Jumapili, 22 Februari 2015

WAZIRI MKUU AWATAKA WATENDAJI KUFANYAKAZI KWA WELEDI ILI KULILETEA TAIFA MAENDELEO.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akisalimiana na Watumishi wa Hospitali ya Wilaya Iringa Mijini.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watendaji wa Halmashari za mkoa wa Iringa kufanya kazi kwa Weledi ili kuongeza ufanisi katika kuleta maendeleo.
Agizo hilo lilitowa na Waziri Mkuu  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ipogolo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano ya kiserikali katika mkoa wa Iringa.
Waziri mkuu Pinda alifanya ziara katika halmashauri zote za mkoa wa Iringa na kukagua miladi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Umwagiliaji na katika halmashauri ya Manispaa ya iringa  amekagua ujenzi wa Maabara katika shule ya sekondari kihesa na kuupongeza ungozi wa kata hiyo kwa kuwa shule ya mfano kwa ufanisi.
“katika shule shule zote nilizopita kukagua ujenzi wa maabara shule yenu ya sekondari Kihesa nimerishwa na ni shule ya kuigwa kwa kazi nzuri inayoendana na matakwa ya serikali imejengwa kwa ufanisi mkubwa”alisema Pinda
Akizungumzia ujenzi wa maabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Waziri mkuu alisema hakfurahishwa na miundombinu iliyotumika katika ujenzi huo kutokana na kutumiwa kwa majengo ya zamani na ambayo hayana Ubora na kwakiwango cha Chini bali alisema amewaagiza viongozi wa halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuyaweka katika hali nzuri.
“Nimetembelea shule ya sekondari pale Ilula ili kukagua agizo la Rais la ujenzi wa maabara linavyoenda siku ridhishwa sana kwani wamechukua maabara za miaka 20 iliyopita na kuzifanya zitumike sasahivi kitu ambacho hakiwezi kufanya vizuri kama ilivyokusudiwa”alieleza
Pia amefungua kituo cha polisi Kiheza kilichojengwa kwa ufadhiri wa Mbunge wa viti maalum mkoani hapa Ritta Kabati ambapo kimetumia zaidi ya Milion 40.
Katika sekta ya Afya Waziri Pinda baada ya kukagua na kuzindua kituo cha Afya Mlowa kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Hospitali ya Wilaya iringa Mjini alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Jumatano, 18 Februari 2015



TASAF KUWANUFAISHA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU
 
NA AGUSTINO KIHOMBO IRINGA

Zaidi ya kaya elfu sita zinazoishi katika mazingira magumu za manispaa ya Iringa zinatarajia kunufaika na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika awamu ya tatu ya mpango wa kupunguza umasikini kwa jamii.

Akizungumza na mtanandao huu Mratibu wa Mfuko huo Manispaa ya Iringa Bi Lucy Mtafya alisema kuwa mpango wa matumizi ya mufuko huo umegawanyika katika awamu tatu ambapo katika awmu ya Kwanza mfiko huo wa maendeleo ulijikita zaidi katika kusaidi katika uboreshaji wa huduma za Elimu na Afya hususani ujenzi wa shule na Zahanati.

Akielezea juu ya Awamu ya kwanza ya TASAF alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kusaidia shughuli za maendeleo ambapo mfuko huo ulikuwa ukichangia kwa asilimia 80% ya ujenzi na wananchi 20% hivyo hadi awamu hizo mbili zimesaidi kujenga zaidi ya Shule tano na zahanati Tatu katika manisipaa ya Iringa.
“Kwa ujumla Mfuko huu wa Maendeleo ya jamii TASAF tumefanikiwa vizuri sana kuwasaidia wananchi katika shughuli zao za maendeleo mfuko huu kila mahali ulipofanya kazi ulichangia aslimia 80% na wananchi walichangia asilimia zinazo baki hiyo katika awamu hizo mbili” alisema

Akizungumzia kuhusiana na awamu hii ya Tatu ambayo imezinduliwa rasmi  Jan 6 2015 Bi Mtafya alisema tayari wamekwisha anza kushughulikia masuala ya kuzitambua kaya za watu wasio jiweza ambao ndiyo wanaolengwa na awamu hii ambapo wanalenga kuzifikia kaya zaidi ya 6000 ili kuwawezesha kiuchumi.

Mratibu huyo alisema wamejipanga kuhakikisha wanaolengwa na Mfuko huo kwa awamu hii ya tatu wananufaika na fedha zitakazotolewa na mfuko huo alisema katika manispaa wanafanya kazi na kata zote za manispaa ya iringa.
“katika awamu hii ya tatu ya Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF imelenga kuwafikia wote wanaohusika hasa wale ambao mitaa yao itakubaliana kuwa ndiyo watakao nufaika zaidi kwani katika siku za nyuma baadhi ya watu walikuwa wanajaribu kutumia ujanja kuwandika watoto wao wasaidiwe na kuwfanya walengwa wakose” alisema

Hivyo amewataka wananchi kusaidiana na serikali katika kuwasaidia waishio katika mazingira magumu ili kuwawezesha kumudu maisha pindi awamu hiyo itakapopita.