“kufuatia tukio lililotokea mnamo 09/06/2017 majira ya saa moja na nusu
usiku katika machimbo ya nyakavangala majambazi 9 yaliwavamia wachimbaji
wadogowadogo na kuwalazimisha walale chini na kuanza kuwashambulia kwa nyundo
na nondo ambapo katika tukio hilo watu 9 walijeruhiwa na mpaka sasa watu 7
tunawashikiria na tunaendelea kuwa hoji ambapo wawili baadhi yao tumewakuta na
silaha Bastola kwani walikuwepo kule katika eneo la tukio kwahiyo tunaendelea
kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani”alisema kamanda
Mjengi
“jana majira ya tatu usiku shimo moja wapo la wachimbaji wadogo wa
madini lilititia na watu nne walifunikwa lakini tayari watatu wameokolewa
lakini mmoja bado anatafuta katika shimo lile hivyo mpaka sasa bado hatujapata
taarifa yoyote hivyo tutawajulisha pindi atakapo patikana”alisema kamanda
Mjenga
Richa ya jeshi la
polisi kufanya doria katika maeneo hayo bado changamoto kubwa inayotajwa ni
uhaba wa mawasiliano yanayochangia kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji wa taarifa
pindi kunapotokea tatizo ambapo wito umetolewa kwa serikali kuboresha
mawasiliano katika eneo hilo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni