![]() | |||||||||
| Wakulima wakipembua na kuundaa vitunguu ili kutafuta wateja |
Idhaa Ally ni miongoni mwa wakulima wa vitunguu katika neneo
hilo alisema kuwa kutokana na changamoto hizo wakulima wengi wameathirika
kiuchumi na kisaikolojia kutokana na wakulima wengi kukopa fedha benki kwa
ajili ya kilimo lakini mwisho wake wameambulia patupu.
“kilimo cha vitunguu kinatumia gharama kubwa kuanzia kuandaa
shamba na matunzo ya mazao lakini ukija kwenye mavunohatupati faida ila
changamoto inakuja kwenye soko na ukiangalia wengi wetu wakulima tumechukua
mikopo na mikopo hiyo tunashindwa kurudisha kutokana na mazao
kutonunulika.”alisema Ally.
Naye Chacha Omary alisema kuwa pembejeo za kilimo zimekuwa
gharama kubwa sana kiasi cha wakulima wadogo kushindwa kumudu gharama hzo na
aliiomba serikali kupunguza gharama za pembejeo za kilimo ili wakulima wadogo
waweze kumudu gharama za pemebejeo hizo.
Kwa upande wake Elizabeth Chilala ambaye amelima hekari
mbili alisema kuwa ametumia zaidi ya Mil.4.5 lakini ameambulia kupata magunia
70 tu hali ambayo imemkatisha tamaa ya
kuendelea kulima zao hilo kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.
“Hapa nimelima hekari mbili,nimetumia Mil.4.5 na nimepata
gunia 70 licha ya kwamba kanuni zote za kilimo nimefuata,na kukokana na
kukosekana kwa masoko ya uhakika vitunguu vyangu vitaozea shambani.”alisema
Chilala
Chilala alisema kuwa matarajio yake alikuwa auze gunia moja
kwa sh.100,000 hadi 150,000 lakini hali imekuwa tofauti na kulazimika kuuza kwa
gunia moja 50,000.
Naye ofisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Lucy
Nyalu alikiri changamoto hiyo na kusema wao kama serikali wanawahamasisha
wakulima kulima kilimo cha kibiashara ili kujihakikishia kuwa na kipato pamoja
na chakula cha uhakika.
Kuhusu masoko alisema kuwa wakulima wengi wanapoona fursa
kwenye kitunguu wengi wao wanakimbilia kulima zao hilo badala ya wachache
kulima na wengine kuendelea kulima mazao mengine hali inayowasababishia kwa
sasa kulima kulima kwa wingi na kukosa masoko.
Nyalu alisema wao kwa sasa wanahamasisha wakulima kulima
kilimo cha mkataba ambacho wanahamasisha kupitia (SAGCOT).
“Mtu azalishe pale anapokuwa ana mtu wa kununua hivyo
ukipata mnunuzi anakuambia niletee tani kadhaa lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti
mazao yamekuwa mengi sokoni,bei imepungua kutokana na gharama alizotumia
kuzalisha.”alisema Nyalu.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
ya Iringa Vijijini Robert Masunya alisema kuwa halmashauri inatambua masuala ya
lumbesa na pia inatambua sheria ya wakala wa vipimo ya mwaka 2002 sura ya 340
ambayo inatoa mwelekeo mzima juu ya usimamizi wa mazao kwa kuzingatia uzito.
“Kwa mfano mahindi ujazo usizidi Kilo 90,nyanya kwa teka
kilo 50,vitunguu kilo 70 na mchele kilo 100 na magunia mengi yanaweza
yakaeleweka kama ni lumbesa ama sio lumbesa na kama magunia yamezidi ujazo huo
maana yake ni lumbesa na wajibu wa serikali ni kusimamia sharia hiyo na
kuwataka wakulima wasiuze kwa uzito ambao unazidi hivyo vipimo.”alisema
Masunya.
Masunya alisema licha ya kutoa sheria hizo kwa wananchi na viongozi wa vijiji kuwataka
wasimamie lakini tatizo linakuja kwa wanunuaji ambao wanawalazimisha wakulima
kuuza kwa bei wanayotaka pamoja na lumbesa na hivyo suluhisho ni taasisi na
wadau wote kushikamana na kuelewa kwenye soko lazima kuzibitiwe ili wanunuzi
wasinunue kwa lumbesa na wao kama halmashauri wanasisimamia kwenye mageti yao
wanapotoza ushuru kabla ya sheria mpya watahakikisha mwenye lumbesa lazima
ashushe apunguze kabla ya kuingiza sokoni.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni