Jumatatu, 26 Januari 2015

WANANCHI  MUFINDI WALALAMIKIA UGUMU WA MAISHA LICHA YA KUWA NA RASILIMALI ZA KUTOSHA

 

WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa ali
yekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
 Makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kasikazini
WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwahutubia wananchi wa jimbo la mufindi kusini ambako anatarajia kugombea ubunge kupitia Chadema.
  ……………………………………………………………………………………………
Wananchi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamelalamikia ugumu wa maisha
wanaokumbana nao kila kukicha licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa
rasilimali ya misitu pamoja na mazao ya biashara Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wilayani mufind Williamu Mungai mmoja wa wananchi hao Clement Mwachanga alisema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya inayofanya vema kwa kuingiza
pato kubwa la taifa lakini wananchi wake wako katika wimbi kubwa la umaskini
Mwachanga amesema anashangaa wilaya kama ya mufindi inayoongoza kwa utoaji wa mbao nyingi lakini cha kushangaza shule nyingi za msingi hazina madawati jambo linalopelekea wanafunzi wengi kukaa chini.
‘’Hii ni aibu kubwa sana kwa wilaya yetu haiwezekani wilaya inarasilimali za kutosha
lakini wananchi wake wengine wanashidwa hata kupata mlo mmoja kwa siku huku
watoto wao wakishidwa kupelekwa shule kutokana na kushidwa kulipa ada ya kumuandikishia mtoto ”
Kwa upande wake Williamu Mungai ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kulichukua
jimbo hilo la mufindi kaskazi ambalo kwa sasa linaongozwa na naibu waziri wa
maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa amewataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha
watoto wote wanaandikishwa shule za msinga hata kama hawana ada ya
kuandikishiwa kwa kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania
Mungai alisema ni kila mtoto ana haki ya kupata elimu ya msingi kwa kuwa ndivyo katiba
inavyosema na kuwataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarudisha
majumba watoto kwa kisingizio cha kukosa hela ya kuwaandikishia
“Niwatake wenyeviti wangu wa mitaa muhakikishe watoto wote wanaandikiswa na kama
kuna mwalimu atagona kumuandikisha kwa kisingizio eti hana shilingi eflu
hamsini jikusanyeni pamoja niiteni na mimi twende wote tuone kama hata
muandikisha kwa maana walishasema elimu bure sasa bure waliyosema ikuwapi”
alisema Mungai
Hata hivyo mungai alisema imefika wakati wakuikomboa mufindi iliyoko katika wimbi la
umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuataka wanamufindi
kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maono ya mbali katika kuwalete
maendeleo na sio porojo za kila siku.
Mungai alisema kuwa atahakikisha anazunguka vijiji vyote 72 vya wilaya ya
mufindi katika harakati zake za kujenga chama na kuweza kutambua kero za
wananchi na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua .

WASANII MKOANI IRINGA WAMEMTUNGIA WIMBO MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI FRANK KIBIKI

20150123_123538MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi kwa mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake.

………………………………………………………

MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi  kwa mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake, ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea  ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa,  wasanii hao walisema wameamua kutengeneza wimbo huo kutokana na mchango mkubwa wa mwanahabari huyo, katika fani yao.
Msanii huyo Richard Kayombo  ‘One Lee’ ambaye alikabidhi wimbo kwa niaba ya wasanii wenzake alisema wimbo huo, unamtambulisha Kibiki, kama kiongozi wa kuigwa kutokana na tabia yake ya ucheshi na kujichanganya na watu.akizungumza wakati wa kukabidhi WIMBO huo msanii  ‘One Lee’ alisema kuwa FRANK KIBIKI amekuwa akiwapa elimu vijana juu ya kujitambua na kuwasaidia jinsi gani ya kujiajili wao wenyewe na kuonyesha njia ya kutokea kimaisha na dio imekuwa sababu ya wasanii wa mkoani hapa kutunga wimbo huo. 
“Wimbo unaitwa ‘Kuwa mfano wa kuigwa’, tumempa kaka yetu kama zawadi, ili wengine waige mfano wake. 
Awali tulitamani uitwe Kibiki, lakini kwa sababu tunataka kuuza tumeamua kuuita jina hilo,”alisema One lee.
Alisema miaka miwili iliyopita, aliwahi kukutwa na jambo ambalo alihitaji msaada wa haraka, alihangaika lakini alipokutana na Kibiki ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, alisaidiwa jambo ambalo lilimfanya aanze kumuheshimu.
Alisema aliposikia kuwa Kibiki ametangaza nia, aliamua kushirikiana na wenzake ili watengeneze wimbo ambao hivi karibuni utaachiwa hewani.
‘One lee’alisena ngoma yake itamtambulisha Kibiki kama alivyo, na kwamba wameamua kumsaidia bila gharama yoyote kama sehemu ya mchango wao wakiamini ikiwa atafanikiwa kupenya na kupata nafasi hiyo, ataweza kuwaunganisha na kuwainua wasanii.
kwa upande wao wasanii wengine wa mkoani irnga walisema kuwa imefika wakati sasa iringa mjini itawaliwe na kiongozi mwenye uelewa juu ya kukuza uchumi wa mkoani na kuzingatia vipaji vya vijana kwa kuwa vijana ndio taifa la leo.

 

Jumamosi, 24 Januari 2015

BREAKING NEWS..!! WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROFESA SOSPITER MUHONGO AJIUZULU.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wanahabari ofisini kwake leo.

Hatimaye Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo amejiuzulu leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Muhongo amechukua uamuzi huo leo ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari.
Kujiuzulu kwa Muhongo kumetokana na maazimio ya Kamati ya Bunge  ya Hesabu za Serikali chini ya Mhe. Zitto Kabwe ilitokana na sakata la ufisadi wa Akaunti ya Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 306 zilichukuliwa kiholea Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha mjadala mzito ndani na nje ya Bunge.

Ukaguzi maalum uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  na uchuguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwenye akaunti hiyo, ulifanywa na ripoti zikatolewa na bunge, likajadili na kufikia tamati kwamba kuna kodi ya umma iliibwa.

Kwa vile suala hili liligusa utendaji wa viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na wanasiasa wengine,  bunge lilitaka kuyumba kutokana na kupendeleana licha ya ukweli kwamba fedha zilizochukuliwa ni nyingi sana .

Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya Uenyekiti wa Zitto Kabwe ilipitia kwa ufasaha ukaguzi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,(CAG)  na uchunguzi wa Takukuru wakatoa ripoti yao na uthibitisho wa kutosha kuwa kuna (aliyekuwa) Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, Waziri wa Madini na Nishati, Profesa Sospiter Muhongo pamoja na watendaji wengine serikalini wamehusika kwa njia moja au nyingine na upotevu wa fedha hizo za Escrow ama kwa kukusudia ama kwa kutojua, kitu ambacho kilielezwa kuwa ni uzembe.
Rais Jakaya Kikwete alichukua uamuzi wa kumfuta kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka  kutokana na madai kuwa alichotewa shilingi Bilioni 1.6  zilizotoka katika akaunti hiyo ya Escrow.

Rais Kikwete alisema Profesa Muhongo alikuwa amemuweka kiporo. Hata hivyo, Watanzania wengi wakati wa kikao cha bunge liliopita walishangazwa kuona baadhi ya wabunge kukaza misuli ya shingo zao na kutetea wizi ili wahusika wasiwajibishwe. Wengine walipingana na ripoti ya CAG.

Wakati wa kikao hicho cha Bunge aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alidaiwa kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye ndiye aliyeanzisha mjadala wa sakata hilo bungeni.

Vyombo vya habari vikatangaza kuwa kama siyo kuzuiwa na mawaziri, Jaji Werema angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga mbunge huyo  kutoka NCCR-Mageuzi, David Kafulila.

Ilidaiwa kuwa tafrani hiyo ilitokea baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni ya siku hiyo, ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni baada ya jaji kuchukizwa na kitendo cha mbunge huyo kijana kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili (na mwanasheria mkuu huyo wa nchi).

Waliomzuia Jaji Werema asizipike baada ya kumzunguka inadaiwa ni baadhi ya mawaziri ambao walimsindikiza hadi nje ya Ukumbi wa Bunge.


Jaji Werema pia alituhumiwa kumtishia kifo Kafulila ambaye alilalamika bungeni. Ikadaiwa kuwa jaji huyo alimtolea maneno hayo ya vitisho mbunge huyo kwenye viunga vya bungeni mjini Dodoma baada ya bunge kuahirishwa.
Jaji Werema alinukuliwa na vyombo vya habari akidaiwa kumwambia Kafulila: "I will take your head, unless you apologize," ikimaanisha atamkata kichwa iwapo hatamwomba msamaha!
Kufuatia tishio hilo Kafulila akajihami kwa kuiandikia barua ya madai ya kutishiwa maisha ofisi ya spika wa bunge, huku nakala ya barua hiyo akiipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu na nakala nyingine ameipeleka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma.


Hili ni tukio baya sana ambalo limeingia katika rekodi. Werema pia alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo.