![]() |
| Baadhi ya Majengo ya Hospitali ya Kisasa ya Halmashauri ya wilaya ya Kilolo |
Halmashauri ya
wilaya kilolo imedhamilia kumaliza kero inazowakabili wananchi hususani katika
sekta ya afya kutokana na mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya
itakayowahudumia zaidi ya kata 12 za wilaya hiyo kutokana na kuikosa
huduma hiyo kwa muda mrefu na kulazimika kuitafuta katika hospital ya Rufaa ya
mkoa wa Iringa
Aloyce Kwezi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya wilaya ya Kilolo Aloisi Kwezi na Asiah Abdallah ni mkuu wa wilaya hiyo waliiambia
SAYARI YA HABARI kuwa halmashaurii hiyo
inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya wilaya kwa kushirikliana na
wakala wa Majengo nchini TBA ikiwa ni miongoni mwa miradi itakayo kuwa na Tija
ya moja kwa moja kwa wanachi kutokana na adha waliyoipata ambapo ujenzi huo
unatarajia kukamilika kwa muda wa miezi 8 kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi
ambapo mpaka hivi sasa imesalia miezi miezi 2 kumalizika kwa muda uliotengwa
ili wananchi kuanza kuifurahia halmashauri yao.
Viongozi hao wa Halmashauri ya wilaya kilolo
walisema kutokana na Jografia ya wilaya hiyo changamoto kubwa ni namna wananchi
wanavyoweza kupata huduma za afya hususani wakazi wa vijiji vya Kiwalamo na
Ruaha Mbuyuni ambapo walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kuitafuta
huduma hiyo huku baadhi ya wananchi wakipoteza ndugu zao wakiwa njiani kufuata
huduma za afya ambapo hivi karibuni itabaki historia.
“hapo awali wananchi wa kilolo wamepata shida
sana pale wanapopata maradhi hasa wanawake wajawazito waliokuwa wanahitaji
huduma ya dharura(upasuaji)kwa kuwa katika Halmashauri yetu hatukuwa na
hospitali kubwa walilazimika kwenda Iringa mjini katika hospitali ya Rufaa au
kwenda katika hospitali Teule ya Ilula jambo lililosababisha baadhi ya akina
mama na watoto kupoteza maisha wakiwa njiani tulikuwa hatuna namna”.walisema
viongozi hao
“wanaendelea kusema kwasasa tunao mradi mkubwa
wa ujenzi wa hospitali unaogharimu kiasi cha shilingi billion 4.2 hii itakuwa
hospitali ya mfano kwani tunamajengo matano ya Ghorofa moja moja yanaendelea
kujengwa hisa sasa yanakaribia kuanza shughuli za upauaji na kufikia mwezi wa
nane tunaweza kuwa katika hatua ya umaliziaji na wananchi wataanza kufurahia
upatikanaji wa huduma za afya na itasaidia sana kupunguza foleni katika
hospitali za Rufaa na Hospitali ya Manispaa ya iringa.”walisema
Akizungumzia ushiriki wa wananchi katika
utekelezaji wa miradi hiyo mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya kilolo Valensi
Kihwaga alisema Halmashauri imeendelea na uelimishaji wa wananchi katika
kutambua umuhimu wa miradi iliyopo ili waweze kuisimamia na kiutumia ipasavyo
huku akiwataka waendelee kuonesha ushirikiano kwa serikali katika kutekeleza
miradi hiyo.
“mimi nisema tu Halmashauri yetu imedhamiria
kumaliza kero za wananchi kwa kiasi kikubwa na hasa kwa kuwashirikisha wananchi
wenyewe na tumeendelea kutoa elimu ya kutosha kwao ili wao ndiyo wawe wamiliki
wa miradi ya maendeleo hasa hii Hospitali kubwa ambayo tunaijenga kama serikali
tutahakikisha tunasimamia na kukamilisha kwa wakati ujenzi wake na ianze kutoa
huduma”alisema kihwaga
Halmashauri ya Kilolo kwa ujumla imekusudia
kupunguza kero za huduma za Jamii kwa wananchi ikiwemo miradi ya barabara,Maji
na Elimu ili kufanya wilaya hiyo ikue kiuchumi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni