![]() |
| Nayman Chavala Katibu Mkuu Dayosisi ya Iringa KKKT |
Hatimaye sasa yamekuwa ambapo waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania kwa umoja wao wameanza maandalizi ya kumpokea askofu mpya wa kanisa hilo Dayosisi ya Iringa Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga ambao watapokea kijiti cha kuisimamia Dayosisi hiyo kutoka mikononi mwa askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella aliyehudumu kwa zaidi ya miaka 30.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Katibu mkuu wa Dayosisi hiyo Nayman Chavala alisema tayari maandalkizi ya ibada hiyo yameanza ambapo ibada hiyo rasmi itafanyika katika viwanja vya Gangilonga huku wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa tayari wameanza kuingia.
"jumapili hii tunatarajia kuwa na Ibada kubwa ya kumuingiza kazini rasmi Askofu mteule Mch Blaston Gavile na tayari maandalizi yanaendelea vizuri na kwa kasi kubwa ningependa niwaalike watu wote katika ibada ambayo itaongozwa na Mkuu wa Kanisa KKKT Askofu Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella ambapo napenda niwaarifu kuwa kabla ya ibada kutakuwa na maandamano ya wachungaji na waumini kuanzia kanisa kuu hadi Gangilonga hivyo niwakaribishe kuungana nasi"alima chavala
Katika hatua nyingine Chavala alisema Ibada hiyo itakuwa mahususi kwaajili ya kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwa tumikia watanzania bila kujali itikadi na kutetea maslahi ya jamii.
"Mh rais anafanya kazi nzuri na kasi aliyonayo inafaa ni vyema watanzania tuendelee kuumunga mkono kwa jitihada anazofanya kutetea masilahi ya Umma sisi kama kanisa tumekuwa tukimuombea mara kwa mara na hii inamaana zaidi kwasababu tumekuwa tukiona jitihada zake za kuleta maendeleo"alisema
Hivyo katika ibada hiyo alisema kutakuwa na wageni wa serikali na Dini kutoka maeneo ,mbalimbali ndani na nje ya Nchi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni