sikiliza na tazama nyimbo kali hapa
Ijumaa, 14 Agosti 2015
Jumatatu, 29 Juni 2015
ZAIDI YA MIL 400 KUTOKA HIFADHI YA RUAHA ZATUMIAKA KATIKA KUJENGA MIRADI YA UJIRANI MWEMA IRINGA VIJIJINI.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisaini baada ya kuwasili ktk shule ya Sekondari Willium Lukuvi kupokea jengo jipya la Bweni la wasichana. |
![]() |
| Dk Christopher David Timbuka Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Nation Park akiwasilisha ripoti ya Ujenzi wa Bweni Pawaga mbaele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza. |
![]() |
| Viongozi mbalimbali walioongozana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakikagua Jengo la Bweni katika shule ya Sekondari ya Willium Lukuvi lililoteketea kwa moto hivi karibuni. |
![]() |
| Bweni jipya la wasichana Shule ya sekondari Willium Lukuvi baada ya moja kuteketea kwa Moto hivi karibuni. |
![]() |
| Baadhi ya Wananchi waliohudhulia Katika makabidhiano ya Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Idodi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk Christopher Timbuka leo. |
![]() |
| Makabidhiano Baina ya Mkuu wa Mkoa na uongozi wa Tanapa na Serikali. |
![]() |
| Picha ya Pamoja |

![]() |
| Wanafunzi wa Shule ya Msingi Malengamakali wakishuhudia makabidhiano ya Nyumba ya walimu wa shule hiyo. |
![]() |
| Mh.Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha DK Christopher Timbuka wa fungua nyumba ya walimu Malengamakali. |
![]() |
| Hii ni Nyumba ya Polisi Idodi i;iyojengwa Kupitia Mradi wa Ujirani Mwema kupitia TANAPA |
“Wote tuhifadhi na tulinde hifadhi yetu ya Taifa ya
Ruaha kwani ni fahari na Urithi wetu wa watoto na watoto wetu”ni kauli
iliyotolewa na wananchi wa wilaya ya Iringa kuonesha furaha yao Baadha ya
Shirika la Hfadhi ya Taifa TANAPA kupitia mradi wake wa Ujirani mwema na vijiji
vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya kuujenga Bweni la wasichana
Katika shule ya Sekondari Willium Lukuvi iliyopo pawaga,Nyumba ya Polisi
iliyopo kata ya idodi na shule za walimu mbili ambazo zamejengwa na mradi huo
kwa kuthamini jitihada za wananchi Katika kulinda Hifadhi ya Ruaha.
Nyumba hizo mbili za Walimu moja imejengwa Katika kijiji
cha Malenga makali kata ya Idodi na nyingine imejengwa Katika kijiji cha Kipera
iliyopo kata ya Nzihi-kipera jimbo la Kalenga ambapo zaidi ya mil 420
zimetumika Katika shughuli hiyo.
Akizungumza wakatika wa kukabidhi nyumba hizo Mkuu
wa Hifadhi ya Ruaha kwaniaaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA,Dk Christopher David
Timbuka amesema Tanapa kwa kutambua mchango wa wananchi Katika kulinda na kutetea
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha walionana ni vyema kurudisha fadhira kwa kuchangia
badhii ya shughuli za maendeleo hivo wameona na vyema kujenga nyumba za walimu Katika
maeneo hayo ili kuwapunguzia mzigo wa michango ambapo amesema TANAPA ilikuwa
ikichangia kiasi 70% ya mradi na wananchi
% zinazosalia.
“Hifadhi ya Ruaha kupita mradi wake wa Ujirani mwema
tumewazesha ufanikishaji wa ujenzi wa nyumba hizi kwa kushirikiana na wananchi
wa maeneo husika ambapo hifadhi tulitumia asilimia 70% na wananchi
zilizosalia,tumetumia zaidi ya mil 400 katika miradi yote”alisema Timbika
Dk Timbuka Amesema ushirikiano huo uliopo baina ya
wananchi na Hifadhi hiyo ndiyo uliosababisha kufanikiwa kwa miradi hiyo mikubwa
ambayo imekuja kwaajili ya kuwanufaisha wananchi hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuunga
mkono juhudi wanazozifanya kwa maendeleo yao na vizazi vijavyo.
Dk Timbuka alisema “tunawaomba wananchi kuendelea
kusaidiana na Hifadhi ya Ruaha Katika ulinzi wa hifadhi dhidi ya majangili ili
iendelee kuwanufaisha Katika masuala ya kimaendeleo”
Akipokea na Kusaini hati ya makabdhiano ya miradi
hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina masenza ameipongeza Hifadhi hiyo kwa kuona
umuhim wa kujihusisha na masuala ya kijamii hususani Katika kuwasaidia wananchi
suala la michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ambapo pia itasaidia kupunguza
kero za walimu vijijini.“niseme jambo moja nimekubalikupokea miradi hii
ikiwa imekamilika Katika ubora wake ambapo nimeona nyumba za walimu za kisasa
zaidi sana mmenisaidia kupunguza kero kwa wanafunzi wa kike Katika shule ya
sekondari ya Willium Lukuvi pale pawaga baada ya bweni lao kuungua kwa moto hivyo
leo mkaona mtukabidhi baada ya kukamilisha ujenzi,”alisema mkuu wa Mkoa
Aidha Mh.Masenza amewataka wananchi wa wanaoishi
kuzunguka hifadhi au maeneo yaliyohifadhiwa badala ya kukaa kimya mnapoona kuna
uharibifu unatokea kwani kwa kufanya hivyo majangili watabeba rasilimali
zilizopo ambazo zingewasaidia Katika shughuli za mendeleo pia amewataka kutunza
miradi hiyo ya majengo ili yaweze kudumu hivyo ameziagiza kamati za shule
kuwaondoa wale wote wasio na mapenzi mema ili na miradi hiyo ili kuwapawengine
watakaoweza kusimamia ipasavyo kwa faida ya wengine wao.
Akishukuru kwa niaba ya viongozi wa vijiji
vilivyonufaika na miradi hiyo mwenyekiti wa kijiji cha kipera Bw Francis Yangi
ameupongeza uongozi mzima wa hifadhi ya Ruaha kwa mchango walioutoa kupitia
Ujirani mwema hivyo ameahidi kusimamia ushirikiano zaidi hususani Katika ulinzi
wa hifadhi na uhifadhi.
Jumatatu, 8 Juni 2015
UVCCM IRINGA KUSAIDIA JITIHADA ZA SERIKALI KUHAMASISHA VIJANA KUJIARI NA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.
katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi wa pili kulia akiwa na katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda.
|
Vijana nchini
hususani mkoani Iringa wameshauriwa kujiandaa na kujiweka sawa katika kupambana
na changamoto za ugumu wa maisha kwa kuchangamkia furusa mbalimbali
zinazojitokeza na kujiajiri wenyewe.
Kauli hiyo imekuja
baada ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na kuonesha kuwa vijana wengi wamekuwa
na mitazamo ya kusubiri serikali iwaletee badala ya kufikiri zaidi namna ya
kujitengenezea ajira zitakazo waletea kipato na kuboresha maisha yao hali
ambayo imeendelea kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Akitoa tathimini ya
kikao cha Baraza la vijana mkoa wa
Iringa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Bw Elisha
Mwampashe amewataka vijana wafanye kazi ili wasiendelee kuilamu serikali.
“ninawaomba vijana
ifike wakati tujitambue na tuone jukumu la kujiletea maendeleo katika familia
zetu tusiwe watu wa kulaumu tu badala kuwa na mawazo chanya kujishughulisha na
shughuli zitakazotuletea maendeleo ili hata kama kuna mkono wa serikali kusaidia
jitihada zetu utukute tukiwa tayari tuna mambo tunafanya” alisema mwampashe
Aidha alisema maadhimio ya vijana wa chama cha
mapinduzi katika kikao hicho ni kutoa
elimu kwa vijana itakayowasaidia kutumia changamoto zilizopo kuwa fulsa
zitakazo waingizia kipato pia ameeleza maadhimio mengine kuwa ni kuwatembelea
vijana na kubaini changamoto zinazowakabili na kutafuta namna ya kuzimaliza
mengine ni kusaidia katika shughuli za kijamii ambapo mapema mwezi huu
wanatarajia kuweka kambi ya pamoja kwaajili ya kufyatua tofari na kuanza ujenzi
wa Bweni la shule ya sekondari Idodi lililoteketea kwa moto hivi karibuni kama
vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa iringa ili kupunguza nguvu ya wananchi
katika kuchangia ujenzi huo.
“tumefanya kikao
cha baraza la vijana wa Chama Cha Mapinduzi na tumejadili na kuadhimia mambo
mengi ambayo tunaamini tutayasimamia na kuyatekereza kama vijana tumeadhimia
kuwafikia vijana wengi ili kuangaliachangamoto zinazowakabili na tuone namna ya
kuzitatua na vijana wenyewe kuhakikisha tunatengeneza vikundi vya
kiujasiliamali vitakavyotuwezesha kupata wafadhiri”.alisema
Hivyo Mwampashe amesema
wao kama vijana watahakikisha wanawafikia vijana wote wa mkoa wa iringa ili
kukumbushana wajibu wao katika kujiletea maendeleo na kutambua kuwa vijana
ndiyo nguvu kazi ya Taifa.
Mwampashe amesema
sio jambo jema kwa vijana wenye nguvu kushinda vijiweni wakizungumza siasa na
kucheza bao wakati wenzao wakiwa katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
“tumepita katika vikundi kadhaa hapa
mkoani na tayari tumekutana na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na
ujasiliamali tumezungumza nao tumewapa elimu na baadhi ya vitendea kazi kama
mashine ya ufyatuaji tofari na kuwahamasisha umoja kwa mustakabari wa maisha
yao kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya vijana wanaokaa vijiweni bila kazi yoyote
na kuilamu serikali jambo ambalo halina
manufaa yoyote kwao”.alisema mwampashe katibu wa vijana
Alisema duniani
kote hakuna serikali inayoweza kuajiri kila mtu mwenye uwezo na sifa za kufanya
kazi na akazungumzia umuhimu wa sekta binafsi katika kushughulikia changamoto
ya ajira kwa vijana.
Akizungumzia
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka hu, Mwampashe amewataka wanawake kuondoa hofu na
kujitokeza kwa wingi kushindana na wanaume katika nafasi mbalimbali za uongozi
zinazogombewa.
Pamoja na wanawake,
amewasishi vijana wenye sifa kutupa karata zao katika uchaguzi huo huku
akiwataka wajiandikishe kwa wingi na kushiriki kikamilifu kuchagua viongozi
bora wanaojali matatizo yao.
Alhamisi, 4 Juni 2015
WANANCHI WA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI WAMPOKEA EXAUD KIGAHE KUWA MGOMBEA UBUNGE ENDAPO ATAPITISHWA KUGOMBEA
EXAUD KIGAHE AGOMBEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI.
![]() | |
| Exaud Kigahe Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini |
Ikiwa mchakato wa kutangaza nia ya kugombea Ubunge
na Urais hapa nchini unaendelea jamii imetakiwa kuwachagua watu wenye nia ya
dhati ya kuwaletea maendeleo chanya katika maeneo husika.
Hayo yamesemwa na Mdau wa maendeleo wilayani Mufindi
Bw Exaud Kigahe wakati akizungumza na wandishi wa habari Mjini mafinga
wailayani Mufindi Mkoani Iringa wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge
katika Jimbo la Mufindi kasikazini ambapo amesema ni vyema na wakati umefika
kwa wananchi kuwachagua viongozi wenye uwezo na uzalendo wanaoweza kushirikiana
nao katika kuleta maendelaeo.
“ni ukweli usiopingika kwamba wakati wa viongozi
kuwarubuni wananchi umekwisha ninahakika kwamba Mufindi ninaijua vizuri sana
yale maisha wanayaishi wananchi wale siyo ndiyo waliyotakiwa kuishi nimekuja
kushirikiana nao tuondoe tatizo la umaskini kikubwa nikipewa ridhaa kwangu
wajibu wangu ni kuwaletea maendeleo wananchi” alisema Kigahe
Bw Kigahe amesema mtazamo wa sasa katika kusimamia
shughuli za maendeleo zinatazamwa zaidi kwa viongozi ambapo anapotokea kiongozi
ambaye hana uwezo hakuna maendeleo yatakayopatikana kwa wakati hivyo amesema
endapo atapata nafasi ya kuongoza jimbo hilo kuna mambo lukuki anayoyaona
yakitumika kama furusa kwa wananchi wa Mufindi yatawapa maendeleo kwa kasi
wananchi hao.
Amesema wilaya ya Mufindi ni miongoni mwa wilaya
zenye raslimali za kutosha ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikituwa na wageni
huku wazawa wakibaki kuwa walinzi jambo ambalo amesema kusingekuwa na maendeleo
hata kwa miaka ijayo bali kwa kutumia rasilimali hizo atahakikisha
anawaunganisha wananchi kwa ushirikishaji wa mambo yote ya maendeleo kwa faida
ya wanamufindi wenyewe.
“rasirimali zilizopo ninaamini zinatosha sana
kutuletea maendeleo wanamufindi ninachokifahamu kwa mufindi na kwamba tuna
misitu lakini kutokana na uongozi kutotujali wamekuwa wakitumia watu wa maeneo
mengine nadhani muda wa wananchi kutumia misitu yao umewadia nitafurahi nao na
kulia nao” alisema
Pia Kigahe amesema inasikitisha kuona rasirimali
kama misitu inavunwa na watu wa nje na wenyeji wakibaki maskini jambo ambalo
haliwezi kuvumilika,amesema wilaya ya Mufindi ina ardhi ya kutosha ambayo kwa
kiasi kikubwa haiwanufaishi wanamufindi.
Hivyo amewataka wananchi kwasasa wasidanganyika na
watu wanakuja wakiwa hawana malengo mema na wananchi bali wanahitaji
kujinufaisha wenyewe bali sasa amekuja kwaajili ya kushirikiana nao kuiondoa
hali hiyo.
“kwa upande
wangu ninaamini kwamba wanamufindi wanahitaji mambo makubwa machache tu ambayo
nikipata ridhaa na wakati maalumu ukifika nitawaeleza na namna tutakavyo weka
mikakati ya maendeleo mimi ninauchungu na maisha yale wanayoishi mama zetu,baba
zetu hata wadogo zetu naomba wanipokee tuyamalize hayo” ni maneno ya Kigahe
Jimbo la Mufindi Kaskazini lenye kata 11 za Ikweha, Sadani, Igombavanu, Ifwagi, Mdabulo, Ihalimba, Kibengu, Mapanda, Mpanga Tazara, Ihanu na Ikongosi, Jimbo la Mufindi Kusini litakuwa na kata 14 za Kiyowela, Makungu, Mninga, Kasanga, Igowole, Mtambula, Itandula, Mbalamaziwa, Idunda, Mlangali, Nyololo, Ihowanza, Mtwango na Luhunga:
Jimbo la Mufindi Kaskazini lenye kata 11 za Ikweha, Sadani, Igombavanu, Ifwagi, Mdabulo, Ihalimba, Kibengu, Mapanda, Mpanga Tazara, Ihanu na Ikongosi, Jimbo la Mufindi Kusini litakuwa na kata 14 za Kiyowela, Makungu, Mninga, Kasanga, Igowole, Mtambula, Itandula, Mbalamaziwa, Idunda, Mlangali, Nyololo, Ihowanza, Mtwango na Luhunga:
Jumatano, 3 Juni 2015
Itazame familia hii iliyotembelewa na Mbunge wa Vitimaalum Ritta Kabati wote wakiwa walemavu.
WANANCHI NA VIONGOZI WAMPONGEZA MBUNGE WA VITIMAALUM KWA JUHUDI ZAKE KATIKA KUPIGANIA MAENDELEO IRINGA.
![]() |
| Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Ritta Kabati alipotembelea familia ya watu watano wote wakiwa walemavu na wanaishi mazingira magumu Wilayani kilolo ambapo aahidi kuwajengea Nyumba ya Kisasa. |
Zikiwa zimebaki siku kadhaa
kumalizika kwa kipindi cha Uongozi wa wabunge hapa nchini hususani wabunge wa
Viti maalumu ambao wanatarajia kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo wananchi
na viongozi mkoani Iringa wampongeza Mbunge wa Viti maalumu Ritta Kabati.
Wakizungumza na Morning star redio
kwa nyakati tofauti wananchi hao wamempongeza Mh.Kabati kwa mchango wake kwa
jamii ya mkoa wa Iringa na kuonyesha moyo wa upendo na kuthamini ubora wa
maisha ya wanairinga wote bila kujali itikadi ya dini,siasa wa rangi ambapo
amekuwa akipigania maendeleo ya watu wa rika zote.
Wananchi hao wamemtaja Mbunge Kabati
kuwa ndiye kiongozi wa kuigwa na viongozi wengine kwa kuwa amekuwa amefanikiwa
kusemea vema mkoa wa Iringa na kutoa kero za wananchi bungeni bila woga na
kuifanya serikali kutekeleza kwa kuzingatia mchango wake.
Wakizitaja baadhi ya kazi
alizozifanya Mh.Kabati kuwa na pamoja na
kulipigania suala la haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume,suala la kuwapa
elimu watoto wa kike ukizingatia katika ofisi ya mbunge huyo imekuwa ikisaidi
watoto wasiojiweza waliohitimu kidato cha nne kwa kuwatafutia vyuo mbalimbali
jambo ambalo limewafanya zaidi ya watoto elfu 15 kuendelea na masomo.
Aidha wamesema amekuwa akipigania
suala la miundombinu pamoja na afya ambapo kupitia jitihada zake zimesaidia
kuboresha wodi za wazazi katika Hospital ya wilaya ya Iringa sambamba na hilo
amejenga kituo cha polisi kwa ghalama ya Sh mil 45 kilichopo Semtema manispaa
ya Iringa.
Kwa upande wa viongozi akiwemo Meya
wa Halmashauri ya Iringa Amani Mwamwindi,Katibu wa CCM mkoa Hasani mtenga na
mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoani Iringa Wamempongeza kwa jitihada za
kuwezesha eneo la kihesa kilolo kuwa eneo la uendelezaji kwa makazi badala ya
kuwa eneo la hifadhi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)




























