Jumamosi, 24 Juni 2017

WANANCHI WA MKOA WA IRINGA WAUNGANA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE

Baadhi ya wananchi waliohudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli
Mbunge vitimaalumu Iringa(kushoto)mkuu wa mkoa wa iringa(katikati)mkuu wa wilaya kilolo(kulia)
Wakuu wa wilaya Iringa,Mufindi na Kilolo

Mamia ya wakazi wa mkoa wa Iringa wameandamana kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamuhuri wya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kutokana na kile anacho kifanya katika kulinda rasilimali za nchi Wananchi na kupigania masilahi ya wanyonge.

Maandamano hayo yaliyopokelewa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza yamefanyika katika viwanja vya mwembetogwa manispaa ya Iringa ambapo yalikusudia kumpongeza Rais Magufuli tangu alipoingia Madarakani kwa kuonesha uzalendo wa kutetea masilahi ya Taifa huku wakimtaka aendelee kufanya kazi hiyo ili kuileta Tanzania mpya huku maandamano hayo yakiwa na kauli mbiu inayoashiria kupingana na vitendo vya baadhi ya watu waliotumia madaraka yao kujinufaisha wenyewe badala ya taifa
Maandamano hayo yameshirikisha watu mbalimbali wakiwemo wanazuoni,Taasisi za serikali na Binafsi ambapo walipata fursa ya kuwasilisha jumbe zao kupitia mabango yao ambapo yote yaliashairia kuunga mkono kazi inayofanywa na seriakali ya awamu ya Tano na kupinga vikali vitendo vya ubadhirifu wa mali za Umma na kumtaka Rais aendelee kufanya kazi bila woga kwani wanaendelea kumuombea ili aweze kuliletea mabadiliko katika Taifa.
Pia taarifa mbalimbali zikatolewa zikilenga kumpongeza na kukubaliana na kazi kubwa inayofanywa na Rais JP Magufuli ambapo baadhi ya makundi yaliyowasilisha Taarifa zao za pongezi ni pamoja na Wazee wa mkoa wa Iringa,Taasisi za Elimu zilizopo mkoani Iringa na wananchi wakiwakilishwa na Mbunge wa Viti maalumu Rita Kabati ambeya katika Taarifa yake aliwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa kujituma kwamaana tayari serikali imetenga bajeti inayogusa maisha yao.

"serikali imetenga bajeti inayogusa maisha ya wananchi wanyonge hivyo tembeeni kifua mbele kwa kuwa seriakali ya awamu hii ni serikali ya wanyonge lazima tuone maisha yakibadilika."alisema kabati

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza katika maandamano hayo aliwataka  wananchi na viongozi wa dini kuungana pamoja katika kuiombea serikali ya awamu ya Tano yenye nia thabiti za kuwaletea maendelea huku akiwataka waendelee kupuuza hoja za baadhi ya watu wanaopinga jitihada hizo kwani hawana nia njema na Taifa.
"niwaombe ndugu zangu wanairinga tuunge mkono mapambano yanyofanywa na serikali hii kwani yana nia njema ya kuifanya Tanzania mpya na yenye manufaa kwa watu wote sisi kama wawakilishi wa Rais mikoani tutafanya kazi ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo pasipo kubagua itikadi wala dini sote ni wamoja"alisema
Richa ya kufanyika kwa maandamano hayo imeelezwa kuwa suala la kulinda amani na usalama wa nchi linapaswa kufanywa na watanzania wote kwani palipo na amani ndipo palipo na maendeleo kwa wananchi wake Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni