukuwa na hospitali kubwa walilazimika kwenda Iringa mjini katika hospitali ya Rufaa au kwenda katika hospitali Teule ya Ilula jambo lililosababisha baadhi ya akina mama na watoto kupoteza maisha wakiwa njiani tulikuwa hatuna namna”.walisema viongozi hao

“wanaendelea kusema kwasasa tunao mradi mkubwa wa ujenzi wa hospitali unaogharimu kiasi cha shilingi billion 4.2 hii itakuwa hospitali ya mfano kwani tunamajengo matano ya Ghorofa moja moja yanaendelea kujengwa hisa sasa yanakaribia kuanza shughuli za upauaji na kufikia mwezi wa nane tunaweza kuwa katika hatua ya umaliziaji na wananchi wataanza kufurahia upatikanaji wa huduma za afya na itasaidia sana kupunguza foleni katika hospitali za Rufaa na Hospitali ya Manispaa ya iringa.”walisema

Akizungumzia ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya kilolo Valensi Kihwaga alisema Halmashauri imeendelea na uelimishaji wa wananchi katika kutambua umuhimu wa miradi iliyopo ili waweze kuisimamia na kiutumia ipasavyo huku akiwataka waendelee kuonesha ushirikiano kwa serikali katika kutekeleza miradi hiyo.

“mimi nisema tu Halmashauri yetu imedhamiria kumaliza kero za wananchi kwa kiasi kikubwa na hasa kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe na tumeendelea kutoa elimu ya kutosha kwao ili wao ndiyo wawe wamiliki wa miradi ya maendeleo hasa hii Hospitali kubwa ambayo tunaijenga kama serikali tutahakikisha tunasimamia na kukamilisha kwa wakati ujenzi wake na ianze kutoa huduma”alisema kihwaga

Halmashauri ya Kilolo kwa ujumla imekusudia kupunguza kero za huduma za Jamii kwa wananchi ikiwemo miradi ya barabara,Maji na Elimu ili kufanya wilaya hiyo ikue kiuchumi.

WAKAZI WA MTAA WA TAGAMENDA MANISPAA YA IRINGA MIAKA 3 WAKOSA HUDUMA YA MAJI SAFI YA KUNYWA

Wananchi wa mtaa wa Tagamenda katika manispaa ya Iringa wamelalamikia adha ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama ya kunywa kwa kipindi cha miaka 3 huku uongozi wa serikali ya manispaa hiyo ukishindwa kutatua changamoto hiyo jambo linalosababisha wananchi hao kufuata maji katika mto ruaha na kuhatarisha maisha yao.

Wakizungumza na SAYARI YA HABARI iliyofika mtaani hapo na kukutana na baadhi ya wananchi wanaokubwa na adha hiyo ambapo wamelalamikia kutelekezwa na serikali huku wakipigwa porojo ya kutatuliwa kwa kero hiyo walisema wamekuwa wakitafuta maji katika mtoRuaha ambapo maji hayo hutumiwa na wanayama,Kuoga,kufua huku yakitumiwa kwa kunywa binadamu huku vitendo vya kubakwa na kufanyanyiwa kuatili vikitishia maisha yao jambo lililowalazimu wanaume kuanza kuwasindikiza wake zaokutafuta maji.

Sara Edoga ni miongoni mwa Wakazi hao ambao wamekuwa wakipata adha na usumbufu mkubwa kwa kufuata maji na kutumia kutoka mto wa Ruaha alisema amekuwa akibeba maji mgongoni kutokana na umri wake kuwa mkubwa hali inayomfanya ashindwe kujitwisha kichwani na ndipo akapaza sauti.

“hapa tunashida ya maji na Umeme kwa zaidi ya miaka 3 tunatumia maji ya mto Ruaha tunatia huruma tumetelekezwa kama kisiwa kwa umri wangu nalazimika kubeba mgongoni maji wakati yamepita hapo chini shule ya Sekondari Tagamenda tuoneeni huruma mbona tupo manispaa”alisema mama huyo kwa huruma

Naye Willium Fungo ni mzee wa mtaa huo kwa uchungu alisema kumekuwa na kauli za baadhi ya viongozi wanaosema eneo la Mtaa wa Tagamenda ni eneo la milimani hivyo hawawezi kupatiwa huduma ya maji jambo linalowafanya wajiulize maswali iweje kauli hizo ikiwa kodi za majengo zinatozwa?akaongeza kusema kasi ya ukuji wa mtaa huo ni kubwa wapo karibu na kituo cha Shirika la Umeme TANESCO lakini hawana pia umeme jambo linalowakatisha Tamaa kushiriki katika shughuli za maendeleo.

“hatuna maji,hatuna Umeme zote ni shida zetu zinatukabili,sasa kuna utaalamu fulani um ekuja wa kusema tuweke maji chooni hivi utaweka maji wakati hayapo na msishangae kuja hapa mnakuta watoto wachafu yote hii ni kwa sababu ya kukosa maji tunateseka sana heri tukose chakula lakini tupate maji safi ya kunywa”alisema mzee huyo

Kwa upande wao baadhi ya Madiwani Dora Nziku vitimaalum ,Bashir Mtove na Mahadhi Hepautwa walizuru katika mtaa huo ili kujionea adha wanayoipata wananchi hao wamesema richa ya mateso na shida wanazozipata za kukosa maji lakini wao kwa umoja wao wamewahakikishia kushughulikia kero hiyo ili kuwaokoa wanawake na vitendo viovu.

“nikweli sisi ni madiwani kutoka kata tofauti tofauti mara baada ya Kusikia kilio cha wananchi hawa ambao ni walipakodi katika Manispaa yetu Tumeamua kufika ili tujionee wenyewe na tuchukue hatua ya kuwasaidia tumeo hali hii siyo nzuri hata kidogo wapo kama kisiwani tuwaahidi wananchi hawa kuwa kero hii sasa imefika mwisho” walisema

Hatimaye Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Iringa Rita Kabati akajitokeza na kuzungumzia changamoto hiyo huku akishangazwa na kauli za baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakidai kuwa katika manispaa ya Iringa hakuna Tatizo la ukosefu wa huduma ya maji na kuwaahidi kuitatua kero hiyo katika kipindi cha muda mfupi ujao.

“nimekuja huku kwa masikitiko makubwa kwani ninaposikia kero ya maji naumia ninapomuwazia mwanamke mwenzangu anayepata adha na kodi analipa na anakabiliwa na vitendo vya ubakaji kwa kufuata maji umbali mrefu imeniuma sana kwanini tunawadanganya wananchi waendelee kupata shida hizi mimi kama kiongozi naanza leo kufuatilia kero hii hapa mnahaki ya kupata maji kama wanavyopata watu wengine mnayo haki ya kupata umeme tena kwakuwa upo karibu hapa.”alisema Kabati


Mtaa wa Tagamenda una zaidi ya kaya 30 na upo umbali wa kilomita 2 kutoka kilipo kituo cha mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iruwasa na mita 800 kilipo chanzo cha umeme wa TANESCO cha Tagamenda lakini mtaa huu hauna maji wa Umeme hali inayowapa shida wananchi na kuwa hatarini kuugua maradhi kutokana na kutumia maji yasiyo salama.

Jumapili, 25 Juni 2017

SAYARI YA HABARI TUWATAKIA WAISLAMU WOTE EID MUBARAK

Image result for eid mubarak
Leo ni siku muhimu nkwa waumini wa Dini ya Kiislamu Duniani kote ambapo mara baada ya kushiriki katika mwezi wa kujiweka karibu na Mungu na kutafakari ukuu wake katika maisha yetu hatimaye leo tumefika salama na kufungua salama.

Kwaniaba ya watanzania wote mtandao wa Sayari ya Habari tunapenda kuwatakia Waislamu wote EID MUBARAK tusherehekee sikuu hii kwa Amani na Furaha tukiendelea kutafakari maisha yetu na namna tunavyozitumia Nafasi zetu katika kujiletea Maendeleo yetu na Taifa Kwaujuml

TUNAKUTAKIA SIKUU NJEMA

VIONGOZI WA DINI NA SERIKALI WAHIMIZWA KUWA NA UZALENDO NA NCHI YAO

  • Acheni kuwatisha wananchi kuweni na Unyenyekevu
  • Suala la kodi katika mashirika ya Dini kikwazo na mzigo kwa uendeshaji wa huduma
  • Serikali iendelee kuwatumikia wananchi kwa misingi ya sheria 
Askofu Dkt Fredlick Shoo Mkuu wa Kanisa KKKT

Askofu wa Dayosisi ya Iringa Braston Gavile(kulia)na Msaidizi wa Askofu Hamidu Saga(kushoto)

Maaskofu waliohudhuria Ibada ya Kuwekwa wakfu Askofu mpya Dayosisi ya Iringa Mch Braston Gavile

Jamuhuri Wiliumu Mkuu wa Wlaya ya Mufindi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa


Viongozi wa Dini na Serikali nchini wametakiwa kuwa na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua wala kutangukiza masilahi yao jambo linaloweza kuwagawa watanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Askofu Dkt Fredrick Shoo wakati wa ibada ya kumumweka wakfu na kumuingiza  kazini Askofu Mpya wa Dayosisi ya Iringa ambapo amesema ni vema kila kiongozi akatumia madaraka yake kwa kuwatumikia wananchi badala ya kutumia vitisho na kutumia mamlaka yao vibaya jambo linaloshusha heshima kwa viongozi kutokana na matendo yao.

“ndugu zangu viongozi wa kiroho na seriakli mliopo hapa tumepewa mamlaka kuwaongoza watanzania siyo kwa kuwatisha bali ni kwa unyeyekavu ili tuwasaidie watambue uhuru wao heshima ya kiongozi yeyote itakuja kwajinsi ulivyowatimikia watu wa Mungu,Mungu amekupa nafasi hiyo ili uwatumikie watanzania ili tuiinue nchi yetu taifa letu lisonge mbele kimaendeleo”alisema Askofu Shoo

Aidha Mkuu huyo wa Kanisa hakusita kuwanyoshea kidole baadhi ya viongozi wanaotumia nafasi zao kwa kujinufaisha wenyewe  badla ya kujali masilahi mapana ya nchi na kuendelea kuona wao ni zaidi kuliko watu wengine hivyo amewataka viongozi wa serikali na Dini nchini kuwa na uzalendo na nchi yao.

“yapo mambo ya aibu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi waliolitumikia Taifa hili  badala ya kufanyakazi ili watu wote wanufaike unakaa kusaini mkataba ambao unaiumiza nchi yako unajiita umesoma hebu tuipende nchi yetu badala ya kuuza nchi kwa masilahi binafsi na kuingia mikataba na mabeberu wa nje.”alisisitiza Shoo

Akizungumza mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Iringa Mch Braston Gavile richa ya kupongeza kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya Tano hakusita kuzungumzia kilio cha Taasisi za dini kutokana na tozo la Kodi katika huduma wanazozitoa ikiwemo Afya na Shule kuwa zimekuwa zikitozwa kodi kubwa bila kutambua taasisi hizo hazifanyi  biashara bali zinatoa huduma.

“taasisi za dini zinashindwa kuendelea kutoa huduma kutokana na kodi zimezidi ikumbukwe kuwa taasisi hizi hazifanyi biashara bali zinatoa huduma tunaomba seriakali yetu iangalie kwa upya suala la kodi nchini  kwa mashirika ya Dini kwamaana kodi hizo zimekuwa mzigo mkubwa katika uendehaji wa huduma hizo”alisema Askofu Gavile
Jamuhuri Wilium ni mkuu wa wilaya ya Mufindi akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa amesema serikali inayoimani kubwa kwa makanisa kwa kazi ya kutoa mafundisho na kukemea maovu jambo linalofanya kuongeza ushirikiano baina ya mihimili hiyo miwili ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Dini kuendelea kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Tanzania ili aendelee kuwatumikia watanzania na kutetea rasilimali za nchi,

“serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za Dini kwani tunatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizi tunakupongeza Baba Askofu kwa kuaminiwa na leo unaanza kuwatumikia wananchi rasmi mimi niseme tuiunge mkono serikali na tuiombee ifanye vizuri katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.”alisema mkuu wa wilaya 

Kanisa la Kiinjili Tanzania ni miongoni mwa makanisa yenye waumini wengi ambapo kwasasa lina jumla ya waumini zaidi ya million 6.7 ambapo wameaswa kuendelea kujituma kufanya kazi ili kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla.

MCHUNGAJI BRASTON GAVILE ASIMIKWA RASMI KUWA ASKOFU WA DAYOSISI YA IRINGA KKKT

Askofu Braston Gavele akiwa katika kiti cha Askofu kuanza kazi rasmi kuiongoza Dayosisi ya Iringa
Wakuu wa wilaya Kilolo,Mufindi na Iringa wakijadili Jambo katika Ibada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Iringa

Askofu Mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na Katibu mkuu wa Dayosisi hiyo Nayman Chavala wakimkabidhi Hati ya Uaskofu Askofu mpya Braston Gavile


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt Frederick Shooakimwingiza kazini Askofu Gavile
 Hatimaye Dayosisi ya Iringa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT imeingia rasmi katika ukurasa mwingine mara baada ya kuapishwa na kuingizwa rasmi Askofu Mpya wa Dayosisi hiyo Mch Braston Gavile ambaye naye amemuapisha mch Himidu Sanga kuwa msaidizi wa Askofu katika
kanisa hilo.

Ibada ya kuwekwa wakfu kwa mchungaji Braston Gavile imehudhuriwa na waumini wa kanisa hilo kutoka maeneo Tofautitofauti katika mkoa wa Iringa,viongozi wa serikali na Maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi.

Miongoni mwa shughuli zitakazofanywa na Askofu Huyo ni pamoja na kusimamia shughuli zote na huduma katika Dayosisi,kuwa msemaji mkuu wa Dayosisi kwa Serikali,Kushiriki katika mkutano mkuu wa Dayosisi kama mwenyekiti,Kuidhinisha kusimamishwa kazi kwa mtumishi yeyote atakyefanya kinyume na Taratibu na mengineyo.

ENDELEA KUWA NASI TUTAKUJUZA YOTE YANAYOENDELEA

IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILE DAYOSISI YA IRINGA



 Waumini wa kanisa la kiinjili Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa wameungana pamoja katika viwanja vya Shule ya msingi Gangilonga kumpokea Askofu Mpya wa Kanisa hilo Mch Blaston Gavile ili kuanza kuongoza Rasmi kanisa hilo huku Ibada hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Kanisa KKKT  Askofu Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella.

Askofu Mteule Gavile anachukua mikoba inachwa na Askofu Owdenburg Mdegella aliyeongoza Dayosisi hiyo kwa zaidi ya miaka 30 ambapo Askofu Mdegela katika kipindi cha uongozi wake amefanikisha kuanzisha miradi mbalimbali ili kulifanya kanisa hilo liweze kujiendesha lenyewe pasipo kutegemea ufadhiri hii inatajwa kuwa ni miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata katika uongozi wake huku waumini wa kanisa hilo wakisubiri kuona mabadiliko makubwa zaidi kutoka kwa Mch Gavile.


Endelea kutufuatilia tukujuze kila kinachojili.