Jumatatu, 29 Juni 2015

ZAIDI YA MIL 400 KUTOKA HIFADHI YA  RUAHA ZATUMIAKA KATIKA KUJENGA MIRADI YA UJIRANI MWEMA IRINGA VIJIJINI.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisaini baada ya kuwasili ktk shule ya Sekondari Willium Lukuvi kupokea jengo jipya la Bweni la wasichana. 
Dk Christopher David Timbuka Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Nation Park akiwasilisha ripoti ya Ujenzi wa Bweni Pawaga mbaele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza.
Viongozi mbalimbali walioongozana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakikagua Jengo la Bweni katika shule ya Sekondari ya Willium Lukuvi lililoteketea kwa moto hivi karibuni.
Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk Christopher David Timbuka (kushoto)akiwa na mkuu wa kitengo cha cha Uhifadhi na ujirani Mwema Bw Molondo wakiteta jambo nje ya Jengo jipya la bweni la wasishana Ktk shule ya Sekondari Willium Lukuvi Pawaga.
Bweni jipya la wasichana Shule ya sekondari Willium Lukuvi baada ya moja kuteketea kwa Moto hivi karibuni.
Baadhi ya Wananchi waliohudhulia Katika makabidhiano ya Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Idodi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk Christopher Timbuka leo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akisati hati za makabidhiano ya Miradi ya Nyumba ya Ujirani mwema zilizojengwa na Shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha DK Christopher Timbuka.

Makabidhiano Baina ya Mkuu wa Mkoa na uongozi wa Tanapa na Serikali.
Picha ya Pamoja

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Malengamakali wakishuhudia makabidhiano ya Nyumba ya walimu wa shule hiyo.
Mh.Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha DK Christopher Timbuka wa fungua nyumba ya walimu Malengamakali.
Hii ni Nyumba ya Polisi Idodi i;iyojengwa Kupitia Mradi wa Ujirani Mwema kupitia TANAPA
NA AGUSTINO KIHOMBO

“Wote tuhifadhi na tulinde hifadhi yetu ya Taifa ya Ruaha kwani ni fahari na Urithi wetu wa watoto na watoto wetu”ni kauli iliyotolewa na wananchi wa wilaya ya Iringa kuonesha furaha yao Baadha ya Shirika la Hfadhi ya Taifa TANAPA kupitia mradi wake wa Ujirani mwema na vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya kuujenga Bweni la wasichana Katika shule ya Sekondari Willium Lukuvi iliyopo pawaga,Nyumba ya Polisi iliyopo kata ya idodi na shule za walimu mbili ambazo zamejengwa na mradi huo kwa kuthamini jitihada za wananchi Katika kulinda Hifadhi ya Ruaha.

Nyumba hizo mbili za Walimu moja imejengwa Katika kijiji cha Malenga makali kata ya Idodi na nyingine imejengwa Katika kijiji cha Kipera iliyopo kata ya Nzihi-kipera jimbo la Kalenga ambapo zaidi ya mil 420 zimetumika Katika shughuli hiyo.

Akizungumza wakatika wa kukabidhi nyumba hizo Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha kwaniaaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA,Dk Christopher David Timbuka amesema Tanapa kwa kutambua mchango wa wananchi Katika kulinda na kutetea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha walionana ni vyema kurudisha fadhira kwa kuchangia badhii ya shughuli za maendeleo hivo wameona na vyema kujenga nyumba za walimu Katika maeneo hayo ili kuwapunguzia mzigo wa michango ambapo amesema TANAPA ilikuwa ikichangia kiasi 70% ya mradi na wananchi  % zinazosalia.

“Hifadhi ya Ruaha kupita mradi wake wa Ujirani mwema tumewazesha ufanikishaji wa ujenzi wa nyumba hizi kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika ambapo hifadhi tulitumia asilimia 70% na wananchi zilizosalia,tumetumia zaidi ya mil 400 katika miradi yote”alisema Timbika
Dk Timbuka Amesema ushirikiano huo uliopo baina ya wananchi na Hifadhi hiyo ndiyo uliosababisha kufanikiwa kwa miradi hiyo mikubwa ambayo imekuja kwaajili ya kuwanufaisha wananchi  hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi wanazozifanya kwa maendeleo yao na vizazi vijavyo.

Dk Timbuka alisema “tunawaomba wananchi kuendelea kusaidiana na Hifadhi ya Ruaha Katika ulinzi wa hifadhi dhidi ya majangili ili iendelee kuwanufaisha Katika masuala ya kimaendeleo”
Akipokea na Kusaini hati ya makabdhiano ya miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina masenza ameipongeza Hifadhi hiyo kwa kuona umuhim wa kujihusisha na masuala ya kijamii hususani Katika kuwasaidia wananchi suala la michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ambapo pia itasaidia kupunguza kero za walimu vijijini.“niseme jambo moja nimekubalikupokea miradi hii ikiwa imekamilika Katika ubora wake ambapo nimeona nyumba za walimu za kisasa zaidi sana mmenisaidia kupunguza kero kwa wanafunzi wa kike Katika shule ya sekondari ya Willium Lukuvi pale pawaga baada ya bweni lao kuungua kwa moto hivyo leo mkaona mtukabidhi baada ya kukamilisha ujenzi,”alisema mkuu wa Mkoa

Aidha Mh.Masenza amewataka wananchi wa wanaoishi kuzunguka hifadhi au maeneo yaliyohifadhiwa badala ya kukaa kimya mnapoona kuna uharibifu unatokea kwani kwa kufanya hivyo majangili watabeba rasilimali zilizopo ambazo zingewasaidia Katika shughuli za mendeleo pia amewataka kutunza miradi hiyo ya majengo ili yaweze kudumu hivyo ameziagiza kamati za shule kuwaondoa wale wote wasio na mapenzi mema ili na miradi hiyo ili kuwapawengine watakaoweza kusimamia ipasavyo kwa faida ya wengine wao.


Akishukuru kwa niaba ya viongozi wa vijiji vilivyonufaika na miradi hiyo mwenyekiti wa kijiji cha kipera Bw Francis Yangi ameupongeza uongozi mzima wa hifadhi ya Ruaha kwa mchango walioutoa kupitia Ujirani mwema hivyo ameahidi kusimamia ushirikiano zaidi hususani Katika ulinzi wa hifadhi na uhifadhi.

Jumatatu, 8 Juni 2015



 UVCCM IRINGA KUSAIDIA JITIHADA ZA SERIKALI KUHAMASISHA VIJANA KUJIARI NA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.
katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi wa pili kulia akiwa na katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda.
Vijana nchini hususani mkoani Iringa wameshauriwa kujiandaa na kujiweka sawa katika kupambana na changamoto za ugumu wa maisha kwa kuchangamkia furusa mbalimbali zinazojitokeza na kujiajiri wenyewe.

Kauli hiyo imekuja baada ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na kuonesha kuwa vijana wengi wamekuwa na mitazamo ya kusubiri serikali iwaletee badala ya kufikiri zaidi namna ya kujitengenezea ajira zitakazo waletea kipato na kuboresha maisha yao hali ambayo imeendelea kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Akitoa tathimini ya kikao  cha Baraza la vijana mkoa wa Iringa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Bw Elisha Mwampashe amewataka vijana wafanye kazi ili wasiendelee kuilamu serikali.

“ninawaomba vijana ifike wakati tujitambue na tuone jukumu la kujiletea maendeleo katika familia zetu tusiwe watu wa kulaumu tu badala kuwa na mawazo chanya kujishughulisha na shughuli zitakazotuletea maendeleo ili hata kama kuna mkono wa serikali kusaidia jitihada zetu utukute tukiwa tayari tuna mambo tunafanya” alisema mwampashe

Aidha  alisema maadhimio ya vijana wa chama cha mapinduzi  katika kikao hicho ni kutoa elimu kwa vijana itakayowasaidia kutumia changamoto zilizopo kuwa fulsa zitakazo waingizia kipato pia ameeleza maadhimio mengine kuwa ni kuwatembelea vijana na kubaini changamoto zinazowakabili na kutafuta namna ya kuzimaliza mengine ni kusaidia katika shughuli za kijamii ambapo mapema mwezi huu wanatarajia kuweka kambi ya pamoja kwaajili ya kufyatua tofari na kuanza ujenzi wa Bweni la shule ya sekondari Idodi lililoteketea kwa moto hivi karibuni kama vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa iringa ili kupunguza nguvu ya wananchi katika kuchangia ujenzi huo.

“tumefanya kikao cha baraza la vijana wa Chama Cha Mapinduzi na tumejadili na kuadhimia mambo mengi ambayo tunaamini tutayasimamia na kuyatekereza kama vijana tumeadhimia kuwafikia vijana wengi ili kuangaliachangamoto zinazowakabili na tuone namna ya kuzitatua na vijana wenyewe kuhakikisha tunatengeneza vikundi vya kiujasiliamali vitakavyotuwezesha kupata wafadhiri”.alisema

Hivyo Mwampashe amesema wao kama vijana watahakikisha wanawafikia vijana wote wa mkoa wa iringa ili kukumbushana wajibu wao katika kujiletea maendeleo na kutambua kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa.

Mwampashe amesema sio jambo jema kwa vijana wenye nguvu kushinda vijiweni wakizungumza siasa na kucheza bao wakati wenzao wakiwa katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

“tumepita katika vikundi kadhaa hapa mkoani na tayari tumekutana na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na ujasiliamali tumezungumza nao tumewapa elimu na baadhi ya vitendea kazi kama mashine ya ufyatuaji tofari na kuwahamasisha umoja kwa mustakabari wa maisha yao kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya vijana wanaokaa vijiweni bila kazi yoyote na kuilamu serikali  jambo ambalo halina manufaa yoyote kwao”.alisema mwampashe katibu wa vijana

Alisema duniani kote hakuna serikali inayoweza kuajiri kila mtu mwenye uwezo na sifa za kufanya kazi na akazungumzia umuhimu wa sekta binafsi katika kushughulikia changamoto ya ajira kwa vijana.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka hu, Mwampashe amewataka wanawake kuondoa hofu na kujitokeza kwa wingi kushindana na wanaume katika nafasi mbalimbali za uongozi zinazogombewa.

Pamoja na wanawake, amewasishi vijana wenye sifa kutupa karata zao katika uchaguzi huo huku akiwataka wajiandikishe kwa wingi na kushiriki kikamilifu kuchagua viongozi bora wanaojali matatizo yao.

Alhamisi, 4 Juni 2015

WANANCHI WA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI WAMPOKEA EXAUD KIGAHE KUWA MGOMBEA UBUNGE ENDAPO ATAPITISHWA KUGOMBEA

EXAUD KIGAHE AGOMBEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI.
Exaud Kigahe Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini
Ikiwa mchakato wa kutangaza nia ya kugombea Ubunge na Urais hapa nchini unaendelea jamii imetakiwa kuwachagua watu wenye nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo chanya katika maeneo husika.

 Hayo yamesemwa na Mdau wa maendeleo wilayani Mufindi Bw Exaud Kigahe wakati akizungumza na wandishi wa habari Mjini mafinga wailayani Mufindi Mkoani Iringa wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mufindi kasikazini ambapo amesema ni vyema na wakati umefika kwa wananchi kuwachagua viongozi wenye uwezo na uzalendo wanaoweza kushirikiana nao katika kuleta maendelaeo.

“ni ukweli usiopingika kwamba wakati wa viongozi kuwarubuni wananchi umekwisha ninahakika kwamba Mufindi ninaijua vizuri sana yale maisha wanayaishi wananchi wale siyo ndiyo waliyotakiwa kuishi nimekuja kushirikiana nao tuondoe tatizo la umaskini kikubwa nikipewa ridhaa kwangu wajibu wangu ni kuwaletea maendeleo wananchi” alisema Kigahe

Bw Kigahe amesema mtazamo wa sasa katika kusimamia shughuli za maendeleo zinatazamwa zaidi kwa viongozi ambapo anapotokea kiongozi ambaye hana uwezo hakuna maendeleo yatakayopatikana kwa wakati hivyo amesema endapo atapata nafasi ya kuongoza jimbo hilo kuna mambo lukuki anayoyaona yakitumika kama furusa kwa wananchi wa Mufindi yatawapa maendeleo kwa kasi wananchi hao.

Amesema wilaya ya Mufindi ni miongoni mwa wilaya zenye raslimali za kutosha ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikituwa na wageni huku wazawa wakibaki kuwa walinzi jambo ambalo amesema kusingekuwa na maendeleo hata kwa miaka ijayo bali kwa kutumia rasilimali hizo atahakikisha anawaunganisha wananchi kwa ushirikishaji wa mambo yote ya maendeleo kwa faida ya wanamufindi wenyewe.

“rasirimali zilizopo ninaamini zinatosha sana kutuletea maendeleo wanamufindi ninachokifahamu kwa mufindi na kwamba tuna misitu lakini kutokana na uongozi kutotujali wamekuwa wakitumia watu wa maeneo mengine nadhani muda wa wananchi kutumia misitu yao umewadia nitafurahi nao na kulia nao” alisema

Pia Kigahe amesema inasikitisha kuona rasirimali kama misitu inavunwa na watu wa nje na wenyeji wakibaki maskini jambo ambalo haliwezi kuvumilika,amesema wilaya ya Mufindi ina ardhi ya kutosha ambayo kwa kiasi kikubwa haiwanufaishi wanamufindi.

Hivyo amewataka wananchi kwasasa wasidanganyika na watu wanakuja wakiwa hawana malengo mema na wananchi bali wanahitaji kujinufaisha wenyewe bali sasa amekuja kwaajili ya kushirikiana nao kuiondoa hali hiyo.

“kwa upande wangu ninaamini kwamba wanamufindi wanahitaji mambo makubwa machache tu ambayo nikipata ridhaa na wakati maalumu ukifika nitawaeleza na namna tutakavyo weka mikakati ya maendeleo mimi ninauchungu na maisha yale wanayoishi mama zetu,baba zetu hata wadogo zetu naomba wanipokee tuyamalize hayo” ni maneno ya Kigahe

Jimbo la Mufindi Kaskazini lenye kata 11 za Ikweha, Sadani, Igombavanu, Ifwagi, Mdabulo, Ihalimba, Kibengu, Mapanda, Mpanga Tazara, Ihanu na Ikongosi, Jimbo la Mufindi Kusini litakuwa na kata 14 za Kiyowela, Makungu, Mninga, Kasanga, Igowole, Mtambula, Itandula, Mbalamaziwa, Idunda, Mlangali, Nyololo, Ihowanza, Mtwango na Luhunga:

Jumatano, 3 Juni 2015

Itazame familia hii iliyotembelewa na Mbunge wa Vitimaalum Ritta Kabati wote wakiwa walemavu.



 WANANCHI NA VIONGOZI WAMPONGEZA MBUNGE WA VITIMAALUM KWA JUHUDI ZAKE KATIKA KUPIGANIA MAENDELEO IRINGA.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Ritta Kabati alipotembelea familia ya watu watano wote wakiwa walemavu na wanaishi mazingira magumu Wilayani kilolo ambapo aahidi kuwajengea Nyumba ya Kisasa.
 

Zikiwa zimebaki siku kadhaa kumalizika kwa kipindi cha Uongozi wa wabunge hapa nchini hususani wabunge wa Viti maalumu ambao wanatarajia kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo wananchi na viongozi mkoani Iringa wampongeza Mbunge wa Viti maalumu Ritta Kabati.

Wakizungumza na Morning star redio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamempongeza Mh.Kabati kwa mchango wake kwa jamii ya mkoa wa Iringa na kuonyesha moyo wa upendo na kuthamini ubora wa maisha ya wanairinga wote bila kujali itikadi ya dini,siasa wa rangi ambapo amekuwa akipigania maendeleo ya watu wa rika zote.

Wananchi hao wamemtaja Mbunge Kabati kuwa ndiye kiongozi wa kuigwa na viongozi wengine kwa kuwa amekuwa amefanikiwa kusemea vema mkoa wa Iringa na kutoa kero za wananchi bungeni bila woga na kuifanya serikali kutekeleza kwa kuzingatia mchango wake.

Wakizitaja baadhi ya kazi alizozifanya Mh.Kabati  kuwa na pamoja na kulipigania suala la haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume,suala la kuwapa elimu watoto wa kike ukizingatia katika ofisi ya mbunge huyo imekuwa ikisaidi watoto wasiojiweza waliohitimu kidato cha nne kwa kuwatafutia vyuo mbalimbali jambo ambalo limewafanya zaidi ya watoto elfu 15 kuendelea na masomo.

Aidha wamesema amekuwa akipigania suala la miundombinu pamoja na afya ambapo kupitia jitihada zake zimesaidia kuboresha wodi za wazazi katika Hospital ya wilaya ya Iringa sambamba na hilo amejenga kituo cha polisi kwa ghalama ya Sh mil 45 kilichopo Semtema manispaa ya Iringa.

Kwa upande wa viongozi akiwemo Meya wa Halmashauri ya Iringa Amani Mwamwindi,Katibu wa CCM mkoa Hasani mtenga na mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoani Iringa Wamempongeza kwa jitihada za kuwezesha eneo la kihesa kilolo kuwa eneo la uendelezaji kwa makazi badala ya kuwa eneo la hifadhi.