Ijumaa, 23 Juni 2017

WATANZANIA WATAKIWA KULINDA AMANI NA UMOJA KATIKA TAIFA


Asiah Abdallah Mkuu wa Wilaya ya Kilolo

Bi Amina Masenza mkuu wa Mkoa wa Iringa akizungumza na umati wa watu walialikwa katika Futari
Richard Kasesela mkuu wa Wilaya ya Iringa
Jamuhuri Wilium Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Baadhi ya waalikwa katika Futari ya Mkuu wa Wilaya Kilolo


Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini wamemetakiwa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa jamii ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali katika kuliletea Taifa maendeleo.

Akizungumza katika Hafla ya futari iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo mkuu wa mkoa wa iringa Amina Masenza alisema katika baadhi ya maeneo kumeibuka Tabia ya baadhi ya watu kutumia kigezo cha Dini kufanya vitendo viovu ikiwemo utapeli jambo linalolenga kuchafua Uislamu huku akitumia nafasi hiyo kutoa wito kuiunga mkono serikali katika kuhakikisha inawaletea maendeleo ya kweli wananchi.

“niwaombe ndugu zangu waislamu tunapowaona watu tunaowatilia mashaka wanakuja katika maeneo yetu ya Ibada wakijifanya waislamu kumbe wanamambo yao wanafanya hebu tutoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwani uislamu utalindwa na waislamu wenyewe lakini pia ndugu zangu niwaombe tushirikiane na serikali katika kujiletea maendeleo”alisema mkuu huyo wa mkoa

Aidha katika hatua nyingine Masenza alitoa wito kwa wananchi kutunza chakula hususani katika msimu huu wa mavuno ambapo mara nyingi baadhi ya wananchi hutumia mazao yao kwa pupa na mwishowe hujikuta wameishiwa kabisa hivyo alisema ni vyema wananchi wakahifadhi chakula bila kusahau utunzaji wa mazingira hususani vyanzo vya maji kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

“nitoe wito kwa wananchi wote waone umuhimu wa kutunza chakula kwani tusipofanya hivyo tatizo la njaa litatumaliza wapo wenye tamaa ya fedha wanauza mazao yao bila kuweka akiba niwaase tunzeni chakula chakutosha kwaajili ya familia zenu lakini pia mkumbuke utunzaji wa mazingira hasa katika vyanzo vya maji ni muhimu kwasasa na baadae mazingira ni uhai”alisema Masenza

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Kilolo Asiah Abdallah akizungumza wakati akiwakaribisha wageni waliohudhuria hafla hiyo ya Futari hakusita kuwakumbusha watanzaniani kuwa nchi hii imepata Rais ambaye Mungu amemchagua jambo la msingi ni kumuunga mkono kwa kazi zake anazofanya maana wapo wanaombeza hivyo aliwataka watanzania kuwapuuza watu hao.

“kila analolipanga mungu lazima litimie Mwenyezi Mungu alipanga Tanzania kuanzia mwaka 2015/2020 tuwe na Rais shupavu John Pombe Magufuli na imekuwa hatuna budi kumuunga mkono kwa yote anayoyafanya kwa masilahi ya watanzania wote “alisema mkuu huyo wa wilaya

Naye Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jumuhuri Willium richa ya kuwataka wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu kutumia vyema mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani aliitaka jamii ijikite katika kuombea amani na umoja wa nchi yetu  hata mara baada ya kumaliza mufungo huo.

“ningependa sana tuutumie mwezi huu wa Ramadhani katika kujitafakari na kumurudia muumba wetu maana kwake ndiko tunakopata Amani tudumishe amani na upendo miongoni mwetu na jamii inayotuzunguka”alisema Jamuhuri

Lakini pia mkuu wa wialaya ya Iringa Richard Kasesela ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafula hiyo ambaye aliwataka waumini wa Dini ya Kiisilamu kutumia uislamu kwa kufanya matendo yanayompendeza Mungu kwani wapo wanaoamini kuwa na alama katika Paji la Uso ndiyo kipimo cha ukamilifu wake bali ni vile wanavyoenda.

Awali wakizungumza katika hafla hiyo Mashekhe wa Mkoa na Wilaya ya Kilolo Abubakari Chalamila na wameitaka seriakali kuwashirikisha katika utoaji wa matamko kwani ipo tofauti pindi tamko linapotolewa na Kiongozi wa Dini jamii huelewa zaidi kuliko linapotolewa na kiongozi wa kisiasa.

“kauli za viongozi wa Dini husikilizwa na huaminiwa zaidi kuliko kauli za wanasiasa tutumieni kwa kuwa yote yanayopigiwa kelele na serikali hii yapo katika vitabu vya mungu nasi tunao wajibu wa kukemea na kuonya pale mtu anapofanya kinyume na agizo la Mwenyezi Mungu hivyo tushirikiane kuijenga nchi yetu”walisema mashekhe

Ilielezwa kuwa miongoni mwa matendo yanayochochea umoja na Mshikamano miongoni mwa jamii ni pamoja kukaa pamoja kila mmoja akitafakari namna anavyoweza kulinda na kusimamia amani iliyopo kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaunganisha watanzania.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni