Jumatatu, 30 Machi 2015

WAFANYABIASHARA IRINGA WATAKIWA KUJIUNGA TANZANIA CHEMBER OF COMMERCE



Wafanyabiashara Mkoa Iringa wametakiwa kujiunga na Chama cha wafanyabiashara Tanzania Chember Of Commers ili kiwasaidie kutatua baadhi changamoto zinazowakabili.

Akizungumza na wandishi wa habari Ofisini kwake Katibu wa chama hicho Bw James Siziya alisema kumekuwa na matatizo mbalimbali yanayowakabili wafanyabiashara yanayosababisha kusimama kwa shughuli zao jambo ambalo amesema linaweza kushughulikiwa na na chama hicho.

"nimeona niwakumbushe wafanyabiashara wajiunge na Chember hii hapa ndipo wataleta malalamiko yao na hapa ndipo watapata majibu ya maswali yao wanayojiuliza juu ya mambo yanayowatatiza" alisema Siziya
 
Bwana Siziya Alisema ni vyema wafanyabiashara wakajiunga katika chama hicho ni maalum kwaajili ya kutetea masilahi ya wafanyabiashara hususani wale waliojiunga nacho ambapo chama hicho ndicho chenye dhamana ya kushughulikia migogolo na malalamiko yao kwa kufikisha mahali panapo husika na kuhakikisha yanashughulikiwa.

Alisema miongoni mwa changamoto zinazo wakabili wafanyabiashara ni pamoja na uelewa mdogo juu ya mambo ya kisheria,Kodi na matumizi ya mashine za kielectronic pamoja na kutojua sheria ya vipimo na mizani jambo ambalo amelitaja kuchangia ongezeko la kodiya usafirishaji bidhaa.

Aidha aliwataka wafanyabiashara kujisajili  na Tanzania Chember Of Commers kwa kuwa kitawasaidia kutambua sheria mbalimbali na kuepukana na usumbufu utakao wacheleweshea utendaji wao wa kazi.