Jumapili, 25 Juni 2017

VIONGOZI WA DINI NA SERIKALI WAHIMIZWA KUWA NA UZALENDO NA NCHI YAO

  • Acheni kuwatisha wananchi kuweni na Unyenyekevu
  • Suala la kodi katika mashirika ya Dini kikwazo na mzigo kwa uendeshaji wa huduma
  • Serikali iendelee kuwatumikia wananchi kwa misingi ya sheria 
Askofu Dkt Fredlick Shoo Mkuu wa Kanisa KKKT

Askofu wa Dayosisi ya Iringa Braston Gavile(kulia)na Msaidizi wa Askofu Hamidu Saga(kushoto)

Maaskofu waliohudhuria Ibada ya Kuwekwa wakfu Askofu mpya Dayosisi ya Iringa Mch Braston Gavile

Jamuhuri Wiliumu Mkuu wa Wlaya ya Mufindi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa


Viongozi wa Dini na Serikali nchini wametakiwa kuwa na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua wala kutangukiza masilahi yao jambo linaloweza kuwagawa watanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Askofu Dkt Fredrick Shoo wakati wa ibada ya kumumweka wakfu na kumuingiza  kazini Askofu Mpya wa Dayosisi ya Iringa ambapo amesema ni vema kila kiongozi akatumia madaraka yake kwa kuwatumikia wananchi badala ya kutumia vitisho na kutumia mamlaka yao vibaya jambo linaloshusha heshima kwa viongozi kutokana na matendo yao.

“ndugu zangu viongozi wa kiroho na seriakli mliopo hapa tumepewa mamlaka kuwaongoza watanzania siyo kwa kuwatisha bali ni kwa unyeyekavu ili tuwasaidie watambue uhuru wao heshima ya kiongozi yeyote itakuja kwajinsi ulivyowatimikia watu wa Mungu,Mungu amekupa nafasi hiyo ili uwatumikie watanzania ili tuiinue nchi yetu taifa letu lisonge mbele kimaendeleo”alisema Askofu Shoo

Aidha Mkuu huyo wa Kanisa hakusita kuwanyoshea kidole baadhi ya viongozi wanaotumia nafasi zao kwa kujinufaisha wenyewe  badla ya kujali masilahi mapana ya nchi na kuendelea kuona wao ni zaidi kuliko watu wengine hivyo amewataka viongozi wa serikali na Dini nchini kuwa na uzalendo na nchi yao.

“yapo mambo ya aibu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi waliolitumikia Taifa hili  badala ya kufanyakazi ili watu wote wanufaike unakaa kusaini mkataba ambao unaiumiza nchi yako unajiita umesoma hebu tuipende nchi yetu badala ya kuuza nchi kwa masilahi binafsi na kuingia mikataba na mabeberu wa nje.”alisisitiza Shoo

Akizungumza mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Iringa Mch Braston Gavile richa ya kupongeza kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya Tano hakusita kuzungumzia kilio cha Taasisi za dini kutokana na tozo la Kodi katika huduma wanazozitoa ikiwemo Afya na Shule kuwa zimekuwa zikitozwa kodi kubwa bila kutambua taasisi hizo hazifanyi  biashara bali zinatoa huduma.

“taasisi za dini zinashindwa kuendelea kutoa huduma kutokana na kodi zimezidi ikumbukwe kuwa taasisi hizi hazifanyi biashara bali zinatoa huduma tunaomba seriakali yetu iangalie kwa upya suala la kodi nchini  kwa mashirika ya Dini kwamaana kodi hizo zimekuwa mzigo mkubwa katika uendehaji wa huduma hizo”alisema Askofu Gavile
Jamuhuri Wilium ni mkuu wa wilaya ya Mufindi akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa amesema serikali inayoimani kubwa kwa makanisa kwa kazi ya kutoa mafundisho na kukemea maovu jambo linalofanya kuongeza ushirikiano baina ya mihimili hiyo miwili ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Dini kuendelea kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Tanzania ili aendelee kuwatumikia watanzania na kutetea rasilimali za nchi,

“serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za Dini kwani tunatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizi tunakupongeza Baba Askofu kwa kuaminiwa na leo unaanza kuwatumikia wananchi rasmi mimi niseme tuiunge mkono serikali na tuiombee ifanye vizuri katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.”alisema mkuu wa wilaya 

Kanisa la Kiinjili Tanzania ni miongoni mwa makanisa yenye waumini wengi ambapo kwasasa lina jumla ya waumini zaidi ya million 6.7 ambapo wameaswa kuendelea kujituma kufanya kazi ili kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni