Jumatano, 14 Juni 2017

Shirikisho la soka Tanzania TFF,limetakiwa kusitisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Agosti Dodoma kwa kile ilichodai haij


Jamal Malinzi TFF
Jamal Malinzi Rais wa TFF

Baraza la michezo Tanzania BMT, limelitaka Shirikisho la soka Tanzania TFF, kusitisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Agosti Dodoma kwa kile ilichodai haijataarifiwa.
 Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, ameiambia Sayari ya Habari, mchakato huo usitishwe mara moja na TFF, waanze upya mchakato huo kwa kuliarifu Baraza la michezo kila kinachoendelea.
 “Kwa kuwa wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu, taratibu za uchaguzi wa viongozi zimefafanuliwa kwenye sera ya maendeleo ya Michezo Ibara ya 5:2:2,”imesema taarifa ya Kiganja kwenda kwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa,” amesema Kiganja.
Kiganja amesema kanuni za BMT, zilizotungwa chini ya kifungu cha 28 za mwaka 1999 kifungu namba 4, 6 (e), uwepo wa Kamati ya Nidhamu, Usuluhishi na Rufaa ibara ya 6 (9) (11) na B vinajieleza wazi juu ya majukumu ya Kamati hiyo. 
Amesema kwa kuwa Tanzania inaongozwa kwa sharia na taratibu ilizojiwekea yenyewe, hivyo hakuna chama, klabu wala shirikisho lenye mamlaka ya juu ya BMT yenye nguvu ya kusimamia chaguzi zavyama.
Kwa sababu hiyo, Kiganja amesimamisha zoezi hilo la uchaguzi wa TFF na kuwaita viongozi wa shirikisho hilo chini ya Rais wake, Jamal Malinzi katika kikao maalum kitakachofanyika ofisi za BMT, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Julai 1, mwaka huu kujadili pamoja na kupanga taratibu za uchaguzi huo.
Endapo jambo hilo litaendelea hivyo Tanzania iko hatarini kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kile kinachoonekana Serikali kutaka kuingilia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni