Alhamisi, 29 Juni 2017

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA IRINGA ROSE TWEVE AENDELEA NA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI


Zaidi ya kata 107 za mkoa wa Iringa kuanzisha mifuko maalumu ya kuwezeshana kiuchumi kutokana na Fedha zinazochangiwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Rose Tweve ili kuwawezesha wanawake kujitegema na kufanya ujasiliamali pasipo kujali itikadi.

Kutokana na Mpango huo wa Mb Rose tayari Zaidi ya kata 40 za wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi zimekwishanufaika na mpango huo unaokiwezesha kikundi cha wanawake katika kila kata kupata Sh 600,000 ambazo hazirudishwi.

Akizungumza wakati akikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa vikundi vya kata za Nyololo na Malangali, Tweve alisema zoezi hilo litaendelea katika kata zingine zote zilizobaki zitakazokamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo ya kuunda uongozi wake na kufungua akaunti benki.

Tweve alisema kwa kupitia mifuko hiyo itakayojulikana kama mifuko ya Rose Tweve ya kila kata wanawake watajiwekea utaratibu wa kuweka na kukopa, kuinuana kimaendeleo na kubuni mambo mengine yatakayowazidishia kasi ya maendeleo yao.

“Wanawake tupo wengi sana, lakini tunakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoturudisha nyuma. Huu ndio muda wa kujipanga upya na kubadili maisha yetu kwa kutumia kauli mbiu ya rais wetu Dk John Magufuli ya Hapa Kazi tu,” alisema.

Alisema kutakuwepo na utaratibu wa kuvifanyia tathimini vikundi hivyo na vile vitakavyofanya vizuri vitapata nyongeza ya fedha kila mwaka kwa kupitia mpango huo.

“Nimeanzisha mpango huu kwa kutumia rasilimali zangu mwenyewe na kwangu mimi naona hili la kusaidia wanawake wenzangu kwa kutumia rasilimali zangu linawezekana,” alisema.

Alisema matokeo chanya yatakayojitokeza  katika vikundi hivyo yatamshawishi atafute wafadhili wengine wa ndani na nje ili wasaidie zaidi.

“Sitoi fedha hizi ili mgawane kwa matumizi yasiofaa, natoa kama jitihada zangu za kuwahamasisheni kuona haja ya kuwekeza kwa pamoja na kwa manufaa ya wote,” alisema.

Akishukuru kwa mchang huo, mmoja wa viongozi wa kikundi cha wanawake wa mfuko wa Rose Tweve wa kata ya Malangali, Judith Kisinini alisema wako katika mchakato wa kuanzisha duka la kuuza pembejeo za kilimo, hatua itakayowawezesha wanawake wakulima wa kata hiyo kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu.



“Fedha hizo pamoja na michango ukiwemo wa mheshimiwa mbunge na faida tutakayokuwa tunapata kutoka katika shughuli tutakazokubaliana kufanya zitatumika kuendeleza wanachama wote bila ubaguzi wowote,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Nyololo, Grace Mbembati alisema; “mchango waliopata kutoka kwa mbunge huyo utatuongezea kasi katika kutimiza wajibu wetu ili kufikia azma tuliyonayo katika kusaidiana kiuchumi.”

Jumatano, 28 Juni 2017

HALMASHAURI YA WILAYA KILOLO YADHAMILIA KUMALIZA KATIKA SEKTA YA AFYA KWA KUJENGA HOSPITALI YA KISASA

Baadhi ya Majengo ya Hospitali ya Kisasa ya Halmashauri ya wilaya ya Kilolo
Halmashauri ya wilaya kilolo imedhamilia kumaliza kero inazowakabili wananchi hususani katika sekta ya afya kutokana na mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya itakayowahudumia zaidi ya  kata 12 za wilaya hiyo kutokana na kuikosa huduma hiyo kwa muda mrefu na kulazimika kuitafuta katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa

Aloyce Kwezi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Aloisi Kwezi na Asiah Abdallah ni mkuu wa wilaya hiyo waliiambia SAYARI YA HABARI kuwa  halmashaurii hiyo inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya wilaya kwa kushirikliana na wakala wa Majengo nchini TBA ikiwa ni miongoni mwa miradi itakayo kuwa na Tija ya moja kwa moja kwa wanachi kutokana na adha waliyoipata ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa muda wa miezi 8 kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi ambapo mpaka hivi sasa imesalia miezi miezi 2 kumalizika kwa muda uliotengwa ili wananchi kuanza kuifurahia halmashauri yao.

Viongozi hao wa Halmashauri ya wilaya kilolo walisema kutokana na Jografia ya wilaya hiyo changamoto kubwa ni namna wananchi wanavyoweza kupata huduma za afya hususani wakazi wa vijiji vya Kiwalamo na Ruaha Mbuyuni ambapo walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kuitafuta huduma hiyo huku baadhi ya wananchi wakipoteza ndugu zao wakiwa njiani kufuata huduma za afya ambapo hivi karibuni itabaki historia.

“hapo awali wananchi wa kilolo wamepata shida sana pale wanapopata maradhi hasa wanawake wajawazito waliokuwa wanahitaji huduma ya dharura(upasuaji)kwa kuwa katika Halmashauri yetu hatukuwa na hospitali kubwa walilazimika kwenda Iringa mjini katika hospitali ya Rufaa au kwenda katika hospitali Teule ya Ilula jambo lililosababisha baadhi ya akina mama na watoto kupoteza maisha wakiwa njiani tulikuwa hatuna namna”.walisema viongozi hao

“wanaendelea kusema kwasasa tunao mradi mkubwa wa ujenzi wa hospitali unaogharimu kiasi cha shilingi billion 4.2 hii itakuwa hospitali ya mfano kwani tunamajengo matano ya Ghorofa moja moja yanaendelea kujengwa hisa sasa yanakaribia kuanza shughuli za upauaji na kufikia mwezi wa nane tunaweza kuwa katika hatua ya umaliziaji na wananchi wataanza kufurahia upatikanaji wa huduma za afya na itasaidia sana kupunguza foleni katika hospitali za Rufaa na Hospitali ya Manispaa ya iringa.”walisema

Akizungumzia ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya kilolo Valensi Kihwaga alisema Halmashauri imeendelea na uelimishaji wa wananchi katika kutambua umuhimu wa miradi iliyopo ili waweze kuisimamia na kiutumia ipasavyo huku akiwataka waendelee kuonesha ushirikiano kwa serikali katika kutekeleza miradi hiyo.

“mimi nisema tu Halmashauri yetu imedhamiria kumaliza kero za wananchi kwa kiasi kikubwa na hasa kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe na tumeendelea kutoa elimu ya kutosha kwao ili wao ndiyo wawe wamiliki wa miradi ya maendeleo hasa hii Hospitali kubwa ambayo tunaijenga kama serikali tutahakikisha tunasimamia na kukamilisha kwa wakati ujenzi wake na ianze kutoa huduma”alisema kihwaga

Halmashauri ya Kilolo kwa ujumla imekusudia kupunguza kero za huduma za Jamii kwa wananchi ikiwemo miradi ya barabara,Maji na Elimu ili kufanya wilaya hiyo ikue kiuchumi.

WAKAZI WA MTAA WA TAGAMENDA MANISPAA YA IRINGA MIAKA 3 WAKOSA HUDUMA YA MAJI SAFI YA KUNYWA

Wananchi wa mtaa wa Tagamenda katika manispaa ya Iringa wamelalamikia adha ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama ya kunywa kwa kipindi cha miaka 3 huku uongozi wa serikali ya manispaa hiyo ukishindwa kutatua changamoto hiyo jambo linalosababisha wananchi hao kufuata maji katika mto ruaha na kuhatarisha maisha yao.

Wakizungumza na SAYARI YA HABARI iliyofika mtaani hapo na kukutana na baadhi ya wananchi wanaokubwa na adha hiyo ambapo wamelalamikia kutelekezwa na serikali huku wakipigwa porojo ya kutatuliwa kwa kero hiyo walisema wamekuwa wakitafuta maji katika mtoRuaha ambapo maji hayo hutumiwa na wanayama,Kuoga,kufua huku yakitumiwa kwa kunywa binadamu huku vitendo vya kubakwa na kufanyanyiwa kuatili vikitishia maisha yao jambo lililowalazimu wanaume kuanza kuwasindikiza wake zaokutafuta maji.

Sara Edoga ni miongoni mwa Wakazi hao ambao wamekuwa wakipata adha na usumbufu mkubwa kwa kufuata maji na kutumia kutoka mto wa Ruaha alisema amekuwa akibeba maji mgongoni kutokana na umri wake kuwa mkubwa hali inayomfanya ashindwe kujitwisha kichwani na ndipo akapaza sauti.

“hapa tunashida ya maji na Umeme kwa zaidi ya miaka 3 tunatumia maji ya mto Ruaha tunatia huruma tumetelekezwa kama kisiwa kwa umri wangu nalazimika kubeba mgongoni maji wakati yamepita hapo chini shule ya Sekondari Tagamenda tuoneeni huruma mbona tupo manispaa”alisema mama huyo kwa huruma

Naye Willium Fungo ni mzee wa mtaa huo kwa uchungu alisema kumekuwa na kauli za baadhi ya viongozi wanaosema eneo la Mtaa wa Tagamenda ni eneo la milimani hivyo hawawezi kupatiwa huduma ya maji jambo linalowafanya wajiulize maswali iweje kauli hizo ikiwa kodi za majengo zinatozwa?akaongeza kusema kasi ya ukuji wa mtaa huo ni kubwa wapo karibu na kituo cha Shirika la Umeme TANESCO lakini hawana pia umeme jambo linalowakatisha Tamaa kushiriki katika shughuli za maendeleo.

“hatuna maji,hatuna Umeme zote ni shida zetu zinatukabili,sasa kuna utaalamu fulani um ekuja wa kusema tuweke maji chooni hivi utaweka maji wakati hayapo na msishangae kuja hapa mnakuta watoto wachafu yote hii ni kwa sababu ya kukosa maji tunateseka sana heri tukose chakula lakini tupate maji safi ya kunywa”alisema mzee huyo

Kwa upande wao baadhi ya Madiwani Dora Nziku vitimaalum ,Bashir Mtove na Mahadhi Hepautwa walizuru katika mtaa huo ili kujionea adha wanayoipata wananchi hao wamesema richa ya mateso na shida wanazozipata za kukosa maji lakini wao kwa umoja wao wamewahakikishia kushughulikia kero hiyo ili kuwaokoa wanawake na vitendo viovu.

“nikweli sisi ni madiwani kutoka kata tofauti tofauti mara baada ya Kusikia kilio cha wananchi hawa ambao ni walipakodi katika Manispaa yetu Tumeamua kufika ili tujionee wenyewe na tuchukue hatua ya kuwasaidia tumeo hali hii siyo nzuri hata kidogo wapo kama kisiwani tuwaahidi wananchi hawa kuwa kero hii sasa imefika mwisho” walisema

Hatimaye Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Iringa Rita Kabati akajitokeza na kuzungumzia changamoto hiyo huku akishangazwa na kauli za baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakidai kuwa katika manispaa ya Iringa hakuna Tatizo la ukosefu wa huduma ya maji na kuwaahidi kuitatua kero hiyo katika kipindi cha muda mfupi ujao.

“nimekuja huku kwa masikitiko makubwa kwani ninaposikia kero ya maji naumia ninapomuwazia mwanamke mwenzangu anayepata adha na kodi analipa na anakabiliwa na vitendo vya ubakaji kwa kufuata maji umbali mrefu imeniuma sana kwanini tunawadanganya wananchi waendelee kupata shida hizi mimi kama kiongozi naanza leo kufuatilia kero hii hapa mnahaki ya kupata maji kama wanavyopata watu wengine mnayo haki ya kupata umeme tena kwakuwa upo karibu hapa.”alisema Kabati


Mtaa wa Tagamenda una zaidi ya kaya 30 na upo umbali wa kilomita 2 kutoka kilipo kituo cha mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iruwasa na mita 800 kilipo chanzo cha umeme wa TANESCO cha Tagamenda lakini mtaa huu hauna maji wa Umeme hali inayowapa shida wananchi na kuwa hatarini kuugua maradhi kutokana na kutumia maji yasiyo salama.

Jumapili, 25 Juni 2017

SAYARI YA HABARI TUWATAKIA WAISLAMU WOTE EID MUBARAK

Image result for eid mubarak
Leo ni siku muhimu nkwa waumini wa Dini ya Kiislamu Duniani kote ambapo mara baada ya kushiriki katika mwezi wa kujiweka karibu na Mungu na kutafakari ukuu wake katika maisha yetu hatimaye leo tumefika salama na kufungua salama.

Kwaniaba ya watanzania wote mtandao wa Sayari ya Habari tunapenda kuwatakia Waislamu wote EID MUBARAK tusherehekee sikuu hii kwa Amani na Furaha tukiendelea kutafakari maisha yetu na namna tunavyozitumia Nafasi zetu katika kujiletea Maendeleo yetu na Taifa Kwaujuml

TUNAKUTAKIA SIKUU NJEMA

VIONGOZI WA DINI NA SERIKALI WAHIMIZWA KUWA NA UZALENDO NA NCHI YAO

  • Acheni kuwatisha wananchi kuweni na Unyenyekevu
  • Suala la kodi katika mashirika ya Dini kikwazo na mzigo kwa uendeshaji wa huduma
  • Serikali iendelee kuwatumikia wananchi kwa misingi ya sheria 
Askofu Dkt Fredlick Shoo Mkuu wa Kanisa KKKT

Askofu wa Dayosisi ya Iringa Braston Gavile(kulia)na Msaidizi wa Askofu Hamidu Saga(kushoto)

Maaskofu waliohudhuria Ibada ya Kuwekwa wakfu Askofu mpya Dayosisi ya Iringa Mch Braston Gavile

Jamuhuri Wiliumu Mkuu wa Wlaya ya Mufindi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa


Viongozi wa Dini na Serikali nchini wametakiwa kuwa na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua wala kutangukiza masilahi yao jambo linaloweza kuwagawa watanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Askofu Dkt Fredrick Shoo wakati wa ibada ya kumumweka wakfu na kumuingiza  kazini Askofu Mpya wa Dayosisi ya Iringa ambapo amesema ni vema kila kiongozi akatumia madaraka yake kwa kuwatumikia wananchi badala ya kutumia vitisho na kutumia mamlaka yao vibaya jambo linaloshusha heshima kwa viongozi kutokana na matendo yao.

“ndugu zangu viongozi wa kiroho na seriakli mliopo hapa tumepewa mamlaka kuwaongoza watanzania siyo kwa kuwatisha bali ni kwa unyeyekavu ili tuwasaidie watambue uhuru wao heshima ya kiongozi yeyote itakuja kwajinsi ulivyowatimikia watu wa Mungu,Mungu amekupa nafasi hiyo ili uwatumikie watanzania ili tuiinue nchi yetu taifa letu lisonge mbele kimaendeleo”alisema Askofu Shoo

Aidha Mkuu huyo wa Kanisa hakusita kuwanyoshea kidole baadhi ya viongozi wanaotumia nafasi zao kwa kujinufaisha wenyewe  badla ya kujali masilahi mapana ya nchi na kuendelea kuona wao ni zaidi kuliko watu wengine hivyo amewataka viongozi wa serikali na Dini nchini kuwa na uzalendo na nchi yao.

“yapo mambo ya aibu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi waliolitumikia Taifa hili  badala ya kufanyakazi ili watu wote wanufaike unakaa kusaini mkataba ambao unaiumiza nchi yako unajiita umesoma hebu tuipende nchi yetu badala ya kuuza nchi kwa masilahi binafsi na kuingia mikataba na mabeberu wa nje.”alisisitiza Shoo

Akizungumza mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Iringa Mch Braston Gavile richa ya kupongeza kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya Tano hakusita kuzungumzia kilio cha Taasisi za dini kutokana na tozo la Kodi katika huduma wanazozitoa ikiwemo Afya na Shule kuwa zimekuwa zikitozwa kodi kubwa bila kutambua taasisi hizo hazifanyi  biashara bali zinatoa huduma.

“taasisi za dini zinashindwa kuendelea kutoa huduma kutokana na kodi zimezidi ikumbukwe kuwa taasisi hizi hazifanyi biashara bali zinatoa huduma tunaomba seriakali yetu iangalie kwa upya suala la kodi nchini  kwa mashirika ya Dini kwamaana kodi hizo zimekuwa mzigo mkubwa katika uendehaji wa huduma hizo”alisema Askofu Gavile
Jamuhuri Wilium ni mkuu wa wilaya ya Mufindi akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa amesema serikali inayoimani kubwa kwa makanisa kwa kazi ya kutoa mafundisho na kukemea maovu jambo linalofanya kuongeza ushirikiano baina ya mihimili hiyo miwili ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Dini kuendelea kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Tanzania ili aendelee kuwatumikia watanzania na kutetea rasilimali za nchi,

“serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za Dini kwani tunatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizi tunakupongeza Baba Askofu kwa kuaminiwa na leo unaanza kuwatumikia wananchi rasmi mimi niseme tuiunge mkono serikali na tuiombee ifanye vizuri katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.”alisema mkuu wa wilaya 

Kanisa la Kiinjili Tanzania ni miongoni mwa makanisa yenye waumini wengi ambapo kwasasa lina jumla ya waumini zaidi ya million 6.7 ambapo wameaswa kuendelea kujituma kufanya kazi ili kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla.

MCHUNGAJI BRASTON GAVILE ASIMIKWA RASMI KUWA ASKOFU WA DAYOSISI YA IRINGA KKKT

Askofu Braston Gavele akiwa katika kiti cha Askofu kuanza kazi rasmi kuiongoza Dayosisi ya Iringa
Wakuu wa wilaya Kilolo,Mufindi na Iringa wakijadili Jambo katika Ibada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Iringa

Askofu Mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na Katibu mkuu wa Dayosisi hiyo Nayman Chavala wakimkabidhi Hati ya Uaskofu Askofu mpya Braston Gavile


Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt Frederick Shooakimwingiza kazini Askofu Gavile
 Hatimaye Dayosisi ya Iringa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT imeingia rasmi katika ukurasa mwingine mara baada ya kuapishwa na kuingizwa rasmi Askofu Mpya wa Dayosisi hiyo Mch Braston Gavile ambaye naye amemuapisha mch Himidu Sanga kuwa msaidizi wa Askofu katika
kanisa hilo.

Ibada ya kuwekwa wakfu kwa mchungaji Braston Gavile imehudhuriwa na waumini wa kanisa hilo kutoka maeneo Tofautitofauti katika mkoa wa Iringa,viongozi wa serikali na Maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi.

Miongoni mwa shughuli zitakazofanywa na Askofu Huyo ni pamoja na kusimamia shughuli zote na huduma katika Dayosisi,kuwa msemaji mkuu wa Dayosisi kwa Serikali,Kushiriki katika mkutano mkuu wa Dayosisi kama mwenyekiti,Kuidhinisha kusimamishwa kazi kwa mtumishi yeyote atakyefanya kinyume na Taratibu na mengineyo.

ENDELEA KUWA NASI TUTAKUJUZA YOTE YANAYOENDELEA

IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILE DAYOSISI YA IRINGA



 Waumini wa kanisa la kiinjili Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa wameungana pamoja katika viwanja vya Shule ya msingi Gangilonga kumpokea Askofu Mpya wa Kanisa hilo Mch Blaston Gavile ili kuanza kuongoza Rasmi kanisa hilo huku Ibada hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Kanisa KKKT  Askofu Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella.

Askofu Mteule Gavile anachukua mikoba inachwa na Askofu Owdenburg Mdegella aliyeongoza Dayosisi hiyo kwa zaidi ya miaka 30 ambapo Askofu Mdegela katika kipindi cha uongozi wake amefanikisha kuanzisha miradi mbalimbali ili kulifanya kanisa hilo liweze kujiendesha lenyewe pasipo kutegemea ufadhiri hii inatajwa kuwa ni miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata katika uongozi wake huku waumini wa kanisa hilo wakisubiri kuona mabadiliko makubwa zaidi kutoka kwa Mch Gavile.


Endelea kutufuatilia tukujuze kila kinachojili.


Jumamosi, 24 Juni 2017

WANANCHI WA MKOA WA IRINGA WAUNGANA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE

Baadhi ya wananchi waliohudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli
Mbunge vitimaalumu Iringa(kushoto)mkuu wa mkoa wa iringa(katikati)mkuu wa wilaya kilolo(kulia)
Wakuu wa wilaya Iringa,Mufindi na Kilolo

Mamia ya wakazi wa mkoa wa Iringa wameandamana kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamuhuri wya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kutokana na kile anacho kifanya katika kulinda rasilimali za nchi Wananchi na kupigania masilahi ya wanyonge.

Maandamano hayo yaliyopokelewa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza yamefanyika katika viwanja vya mwembetogwa manispaa ya Iringa ambapo yalikusudia kumpongeza Rais Magufuli tangu alipoingia Madarakani kwa kuonesha uzalendo wa kutetea masilahi ya Taifa huku wakimtaka aendelee kufanya kazi hiyo ili kuileta Tanzania mpya huku maandamano hayo yakiwa na kauli mbiu inayoashiria kupingana na vitendo vya baadhi ya watu waliotumia madaraka yao kujinufaisha wenyewe badala ya taifa
Maandamano hayo yameshirikisha watu mbalimbali wakiwemo wanazuoni,Taasisi za serikali na Binafsi ambapo walipata fursa ya kuwasilisha jumbe zao kupitia mabango yao ambapo yote yaliashairia kuunga mkono kazi inayofanywa na seriakali ya awamu ya Tano na kupinga vikali vitendo vya ubadhirifu wa mali za Umma na kumtaka Rais aendelee kufanya kazi bila woga kwani wanaendelea kumuombea ili aweze kuliletea mabadiliko katika Taifa.
Pia taarifa mbalimbali zikatolewa zikilenga kumpongeza na kukubaliana na kazi kubwa inayofanywa na Rais JP Magufuli ambapo baadhi ya makundi yaliyowasilisha Taarifa zao za pongezi ni pamoja na Wazee wa mkoa wa Iringa,Taasisi za Elimu zilizopo mkoani Iringa na wananchi wakiwakilishwa na Mbunge wa Viti maalumu Rita Kabati ambeya katika Taarifa yake aliwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa kujituma kwamaana tayari serikali imetenga bajeti inayogusa maisha yao.

"serikali imetenga bajeti inayogusa maisha ya wananchi wanyonge hivyo tembeeni kifua mbele kwa kuwa seriakali ya awamu hii ni serikali ya wanyonge lazima tuone maisha yakibadilika."alisema kabati

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza katika maandamano hayo aliwataka  wananchi na viongozi wa dini kuungana pamoja katika kuiombea serikali ya awamu ya Tano yenye nia thabiti za kuwaletea maendelea huku akiwataka waendelee kupuuza hoja za baadhi ya watu wanaopinga jitihada hizo kwani hawana nia njema na Taifa.
"niwaombe ndugu zangu wanairinga tuunge mkono mapambano yanyofanywa na serikali hii kwani yana nia njema ya kuifanya Tanzania mpya na yenye manufaa kwa watu wote sisi kama wawakilishi wa Rais mikoani tutafanya kazi ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo pasipo kubagua itikadi wala dini sote ni wamoja"alisema
Richa ya kufanyika kwa maandamano hayo imeelezwa kuwa suala la kulinda amani na usalama wa nchi linapaswa kufanywa na watanzania wote kwani palipo na amani ndipo palipo na maendeleo kwa wananchi wake Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.


Ijumaa, 23 Juni 2017

Salah surprises Liverpool fans on Anfield tour

VIDEO: Salah surprises Liverpool fans on Anfield tour
The new signing started making friends with his new club's fan base on his first day, visiting with a group of supporters as they toured the stadium
Mohamed Salah is already making friends with Liverpool supporters, and the club's record signing has barely been a member of the team for a full day.
The hype around the Egyptian joining the club has been massive, with manager Jurgen Klopp claiming that the former Chelsea winger has everything he needs to win big at Liverpool and the player himself saying that people should expect something different than what they saw from him with the Blues.
Gotze hints at BVB return
Still, endearing yourself to the fanbase seems like a great idea for any new signing and Salah has hit a master-stroke in that department, making the day of some supporters with a surprise visit to an Anfield tour group.
The winger stopped to take photos with the group of fans and signed a few autographs along the way.
And this was just his first day at Anfield!
It's a savvy move from the former Roma star, but if he really wants to make friends in Liverpool he can help the club claim a Premier League title next season.

WATANZANIA WATAKIWA KULINDA AMANI NA UMOJA KATIKA TAIFA


Asiah Abdallah Mkuu wa Wilaya ya Kilolo

Bi Amina Masenza mkuu wa Mkoa wa Iringa akizungumza na umati wa watu walialikwa katika Futari
Richard Kasesela mkuu wa Wilaya ya Iringa
Jamuhuri Wilium Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Baadhi ya waalikwa katika Futari ya Mkuu wa Wilaya Kilolo


Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini wamemetakiwa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa jamii ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali katika kuliletea Taifa maendeleo.

Akizungumza katika Hafla ya futari iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo mkuu wa mkoa wa iringa Amina Masenza alisema katika baadhi ya maeneo kumeibuka Tabia ya baadhi ya watu kutumia kigezo cha Dini kufanya vitendo viovu ikiwemo utapeli jambo linalolenga kuchafua Uislamu huku akitumia nafasi hiyo kutoa wito kuiunga mkono serikali katika kuhakikisha inawaletea maendeleo ya kweli wananchi.

“niwaombe ndugu zangu waislamu tunapowaona watu tunaowatilia mashaka wanakuja katika maeneo yetu ya Ibada wakijifanya waislamu kumbe wanamambo yao wanafanya hebu tutoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwani uislamu utalindwa na waislamu wenyewe lakini pia ndugu zangu niwaombe tushirikiane na serikali katika kujiletea maendeleo”alisema mkuu huyo wa mkoa

Aidha katika hatua nyingine Masenza alitoa wito kwa wananchi kutunza chakula hususani katika msimu huu wa mavuno ambapo mara nyingi baadhi ya wananchi hutumia mazao yao kwa pupa na mwishowe hujikuta wameishiwa kabisa hivyo alisema ni vyema wananchi wakahifadhi chakula bila kusahau utunzaji wa mazingira hususani vyanzo vya maji kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

“nitoe wito kwa wananchi wote waone umuhimu wa kutunza chakula kwani tusipofanya hivyo tatizo la njaa litatumaliza wapo wenye tamaa ya fedha wanauza mazao yao bila kuweka akiba niwaase tunzeni chakula chakutosha kwaajili ya familia zenu lakini pia mkumbuke utunzaji wa mazingira hasa katika vyanzo vya maji ni muhimu kwasasa na baadae mazingira ni uhai”alisema Masenza

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Kilolo Asiah Abdallah akizungumza wakati akiwakaribisha wageni waliohudhuria hafla hiyo ya Futari hakusita kuwakumbusha watanzaniani kuwa nchi hii imepata Rais ambaye Mungu amemchagua jambo la msingi ni kumuunga mkono kwa kazi zake anazofanya maana wapo wanaombeza hivyo aliwataka watanzania kuwapuuza watu hao.

“kila analolipanga mungu lazima litimie Mwenyezi Mungu alipanga Tanzania kuanzia mwaka 2015/2020 tuwe na Rais shupavu John Pombe Magufuli na imekuwa hatuna budi kumuunga mkono kwa yote anayoyafanya kwa masilahi ya watanzania wote “alisema mkuu huyo wa wilaya

Naye Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jumuhuri Willium richa ya kuwataka wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu kutumia vyema mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani aliitaka jamii ijikite katika kuombea amani na umoja wa nchi yetu  hata mara baada ya kumaliza mufungo huo.

“ningependa sana tuutumie mwezi huu wa Ramadhani katika kujitafakari na kumurudia muumba wetu maana kwake ndiko tunakopata Amani tudumishe amani na upendo miongoni mwetu na jamii inayotuzunguka”alisema Jamuhuri

Lakini pia mkuu wa wialaya ya Iringa Richard Kasesela ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafula hiyo ambaye aliwataka waumini wa Dini ya Kiisilamu kutumia uislamu kwa kufanya matendo yanayompendeza Mungu kwani wapo wanaoamini kuwa na alama katika Paji la Uso ndiyo kipimo cha ukamilifu wake bali ni vile wanavyoenda.

Awali wakizungumza katika hafla hiyo Mashekhe wa Mkoa na Wilaya ya Kilolo Abubakari Chalamila na wameitaka seriakali kuwashirikisha katika utoaji wa matamko kwani ipo tofauti pindi tamko linapotolewa na Kiongozi wa Dini jamii huelewa zaidi kuliko linapotolewa na kiongozi wa kisiasa.

“kauli za viongozi wa Dini husikilizwa na huaminiwa zaidi kuliko kauli za wanasiasa tutumieni kwa kuwa yote yanayopigiwa kelele na serikali hii yapo katika vitabu vya mungu nasi tunao wajibu wa kukemea na kuonya pale mtu anapofanya kinyume na agizo la Mwenyezi Mungu hivyo tushirikiane kuijenga nchi yetu”walisema mashekhe

Ilielezwa kuwa miongoni mwa matendo yanayochochea umoja na Mshikamano miongoni mwa jamii ni pamoja kukaa pamoja kila mmoja akitafakari namna anavyoweza kulinda na kusimamia amani iliyopo kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaunganisha watanzania.