Jumatano, 14 Juni 2017

Watu kadha wafariki baada ya moto kuteketeza jengo refu London

 Moshi unaweza kuonekana kutoka mbali
Watu kadha wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London.

Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.
Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini.

Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limesema kuwa kulikuwa na hofu kuwa jengo hilo lingeporomoka.


Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza.

Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni