Jumanne, 23 Desemba 2014
Vocaroo Voice Message
Mwimbaji wa Nyimbo za Injiri Nyanda za juu kusini anayetarajia kuanza rasmi show mbalimbali na mona kati ya vibao alivyonavyo ni hiki kinasema ANAWEZA
Ijumaa, 5 Desemba 2014
Mwasabwite kukonga Tamasha la Krismasi
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini Edson Mwasabwite anayetamba
kwa sasa na kibao chake kijulikanacho kwa jina la ‘Ni kwa Neema na
Rehema’ amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la
Krismasi litakalofanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea Desemba
mwaka huu.
Mwasabwite alisema amejipanga kikamilifu kukonga nyoyo za
mashabiki wake katika tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 25,
26 na 28 hivyo mashabiki zake wajitokeze kwa wingi kupata burudani ya
nguvu kutoka kwake.
Mwasabwite alisema mwaka huu watanzania wakae mkao wa kula kwa
kusifu na kuabudu katika Tamasha la Krismasi kwani tayari amezindua
albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la ‘Asilimia mia Mungu
amenihurumia’ yenye nyimbo tisa.
“Nimejipanga vizuri kutoa burudani kwa mashabiki wangu katika
tamasha la mwaka huu la Krismasi kwani maandalizi ni mazuri, safari hii
itakuwa zaidi ya mwaka jana kwa sasa nina nyimbo nyingi zitakazowabariki
mashabiki zangu na tayari nimeshazindua albamu mpya,” alisema
Mwasabwite.
Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Msama Promotions kwa kuweza
kuandaa Tamasha kubwa la Kikristo lenye mafanikio makubwa kwa kuweza
kuwakutanisha waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa
lengo la kutangaza injili Tanzania.
“Makampuni ya Msama yanaaminika na kukubalika kwa watanzania na
nchi nyingine za jirani ndio maana hata tamasha linafanikiwa, tunaomba
wananchi waendelee kununua kazi zetu, tunaomba sapoti kutoka kwa waumini
na mashabiki wa muziki wa Injili,” alisema Mwasabwite.
MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA KUJITOLEA DUNIANI
Siku
ya Kimataifa ya Kujitolea Duniani huadhimishwa tarehe 5 Desemba kila mwaka kwa
lengo la kutambua mchango wa kujitolea unaotolewa kwa ajili ya maendeleo katika
jamii tunamoishi, kitaifa na kimataifa.
Kujitolea
hujumuisha hiari, umoja, utu na kuaminiana na kunatoa fursa muhimu katika
kupambana na maradhi, ujinga, umasikini, hifadhi ya mazingira na maeneo mengi
ya kimaendeleo ambayo yanahitaji msukumo.
Aidha,
kujitolea kunatoa mchango muhimu katika kushughulikia majanga pale yanapotokea,
kuimarisha umoja katika jamii na kuboresha maisha ya watu.
Tanzania
kama sehemu ya jamii ya Kimataifa itaadhimisha siku hiyo katika katika ukumbi
wa Chuo cha Utalii kilichopo karibu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),saa
mbili na nusu asubuhi.
Kaulimbiu
ya Maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Ushiriki na Ushirikishwaji katika kuleta
maendeleo katika ngazi zote za mitaa, taifa na kimataifa.’
Katika
maadhimisho hayo, wananchi hasa vijana watashiriki katika mdahalo kuhusu
umuhimu wa kujitolea kwa ajili ya kuleta maendeleo. Aidha, kutakuwa na shuhuda
na maonyesho ya taasisi zinazoshiriki katika shughuli za kujitolea ili
kuhamasisha na kufufua moyo wa kujitolea miongoni mwa jamii.
Watanzania
hususan Vijana wanahamasishwa kuibua shughuli za kujitolea na kushiriki katika
zile zilizokwisha anzishwa ikizingatiwa kuwa wao ndiyo nguvu kazi kubwa
ya jamii.
Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inawakaribisha wananchi wote kushiriki
katika maadhimisho hayo muhimu ili kushiriki katika mdahalo huo na kujionea
jinsi watu mbalimbali wanavyotoa mchango mkubwa katik jamii kupitia shughuli za
kujitolea.
Top of Form
Bottom of Form
Bottom of Form
Top of Form
Bottom of Form
Bottom of Form
Jumatano, 12 Novemba 2014
MUCOBA BENKI YAWA CHACHU YA MAENDELEO KWA WAKULIMA MKOANI
IRINGA
| Meneja wa Benki ya Wananchi MUCOBA Bw Beny Mahenge akielezea utendaji wa Benki hiyo |
| Wadau wa Benki ya wananchi MUCOBA |
Wakulima wa mkoa wa Iringa wameanza kunufaika na ruzuku za
pembejeo kupitia Benki ya wananchi Mufindi(MUCOBA) ambayo kwa sasa inajulikana
kwa jina la MUCOBA Bank PLC ikijumuisha wananchi wote wa mkoani wa Iringa imeanza
kutoa mikopo ya pembejeo kwa vikudi vya wakulima.
Akielezea juu ya namna mwananchi atakavyonufaika na ruzuku
hiyo Meneja wa Benki hiyo Bw Ben Mahenge amesema serikali imeamua kutoa ruzuku
kwa mkulima kupitia Benki ya wananchi kutokana na ukaribu wa Benki hiyo kwa
wananchi wa maeneo yote ya mkoa wa Iringa ili kulinda usalama wa chakula kwa
mkulima.
Amesema kuwa walengwa wakuu ni wananchi wa kipato cha chini
ili wawe na uhakika wa kupata chakula cha kutosha hususani kwa wale waliolima
ukubwa wa shamba la kuanzia ekali moja ambao watasaidiwa kupatiwa ruzuku ya
mifuko mitatu ya mbolea na mfuko mmoja wa mbegu kwa mazao ya Mpunga na Mahindi
ikiwa ndiyo mazao pekee yanayopendelewa na wananchi wa mkoa wa Iringa.
Bw Mahenge ameendelea kufafanua juu ya ruzuku hizo kuwa
itatolewa kwa wakulima watakaojiunga katika vikundi mbalimbali
vitakavyojumuisha wanakikundi wasiopungua 10 ambao kila mmoja atapatiwa mkopo
wa pembejeo zenye ruzuku ya serikali.
Ameelezea kuwa ruzuku hiyo itatokana na riba ya mkopo
atakaoupa kutoka benki ambayo ghalama yake ya ni 18% ambapo serikali inalipa
riba ya asilimia 14% ya riba ikiwa kwa upande wa mkulima atalipa riba ya
asilimia 4% kutoka kwenye riba ya asilimia 18% ya mkopo wote.
Aidha amesema kupitia benki hiyo ya MUCOBA wananchi
watajipatia pembejeo wanazozihitaji badala ya kupangiwa aina ya pembejeo za
kilimo ili kuboresha zaidi kipato na mazao ya mkulima ambapo amesema mkopo huo
utalipwa baada ya mavuno pamoja na kwa kabla ya mkulima kupewa mkopo huo
atatakiwa kulipa asilimia 20 ya kianzio kuonesha nia ya kuhitaji ruzuku.
Hivyo amewataka wananchi kushiriki katika vikundi mbalimbali
ili wawe sehemu rahisi ya kupata pembejeo zenye ruzuku ya serikali kwa urahisi
zaidi pia amewataka wakulima kumchangua wakala wa pembejeo atakayeshirikiana
katika kuzipata zenye viwango vya hali ya juu.
Jumanne, 11 Novemba 2014
HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss.
“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!
MADIWANI MANISPAA YA IRINGA WAANZA KUTAKELEZA KAULI YA
KATIBU MKUU WA CCM KWA VITENDO.
Baraza la Madiwani manispaa ya Iringa lakumbushwa umuhim wao
katika kusimamia miradi ya Maendeleo ikiwa ni nguzo ya muhim katika kuendeleza
uchumi wa familia,jamii na Taifa.
Hayo yamejili mwisho wa wiki katika kikao charobo ya mwaka
wa fedha 2014/2015 cha Baraza la
Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa mjini ambapo Meya ambaye pia
ndiye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo Aman Mwamwindi aliwambia madiwani kuwa
nisehemu ya serikali hivyo wanaowajibu wa kusimamia miradi inayoanzishwa na
serikali ikiwemo miradi ya Afya,elimu,miundombinu na shughuli za uchumi ili
kuongeza upatikanaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Alisema pamoja na kwamba madiwani hao wanashiriki kwa kiasi
kikubwa katika usimamizi wa miradi hiyo lakini pia alipata fulsa ya
kuwakumbusha kuwa usimamizi wa miradi hiyo unashirikisha viongozi wa ngazi ya
kijiji hadi Taifa,wananchi wa maeneo husika pamoja na asasi za kiraia na
kashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa na lengo la kuboresha maisha ya watanzani.
“Waheshimiwa madiwani
tumekuwa mstari wa mbele kusimamia miradi inayoanzishwa katika kata zetu japo
wapo wachache ambao kazi yao ni kuturudisha nyuma kwa makusudi maana tumekuwa
na miradi mingi na inafanya vizuri kwaajili yetu sote na jamii zinazotuzunguka
sasa unapoona mtu anaingiza kitu ambacho kinarudisha nyuma juhudi za serikali
ukanyamaza manaake unashiriki mojakwamoja kuangamiza maisha ya
watanzani”alisema meya
Hivyo amesema usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo mara
nyingi inasababisha baadhi ya miradi kufanyika chini ya kiwango.
Baraza hilo pia lilipata nafasi ya kupata semina juu ya
ushiriki wao katika mapambano dhidi ya rushwa ambalo limekuwa janga la dunia
ambalo limekuwa likiwahusisha zaidi watendaji wa serikali.
Akitoa semina hiyo Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa(TAKUKURU)Bw Ismail Bukuku aliwambia madiwani kuwa lengo la semina
hiyo ni kuwakumbusha uwajibikaji kwa kufuatamisingi ya sheria huku wakitambua
usimamizi mzuri wa raslimali za umma kutasaidia kuziba mianya ya
Rushwa,itasaidia fedha za miradi kutumika kwa malengo yaliyo kusudiwa.
Huku akiwataka madiwani hao kuwaelimisha wananchi kutambua
haki zao katika kupata huduma za msingi ikiwa nipamoja na matibabu,ajira,elimu
bila kutoa wala kupokea rushwa vilevile
kuzijua sheria.
Jumatano, 24 Septemba 2014
MH.MGIMWA AWAHAMASISHA VIJANA KUUNDA VIKUNDI ILI WAWEZESHWE.
Vijana nchini wametakiwa kujiunga katika vikundi vya
ujasiliamali vitakavyo warahisishia kupewa dhamana ya mitaji kutoka katika
mifuko ya vijana ya serikali.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kalenga
mkoani hapa Mh.Godfrey Mgimwa wakati wa mahojiano maalumu na Overcomers redio
katika kipindi cha tujadili asubuhi kuhusu namna viongozi wanakusudia kuwapa
fulsa vijana wote pasipo kuangalia mjini wala vijijini.
Mh.Mgimwa amesema imefika wakati wao kama viongozi
vijana kupigania maslahi ya vijana na haki zao za kuwezeshwa kimaisha ili
waweze kujikwamua kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo fedha za mifuko ya vijana
zitawafikia katika vikundi.
Hivyo amewataka vijana kushirikiana kwa pamoja
katika kujiletea maendeleo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





