Jumatano, 12 Novemba 2014



MUCOBA BENKI YAWA CHACHU YA MAENDELEO KWA WAKULIMA MKOANI IRINGA

Meneja wa Benki ya Wananchi MUCOBA Bw Beny Mahenge akielezea utendaji wa Benki hiyo
Wadau wa Benki ya wananchi MUCOBA
Wakulima wa mkoa wa Iringa wameanza kunufaika na ruzuku za pembejeo kupitia Benki ya wananchi Mufindi(MUCOBA) ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la MUCOBA Bank PLC ikijumuisha wananchi wote wa mkoani wa Iringa imeanza kutoa mikopo ya pembejeo kwa vikudi vya wakulima.

Akielezea juu ya namna mwananchi atakavyonufaika na ruzuku hiyo Meneja wa Benki hiyo Bw Ben Mahenge amesema serikali imeamua kutoa ruzuku kwa mkulima kupitia Benki ya wananchi kutokana na ukaribu wa Benki hiyo kwa wananchi wa maeneo yote ya mkoa wa Iringa ili kulinda usalama wa chakula kwa mkulima.

Amesema kuwa walengwa wakuu ni wananchi wa kipato cha chini ili wawe na uhakika wa kupata chakula cha kutosha hususani kwa wale waliolima ukubwa wa shamba la kuanzia ekali moja ambao watasaidiwa kupatiwa ruzuku ya mifuko mitatu ya mbolea na mfuko mmoja wa mbegu kwa mazao ya Mpunga na Mahindi ikiwa ndiyo mazao pekee yanayopendelewa na wananchi wa mkoa wa Iringa.

Bw Mahenge ameendelea kufafanua juu ya ruzuku hizo kuwa itatolewa kwa wakulima watakaojiunga katika vikundi mbalimbali vitakavyojumuisha wanakikundi wasiopungua 10 ambao kila mmoja atapatiwa mkopo wa pembejeo zenye ruzuku ya serikali.

Ameelezea kuwa ruzuku hiyo itatokana na riba ya mkopo atakaoupa kutoka benki ambayo ghalama yake ya ni 18% ambapo serikali inalipa riba ya asilimia 14% ya riba ikiwa kwa upande wa mkulima atalipa riba ya asilimia 4% kutoka kwenye riba ya asilimia 18% ya mkopo wote.

Aidha amesema kupitia benki hiyo ya MUCOBA wananchi watajipatia pembejeo wanazozihitaji badala ya kupangiwa aina ya pembejeo za kilimo ili kuboresha zaidi kipato na mazao ya mkulima ambapo amesema mkopo huo utalipwa baada ya mavuno pamoja na kwa kabla ya mkulima kupewa mkopo huo atatakiwa kulipa asilimia 20 ya kianzio kuonesha nia ya kuhitaji ruzuku.

Hivyo amewataka wananchi kushiriki katika vikundi mbalimbali ili wawe sehemu rahisi ya kupata pembejeo zenye ruzuku ya serikali kwa urahisi zaidi pia amewataka wakulima kumchangua wakala wa pembejeo atakayeshirikiana katika kuzipata zenye viwango vya hali ya juu.

Jumanne, 11 Novemba 2014


HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss.

HATARI!! Diamond aamua kuwapa ''makavu live'' team Wema baada ya wao kumdiss.

Baada ya mashabiki wa mwanadada Wema "kumjia juu mwanamuziki Diamond Platnumz" kuhusu tuhuma za yeye kumtumia mwanadada huyu kimwili zaidi bila kumuendeleza, hatimaye raisi huyu wa kundi la WCB ameamua nay eye kufunguka haya mazito juu ya kauli hizo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao ule maarufu wa kijamii Diamond ameandika haya..

“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!


MADIWANI MANISPAA YA IRINGA WAANZA KUTAKELEZA KAULI YA KATIBU MKUU WA CCM KWA VITENDO.

Baraza la Madiwani manispaa ya Iringa lakumbushwa umuhim wao katika kusimamia miradi ya Maendeleo ikiwa ni nguzo ya muhim katika kuendeleza uchumi wa familia,jamii na Taifa.

Hayo yamejili mwisho wa wiki katika kikao charobo ya mwaka wa fedha 2014/2015 cha  Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa mjini ambapo Meya ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo Aman Mwamwindi aliwambia madiwani kuwa nisehemu ya serikali hivyo wanaowajibu wa kusimamia miradi inayoanzishwa na serikali ikiwemo miradi ya Afya,elimu,miundombinu na shughuli za uchumi ili kuongeza upatikanaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
Alisema pamoja na kwamba madiwani hao wanashiriki kwa kiasi kikubwa katika usimamizi wa miradi hiyo lakini pia alipata fulsa ya kuwakumbusha kuwa usimamizi wa miradi hiyo unashirikisha viongozi wa ngazi ya kijiji hadi Taifa,wananchi wa maeneo husika pamoja na asasi za kiraia na kashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa na lengo la kuboresha maisha ya watanzani.

“Waheshimiwa madiwani tumekuwa mstari wa mbele kusimamia miradi inayoanzishwa katika kata zetu japo wapo wachache ambao kazi yao ni kuturudisha nyuma kwa makusudi maana tumekuwa na miradi mingi na inafanya vizuri kwaajili yetu sote na jamii zinazotuzunguka sasa unapoona mtu anaingiza kitu ambacho kinarudisha nyuma juhudi za serikali ukanyamaza manaake unashiriki mojakwamoja kuangamiza maisha ya watanzani”alisema meya

Hivyo amesema usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo mara nyingi inasababisha baadhi ya miradi kufanyika chini ya kiwango.
Baraza hilo pia lilipata nafasi ya kupata semina juu ya ushiriki wao katika mapambano dhidi ya rushwa ambalo limekuwa janga la dunia ambalo limekuwa likiwahusisha zaidi watendaji wa serikali.

Akitoa semina hiyo Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Bw Ismail Bukuku aliwambia madiwani kuwa lengo la semina hiyo ni kuwakumbusha uwajibikaji kwa kufuatamisingi ya sheria huku wakitambua usimamizi mzuri wa raslimali za umma kutasaidia kuziba mianya ya Rushwa,itasaidia fedha za miradi kutumika kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Huku akiwataka madiwani hao kuwaelimisha wananchi kutambua haki zao katika kupata huduma za msingi ikiwa nipamoja na matibabu,ajira,elimu bila kutoa wala kupokea rushwa vilevile  kuzijua sheria.