Wahariri wa magazeti ya Ujerumani(14.06.2017)wamejishughulisha
zaidi na mada kuhusu mkutano wa kilele kuhusu bara la Afrika, mkutano
wa mawaziri wa mambo ya ndani wa majimbo ya
Ujerumani kuhusu hali ya usalama.
Mada nyingine ni kuhusu jinsi alivyohojiwa mwanasheria mkuu wa
Marekani Jeff Sessions na kamati ya baraza la Seneti hapo jana.
Mada
kuhusu mkutano wa kilele kuhusu bara la Afrika uliomalizika
jana mjini Berlin hapa Ujerumani. Mhariri wa gazeti la Die
Rheipfalz anaandika kwamba , kwanini misaada ya maendeleo haileti
maendeleo? Mhariri anaendelea kuandika
"Ni
kwasababu , kwanza ; Ni wanasiasa pekee na wale wenye uwezo kiuchumi
ndio wanafaidika zaidi katika nchi hizo zinazopokea misaada. Kwa
wale mamilioni ya Waafrika ambao wakati wote wako katika hali
ngumu ya maisha hawapati chochote. Kwa upande wa nchi wafadhili ,
kitengo cha misaada ya maendeleo , ni chombo cha kujinufaisha.
Ndio sababu juhudi za Merkel zina kiini cha kushindwa, kwa kuwa
hazihusiani kabisa na maendeleo. Ukweli ni kwamba wanataka
kuwazuwia watu wanaotaka kuhama kutoka bara la Afrika kuja
Ulaya. Unaweza mtu kusema hilo, na Merkel anapaswa kusema hivyo
sio kujaribu kuleta matumaini ambayo hayapo."
Msingi wa hamasa mpya kuhusu bara la Afrika ni nyingine
kabisa, anaandika mhariri wa gazeti la Hannoversche Allgemeine
Zeitung kuhusiana na mkutano huo wa kilele kwa ajili ya bara
la Afrika. Mhariri anaendelea ....
"Ni kuhusu
kuzuwia uhamiaji. Waafrika hawatakiwi kuja kwetu, wanatakiwa
kutafuta kazi katika nchi zao na wabakie huko. Ndivyo
wanavyofikiri watu wa huku kaskazini. Utaratibu sio kuwakataa
kabisa , lakini umo katika makosa yetu. Ukuaji wa uchumi
hautazuwia uhamiaji, badala yake unahimiza. Waafrika wengi
wamehamia nchi za nje katika wakati wa ukuaji mkubwa wa uchumi
hivi karibuni kuliko wakati mwingine wowote. Ghana , Senegal ,
Nigeria, si kitu cha bahati mbaya kwamba watu wengi walioomba
hifadhi wanatoka nchi hizi zilizoneemeka. Masikini wengi hawana
fedha ama nguvu za kuweza kufanya safari za kuhamia nchi za
nje. Inahitaji zaidi ya ukuaji wa uchumi , kwa watu kubakia
katika nchi zao. Wakati kundi la G20 linalenga kuwekeza katika
sekta binafsi kama nguvu ya kuleta maendeleo katika bara la
Afrika, haina maana ya kuondoa kiini cha matatizo , ambayo ni
rushwa."
Kuhusu mada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa
serikali za majimbo nchini Ujerumani kuzungumzia kuhusu usalama
wa ndani kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Septemba , mhariri wa
gazeti la Stuttgarter Zeitung anaandika:
"Sheria
zilizopo za usalama haziwezi tena kuufanya ulimwengu kuwa salama.
Tunapata uzoefu huo na mawaziri wa mambo ya ndani kutoka
serikali kuu na za majimbo watakuwa waangalifu sana kuweza
kulichokoza suala hilo, kwa kuwa wakiamua kuleta sheria mpya
huenda wakawaweka wananchi katika hali ngumu. Ni somo pia
kutokana na tukio lililofanywa na mhamiaji Amri , ambaye kama sio
kushindwa kushindwa kwa maafisa wa usalama kumdhibiti mambo
yaliyotokea yasingetokea."

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni