![]() |
| Vyakula vilivyokabidhiwa na Mstahiki Meya manispaa ya Iringa katika kituo cha Kitanzini Islamic Centre kwa n iaba ya Mbunge Msigwa |
![]() |
| Mstahiki Meya Elex Kimbe akikabidhi chakula kwaajili ya Futari |
Kutokana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili
katika jamii hususani vijana Viongozi wa Dini wametakiwa kutumia nafasi zao
katika kufundisha mbinu masuala ya maadili katika misikiti na Makanisani
kutokana na kuaminiwa zaidi na waumini wao.
Rai hiyo ilitolewa na mstahiki Meya Manispaa ya Iringa wakati akikabidi msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea Vijana kilichopo kitanzini manipaa ya Iringa kwaniaba ya Mbunge wa Jimbo hilo ambapo pamoja na kuwasilisha salamu kutoka kwa Mb Msigwa,Kimbe alisema kwakuwa waumini wa Kiislamu Duniani kote wakiwa kwenya mfungo au mwezi mtukufu wa Ramadhan ni vema jamii ikatumia mwezi huu kumrudia muumba wao na kuacha maovu.
Kimbe amesema yapo mengi yanayochangia mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana ila miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na baadhi ya wanajamii kuishi kwa kutokumuogopa mwenyezi Mungu hivyo kila mtu pale anapoishi anaowajibu wa kufanya jambo linaloweza kufanya mabadiliko chanya kwa jamii inayomzunguka hivyo aliwataka viongozi wa dini kutumia nafasi zao za kuwalea na kuwafundisha vijana maadili mema.
“wito wangu kwa viongozi wa Kiislamu na madhebu mengine ningependa watumie nafasi zao kwani wao ndiyo wanayonguvu ya kukemea na kufundisha vijana ili waishi kwa kumuogopa Mungu kwa kwa kuishi hivyo kunasaidi kuwa na watu ambapo wanajua wajibu wao na taifa litakuwa na watu wanaoweza kuliletea Taifa maendeleo”alisema kimbe
Kimbe amakabidhi chakula chenye thamani ya Tsh million 3 ambacho ni Tende,Tambi na Sukari mifuko 20 ambavyo alisema vyakula hivyo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa lengo la kuendelea kuonesha ushirikiano baina ya jamii hivyo aliwaomba kuunga mkono na kumuombea katika majukumu yake kwa manufaa ya watu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla.
“Mh Mbunge Peter Simon Msigwa alitamani sana awepo mwenyewe ili ale Futari pamoja na Waislamu lakini kwa bahati mbaya yupo katika majukumu ya kibunge lakini tunapenda mjue kuwa dhamira ya mbunge ni njema hivyo tunaomba mvipokee vyakula hivi tunaamini vitasaidia katika mwezi huu Mtukufu”alisema kimbe
Akizungumzia dhana ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani Mfadhiri wa kituo hicho alisema katika imani mwezi huu unalenga kuwa ni darasa la kuwafanya watu kumrudia muumba wao hivyo sit u katika mwezi huu bali Mwenyezi Mungu anakataa matendo maovu bali katika kumkumbuka yeye na kutenda yale yanayompendeza alisema mmomonyoka wa maadili unatoka na baadhi ya watu kuishi maisha yasiyo mwelekea Muumba.
“niseme tafusri nyepesi iliyopo ndani ya mwezi huu ni darasa la kukumbushana namna ya kuwa karibu na muumba sasa kuna mengi ameamlisha na mengine kuyakataza nayo ni haya ambayo hayafurahishi hivyo tunasema ni mwezi darasa ili kuanza kujizoesha kuwa karibu na Mungu Dini zi=ote zimeelekeza watu kuacha Tabia isiyo mpendeza Mungu”alisema
Ostaz Omary Amiry Kasimu ni msimamizi msaidizi wa
kituo hicho alisema vijana wanatakiwa kujitambua kuwa wao ndiyo zao jipya baada
ya wazee hivyo wanatakiwa kuyakubali maadili na maelekezo ya wazee huku wakiwa
na utayari wa kupokea maelekezo ya wazee na viongozi ili yawafae katika maisha
yao na familia zao pamoja na Taifa kwani Taifa linawategemea vijana wajitambue.
“maadili hayawezi kuingia ikiwa vijana wenyewe
hawatakuwa tayari kuyapokea maelekezo ya wazee bali wakikubali kujitambua na
kupokea maelekezo naamini suala la maadili litazingatiwa hata sisi tulilelewa
na kuelekezwa na wazee tukayakubali na tukayafuata hivyo vijana wanatakiwa
wazingaztie na kuyafuata maelekezo ya wazee wakifuata watakuwa wtu wazuri”alisema




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni