Jumanne, 23 Desemba 2014
Vocaroo Voice Message
Mwimbaji wa Nyimbo za Injiri Nyanda za juu kusini anayetarajia kuanza rasmi show mbalimbali na mona kati ya vibao alivyonavyo ni hiki kinasema ANAWEZA
Ijumaa, 5 Desemba 2014
Mwasabwite kukonga Tamasha la Krismasi
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini Edson Mwasabwite anayetamba
kwa sasa na kibao chake kijulikanacho kwa jina la ‘Ni kwa Neema na
Rehema’ amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la
Krismasi litakalofanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea Desemba
mwaka huu.
Mwasabwite alisema amejipanga kikamilifu kukonga nyoyo za
mashabiki wake katika tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 25,
26 na 28 hivyo mashabiki zake wajitokeze kwa wingi kupata burudani ya
nguvu kutoka kwake.
Mwasabwite alisema mwaka huu watanzania wakae mkao wa kula kwa
kusifu na kuabudu katika Tamasha la Krismasi kwani tayari amezindua
albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la ‘Asilimia mia Mungu
amenihurumia’ yenye nyimbo tisa.
“Nimejipanga vizuri kutoa burudani kwa mashabiki wangu katika
tamasha la mwaka huu la Krismasi kwani maandalizi ni mazuri, safari hii
itakuwa zaidi ya mwaka jana kwa sasa nina nyimbo nyingi zitakazowabariki
mashabiki zangu na tayari nimeshazindua albamu mpya,” alisema
Mwasabwite.
Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Msama Promotions kwa kuweza
kuandaa Tamasha kubwa la Kikristo lenye mafanikio makubwa kwa kuweza
kuwakutanisha waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa
lengo la kutangaza injili Tanzania.
“Makampuni ya Msama yanaaminika na kukubalika kwa watanzania na
nchi nyingine za jirani ndio maana hata tamasha linafanikiwa, tunaomba
wananchi waendelee kununua kazi zetu, tunaomba sapoti kutoka kwa waumini
na mashabiki wa muziki wa Injili,” alisema Mwasabwite.
MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA KUJITOLEA DUNIANI
Siku
ya Kimataifa ya Kujitolea Duniani huadhimishwa tarehe 5 Desemba kila mwaka kwa
lengo la kutambua mchango wa kujitolea unaotolewa kwa ajili ya maendeleo katika
jamii tunamoishi, kitaifa na kimataifa.
Kujitolea
hujumuisha hiari, umoja, utu na kuaminiana na kunatoa fursa muhimu katika
kupambana na maradhi, ujinga, umasikini, hifadhi ya mazingira na maeneo mengi
ya kimaendeleo ambayo yanahitaji msukumo.
Aidha,
kujitolea kunatoa mchango muhimu katika kushughulikia majanga pale yanapotokea,
kuimarisha umoja katika jamii na kuboresha maisha ya watu.
Tanzania
kama sehemu ya jamii ya Kimataifa itaadhimisha siku hiyo katika katika ukumbi
wa Chuo cha Utalii kilichopo karibu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),saa
mbili na nusu asubuhi.
Kaulimbiu
ya Maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Ushiriki na Ushirikishwaji katika kuleta
maendeleo katika ngazi zote za mitaa, taifa na kimataifa.’
Katika
maadhimisho hayo, wananchi hasa vijana watashiriki katika mdahalo kuhusu
umuhimu wa kujitolea kwa ajili ya kuleta maendeleo. Aidha, kutakuwa na shuhuda
na maonyesho ya taasisi zinazoshiriki katika shughuli za kujitolea ili
kuhamasisha na kufufua moyo wa kujitolea miongoni mwa jamii.
Watanzania
hususan Vijana wanahamasishwa kuibua shughuli za kujitolea na kushiriki katika
zile zilizokwisha anzishwa ikizingatiwa kuwa wao ndiyo nguvu kazi kubwa
ya jamii.
Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inawakaribisha wananchi wote kushiriki
katika maadhimisho hayo muhimu ili kushiriki katika mdahalo huo na kujionea
jinsi watu mbalimbali wanavyotoa mchango mkubwa katik jamii kupitia shughuli za
kujitolea.
Top of Form
Bottom of Form
Bottom of Form
Top of Form
Bottom of Form
Bottom of Form
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)