Jumamosi, 10 Juni 2017

WACHIMBAJI 9 WA MADINI WAJERUHIWA NA MAJAMBAZI NYAKAVANGALA IRINGA.


DC Richard Kasesela Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya Ya Iringa

Gloria Mnyonge Muuguzi wa zamu Hospitali ya Rufaa Iringa.
Msungu Shija Mchimbaji wa madini Nyakavangala
Wachimbaji wa madini wakiwa kazini Eneo la Nyakabangala Wilaya ya Iringa
Watu 9 ambao niwajimbaji wa madini katika mgodi wa nyakavangala uliopo katika tarafa ya ismani mkoani iringa wamenusurika kufa kwa kuvamiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi huku watu wawili wakiwa katika uangalizi wa madaktari ambapo majambazi hayo yakifanikiwa kupora pesa zaidi ya shilingi milioni 81 pamoja na gram 400 za dhahabu.
Sayari ya Habari ilifanikiwa kuzungumza na baadhi ya Majeruhi Msungu Shija mkazi wa Geita,Eliasi Mushi mkazi wa Arusha ambao wanasema baadaya kuteswa kwa muda mrefu ndipo bosi wao akajitokeza na kupigwa nyundo za miguu huku wakidai kuwa walikuwa wakimtafuta kwa zaidi ya wiki mbili bila mafanikio na wakihitaji madini pamoja na fedha.
“Ilikuwa majira ya saa moja jioni wakaja watu 8 wakatuambia tupo chini ya ulinzi tukalala chini wakaanza kupiga na nyundo wakasema wanamtaka bosi tukauliza shida nini hawakusema wakamfuata ndani walipomkuta wakamtoa nje huku wakimpiga wakitaka atoe hela za madini yaliyopatikana juzi ikabidi atoe wakaondoka lakini kwasababu pale hakuna kituo cha polisi ilikuwa shida kupata msaada walitusurubisha kwa muda kama wa saa moja ”.
Gaspa mbanda nimiongoni mwa wachimbaji wadogo ambaye aliyenusurika anasema baada ya kusikia milio ya risasi alijificha alisema wakati majambazi hao wanavamia baadhi ya wachimbaji walikuwa bado wapo mgodini akiwa katika harakati za kutoka mgodini ndipo aliposikia milio ya risasi akamrazimu ajifiche ili kunusuru maisha yake jambo lililomfanya kuiomba serikali kujenga kituo cha polisi ili kimarisha hali ya ulinzi nausalama kwa wachimbaji hao kwani katika eneo hilo hakuna kituo cha polisi.
“nilikuta watu wakipiga kelele kudai kuwa wamevamiwa tena alikuwa ndugu yangu ambaye alikuwa ameuza mzigo kutazama nikakuta amekamatwa na anapigwa walipoondoka majambazi hao ilibidi tuwachukue kuwaleta hospitali kwa kweli hakuwa tukio zuri maana tupo zaidi ya watu 3000 katika hili eneo kama ingewezekana serikali itujengee kituo cha polisi pale tunaomba ili usalama uwepo”.
Kwaupande wake muuguzi wazamu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Grolia Mnyonge alikiri kupokea baadhi ya majeruhi ambao kwasasa wanaendelea kupatiwa matibabu na wanne wanendelea vizuri na huku wawili wakiwa katika hali mbaya.
“Hapa tumepata majeruhi wanne mmoja ameruhusiwa wamebaki watatu mmoja yupo chumba cha Upasuaji ambaye hali yake bado si nzuri baadhi yao wana michubuko midogomidogo miguuni na mikononi hali zao zikiendelea kuwa hivi watakuwa vizuri pasipo shaka”.
Akizungumzia tukia hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Iringa ambaye ndiye mkuu wa wilaya ya iringa Richard kasesela amwaambia wandishi wa habari kuwa takribani wiki sita kumekuwa na ongezeko kubwala watu wanaokwenda kutafuta riziki kutokana na kupatikana dhahabu lakini jana kunatukio la uvamizi limetokea majambazi waliokuwa na silaha mbalimbali za jadi ambapo aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Mginya Dadae mkazi wa Morogoro (38),Bakari Beka,Sungali Shija mkazi wa Geita,Fadhiri Ramadhan,Nsulwa Msanda,Odrick Michael,Kitandu Mabura,Daniel Msonja,Elia Mushi,na aliwataka wachimbaji hao kuacha tabia kutembea na fedha nyingi hali itakayo saidia kupunguza matukio ya ujambazi .
“ni kweli tukio hilo limetokea katika wilaya yetu lakini Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kuwasaka wahusika wa kosa hilo lakini niwaombe wananchi na wachimbaji kutumia njia mbadala katika kulipana fadha badala ya kutembea na fedha mkononi”.
Tangu kugundulika uwepo wa madini katika kijiji cha nyakavangala tarafa ya isimani kumekuwanaongezeko la watu kila uchwao kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo mpaka hivi sasa eneo hilo linatajwa kuwa na zaidi ya watu 5000.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni