Wananchi wa mtaa wa Tagamenda
katika manispaa ya Iringa wamelalamikia adha ya ukosefu wa huduma ya maji safi
na salama ya kunywa kwa kipindi cha miaka 3 huku uongozi wa serikali ya
manispaa hiyo ukishindwa kutatua changamoto hiyo jambo linalosababisha wananchi
hao kufuata maji katika mto ruaha na kuhatarisha maisha yao.
Wakizungumza na SAYARI YA
HABARI iliyofika mtaani hapo na kukutana na baadhi ya wananchi wanaokubwa na
adha hiyo ambapo wamelalamikia kutelekezwa na serikali huku wakipigwa porojo ya
kutatuliwa kwa kero hiyo walisema wamekuwa wakitafuta maji katika mtoRuaha
ambapo maji hayo hutumiwa na wanayama,Kuoga,kufua huku yakitumiwa kwa kunywa
binadamu huku vitendo vya kubakwa na kufanyanyiwa kuatili vikitishia maisha yao
jambo lililowalazimu wanaume kuanza kuwasindikiza wake zaokutafuta maji.
Sara Edoga ni miongoni mwa
Wakazi hao ambao wamekuwa wakipata adha na usumbufu mkubwa kwa kufuata maji na
kutumia kutoka mto wa Ruaha alisema amekuwa akibeba maji mgongoni kutokana na
umri wake kuwa mkubwa hali inayomfanya ashindwe kujitwisha kichwani na ndipo
akapaza sauti.
“hapa tunashida ya maji na
Umeme kwa zaidi ya miaka 3 tunatumia maji ya mto Ruaha tunatia huruma
tumetelekezwa kama kisiwa kwa umri wangu nalazimika kubeba mgongoni maji wakati
yamepita hapo chini shule ya Sekondari Tagamenda tuoneeni huruma mbona tupo
manispaa”alisema mama huyo kwa huruma
Naye Willium Fungo ni mzee wa
mtaa huo kwa uchungu alisema kumekuwa na kauli za baadhi ya viongozi wanaosema
eneo la Mtaa wa Tagamenda ni eneo la milimani hivyo hawawezi kupatiwa huduma ya
maji jambo linalowafanya wajiulize maswali iweje kauli hizo ikiwa kodi za
majengo zinatozwa?akaongeza kusema kasi ya ukuji wa mtaa huo ni kubwa wapo
karibu na kituo cha Shirika la Umeme TANESCO lakini hawana pia umeme jambo
linalowakatisha Tamaa kushiriki katika shughuli za maendeleo.
“hatuna maji,hatuna Umeme zote
ni shida zetu zinatukabili,sasa kuna utaalamu fulani um ekuja wa kusema tuweke
maji chooni hivi utaweka maji wakati hayapo na msishangae kuja hapa mnakuta
watoto wachafu yote hii ni kwa sababu ya kukosa maji tunateseka sana heri
tukose chakula lakini tupate maji safi ya kunywa”alisema mzee huyo
Kwa upande wao baadhi ya
Madiwani Dora Nziku vitimaalum ,Bashir Mtove na Mahadhi Hepautwa walizuru
katika mtaa huo ili kujionea adha wanayoipata wananchi hao wamesema richa ya
mateso na shida wanazozipata za kukosa maji lakini wao kwa umoja wao
wamewahakikishia kushughulikia kero hiyo ili kuwaokoa wanawake na vitendo
viovu.
“nikweli sisi ni madiwani
kutoka kata tofauti tofauti mara baada ya Kusikia kilio cha wananchi hawa ambao
ni walipakodi katika Manispaa yetu Tumeamua kufika ili tujionee wenyewe na
tuchukue hatua ya kuwasaidia tumeo hali hii siyo nzuri hata kidogo wapo kama kisiwani
tuwaahidi wananchi hawa kuwa kero hii sasa imefika mwisho” walisema
Hatimaye Mbunge wa Vitimaalumu
mkoani Iringa Rita Kabati akajitokeza na kuzungumzia changamoto hiyo huku akishangazwa
na kauli za baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakidai kuwa katika manispaa ya
Iringa hakuna Tatizo la ukosefu wa huduma ya maji na kuwaahidi kuitatua kero
hiyo katika kipindi cha muda mfupi ujao.
“nimekuja huku kwa masikitiko
makubwa kwani ninaposikia kero ya maji naumia ninapomuwazia mwanamke mwenzangu
anayepata adha na kodi analipa na anakabiliwa na vitendo vya ubakaji kwa
kufuata maji umbali mrefu imeniuma sana kwanini tunawadanganya wananchi
waendelee kupata shida hizi mimi kama kiongozi naanza leo kufuatilia kero hii
hapa mnahaki ya kupata maji kama wanavyopata watu wengine mnayo haki ya kupata
umeme tena kwakuwa upo karibu hapa.”alisema Kabati
Mtaa wa Tagamenda una zaidi ya
kaya 30 na upo umbali wa kilomita 2 kutoka kilipo kituo cha mamlaka ya maji
safi na usafi wa mazingira Iruwasa na mita 800 kilipo chanzo cha umeme wa
TANESCO cha Tagamenda lakini mtaa huu hauna maji wa Umeme hali inayowapa shida
wananchi na kuwa hatarini kuugua maradhi kutokana na kutumia maji yasiyo
salama.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni