Jumatano, 24 Septemba 2014



 MH.MGIMWA AWAHAMASISHA VIJANA KUUNDA VIKUNDI ILI WAWEZESHWE.
Mh.Gogfrey Mgimwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga
Vijana nchini wametakiwa kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali vitakavyo warahisishia kupewa dhamana ya mitaji kutoka katika mifuko ya vijana ya serikali.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani hapa Mh.Godfrey Mgimwa wakati wa mahojiano maalumu na Overcomers redio katika kipindi cha tujadili asubuhi kuhusu namna viongozi wanakusudia kuwapa fulsa vijana wote pasipo kuangalia mjini wala vijijini.

Mh.Mgimwa amesema imefika wakati wao kama viongozi vijana kupigania maslahi ya vijana na haki zao za kuwezeshwa kimaisha ili waweze kujikwamua kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo fedha za mifuko ya vijana zitawafikia katika vikundi.

Hivyo amewataka vijana kushirikiana kwa pamoja katika kujiletea maendeleo.

Jumanne, 23 Septemba 2014

KAZI KWENU WAKAZI WA JIMBO LA ISIMANI MWAKA 2015
HUYU NDIYE MPINZANI WA MH.WILLIAM LUKUVI KIJANA WA KIMASAI
Patrick Sosopi akizungumza na wananchi ambaye sasa ni makamu mwenyekiti wa BAVICHA Bara.
  

Jumatatu, 22 Septemba 2014

UZINDUZI WA KIJANA MWIMBAJI NA PRODUCER YUSUFU NGALOWOKA WAFANA IRINGA ZAIDI YA MILION 3 ZAPATIKANA.
 




MAHAMUDU MADENGE ACHANGIA MILIONI MOJA KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YA MWIMBAJI YUSUFU NGALOWOKA.

MNEC MAHAMUDU MADENGE
Akiimba pamoja na waumini wa kanisa hilo
Akipongezwa kwa nasaha nzuri
Pongezei ziliendelea
Akipewa zawadi ya CD moja baada ya kuzindua albamu ya mwimbaji huyo
Baadhi ya waumini waliokuwepo
wengine walikaa upande huu
Hapa akiagwa kwa shamrashamra kubwa
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC-CCM), Mahamudu Madenge amewaambiwa wakristo wenye nia ya kushiriki maandamano yanayoitishwa na wanasiasa kwa nia mbaya kwamba yanawaweka jirani na dhambi.
Hivi karibuni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kilitangaza kuitisha maandamano yasio na ukomo nchini nzima kwa lengo la kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba.
Wakati baadhi ya wanasiasa na wafuasi wa chama hicho wakiyaunga mkono maandamano hayo ambayo hata hivyo yamedhibitiwa na Polisi, wananchi wengi wamenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari wakiyaponda kwa kile walichosema yanalenga kuvuruga amani ya nchi na kuchochea uhalifu.
“Tuache kufuata mikumbo ya siasa, kama tunataka maandamano, tuandamane kuelekea makanisani na kufanya kazi inayompendeza Mungu, tuishi kama alivyoishi Yesu” alisema Madenge anayeshikilia nafasi hiyo nyeti kupitia manispaa ya Iringa.
Aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa albamu ya injili ya muimbaji Yusuph Ngaluoka wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) la mjini Iringa, uliofanyika jana katika ukumbi wa Highlands mjini hapa.
Akiunga mkono kazi inayofanywa na muimbaji huyo, Madenge alitoa mchango wa Sh Milioni moja na kuwataka watanzania wengine kuunga mkono kazi za wasanii wa injili kama wanavyofanya kwa wasanii wengine.
“Wasanii wa injili wanahubiri upendo, amani na utulivu. Na sisi wote tunataka kuishi katika hali ya upendo, amani na utulivu; ni muhimu tukawaogopa wanaotoka kutuingiza kwenye machafuko,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini wa dini hiyo waliojitokeza katika uzinduzi huo.
Alisema kama ilivyoandikwa katika kitabu kitakatifu cha Biblia kwamba wenye moyo safi ndio watakaomuona Mungu ni muhimu wanadamu wakatafakari na kuzipuuza kauli za wanasiasa zinazoweza kuwaondoa katika sifa hiyo.
Wakati akichangia kiasi hicho cha fedha, Madenge aliimba pamoja na waumini hao wimbo maarufu unaotumiwa na wakristo kwenye shughuli mbalimbali wa “Mungu ni Pendo, apenda watu, Mungu ni Pendo anipenda.”
Wakati wimbo huo ukiendelea kuimbwa, Madenge alisema alichagua kufanya kazi ya jamii hivyo haoni sababu ya kuogopa kushirikiana na watu wa makundi mbalimbali pale anapohitajika au kuombwa kufanya hivyo.  
Akishukuru kwa mchango wa Madenge na nasaha zake, muimbaji huyo alimtaja kiongozi huyo kama mmoja wa viongozi wa mfano mwenye moyo wa kusaidia jamii kila anapoombwa kufanya hivyo.
“Mungu akubariki ; nitalia kwa Mungu ili akupe zaidi na zaidi na afanye kitu juu yako utakachokikumbuka katika maisha yako yote,” alisema mbele ya mamia ya waumini wa kanisa hilo waliofurika katika ukumbi huo.

 

ZAIDI YA WASICHANA MILIONI 58 DUNIANI WAMEOLEWA WAKIWA NA UMRI WA CHINI YA MIAKA 18.

SALMA KIKWETE 
 Zaidi ya wasichana milioni 58 Duniani wameolewa wakiwa na  umri wa chini ya  miaka 18  kati ya hao milioni 15 wana umri wa kati ya miaka 10 hadi 14 jambo linalowasababisha kupata maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi na kufanyiwa ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wa Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa wasichana wanajihusisha mapema zaidi katika mapenzi ukilinganisha na watoto wa kiume kwani asilimia 13 ya wasichana wanaanza kufanya mapenzi wakiwa na umri wa chini ya miaka 15 wakati kwa upande wa wavulana ni asilimia saba.
Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akifungua mkutano uliojadili elimu ya afya ya uzazi na jinsia kwa vijana ulioandaliwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani Gerd Mueller na kufanyika katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo uliopo mjini New York nchini Marekani.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kutokana na kitendo cha wasichana kujihusisha na mapenzi wakiwa na umri mdogo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la mimba za utotoni na hivyo wengi wao kushindwa kupata elimu.
“Nchini Tanzania kati ya msichana mmoja hadi wanne wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wana mimba  au watoto , takwimu hizi ni kubwa zaidi katika nchi zingine za kanda ya Afrika ya Mashariki na Kusini”.
Idadi hii inaonyesha wasichana wataendelea kuwa kundi lililoathirika kwa kukosa haki zao za kupata afya, watakabiliana na unyanyasaji na maisha yao yataisha mapema. Tukichukua hatua ya kuwasaidia sasa tutaokoa  wasichana wengi na kuwasaidia kuwa na maisha mazuri hapo baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema vijana wa Afrika wanatakiwa kupewa elimu ya maisha, afya ya uzazi na usawa wa jinsia ambayo itaendana na mila na desturi zao ili waweze kuwa na uchaguzi mzuri wa maisha yao kwani theluthi ya idadi ya watu wanaoishi nchi zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara ni vijana wa kati ya miaka 20 na 24.
Mama Kikwete alisema, “Afrika ya baadaye na ukubwa wa Dunia inategemea na jinsi tutakavyowaandaa vijana kujenga maisha yao ya baadaye. Hii itawezekana kama tutawasaidia kuchagua njia nzuri kuhusu afya yao na kuwaokoa kutoka katika tabia hatarishi”.
Kutimiza hili tunahitaji kuwa na elimu bora ili mambo ya afya ya uzazi na stadi za maisha yapewe kipaumbele na uangalizi mkubwa unatakiwa kwa watoto wa kike”.
Akiwakaribisha wadau wa elimu na afya waliohudhuria mkutano huo Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani Gerd Mueller alisema kwa zaidi ya miaka 20 Serikali yake imekuwa ikifanya kazi ya kuhakikisha vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua na upatikanaji wa huduma ya uzazi wa mpango inaimarika.
“Jambo la ziada linatakiwa kufanyika hasa katika Bara la Afrika lenye matumaini tutaongeza ushirikiano tukilenga zaidi katika elimu hasa elimu ya ufundi kwa wasichana na wavulana”.
Tunahitaji kufanya jambo la ziada kama tunataka kufanikiwa katika afya na elimu kwa vijana hasa wasichana. Wasichana wengi wenye umri wa chini ya miaka 18 katika nchi zinazoendelea wanapata mimba zinazowaletea matatizo yanayopelekea vifo vyao”, alisema Mueller.
Alisema Serikali ya Ujerumani itatoa fedha zingine Euro milioni 3 kwa ajili ya na kuandaa programu za pamoja ambazo zitaongeza elimu ya afya ya  ujinsia na huduma za afya ya uzazi kwa vijana katika nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kusini.
Akichangia mada katika mkutano huo Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupamba na Ukimwi (UNAIDS)  Prof. Sheila Tlou alisema vijana wanahitaji kupata elimu ya afya ya uzazi na jinsia ili waweze kujikinga na ndoa za utotoni na Ugonjwa wa Ukimwi.
 Takwimu zinaonyesha kwa kila saa moja kuna maambukizi mapya 50 ya HIV kwa vijana hii ina maana kuwa kwa mwaka kuna maambukizi mapya 430000. Kwa sasa kuna vijana milioni 2.6 wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU).
 Prof. Tlou alisema mwaka mmoja umepita tangu  Mawaziri wa Afya na Elimu kutoka nchi 21 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakubaliane maazimio ya kuongoza juhudi za kuandaa mazingira salama na wezeshi kwa makuzi ya vijana katika nchi zao.
“Ni muhimu kuyafanyia kazi maazimio hayo ambayo yatawasaidia  vijana kupata elimu kuhusiana na afya ya uzazi na jinsia jambo ambalo litawasaidia  kufahamu zaidi  ugonjwa Ukimwi”, alisema Prof. Tlou.
 Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Mke wa Rais wa Malawi Gertrude Mutharika ni moja ya maandalizi ya Mkutano wa  69 wa Umoja wa Mataifa (UN) utaofanyika hivi karibuni mjini humo.

Jumamosi, 20 Septemba 2014



KABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA
KUNA wakati maisha yako yanaporomoka kutokana na kupatwa na misukosuko ya maisha kama vile kufiwa na mke, mume au mtoto wako, kusalitiwa na marafiki uliowategemea maishani mwako, kukimbiwa na mke au mume wako, kufilisika, kupoteza kazi uliyokuwa ukiitegemea, au daktari kukuambia kuwa ugonjwa unaokusumbua si rahisi kupona.

Hali hiyo inapokutokea, unajikuta unakata tamaa ya maisha na kujiona kuwa hustahili kuishi katika dunia hii inayokuzunguka, lakini kumbuka hiyo ni njia ya kupitia katika maisha haya tunayoishi.
Hivyo ni vizuri kumtafuta rafiki yako wa karibu au kiongozi wako wa dini kwa msaada zaidi. Kwani viongozi wa dini mara nyingi wamekuwa washauri wazuri katika maisha yetu ya kila siku.
Pia ukubaliane na hali ile ambayo huwezi kuibadilisha katika maisha yako. Na kukataa kuendekeza nafsi yako katika hali ya kujisikitikia kwani hali ya kujihurumia ni ugonjwa, kama vile acid.
Hali hiyo itakuondolea hadhi yako, itakuongezea sononeko na kukata tamaa. Itakuharibia uhusiano wako na wengine. Itakusababishia hali ya kuwa na chuki. Hakuna jambo zuri litakalokujia katika maisha yako kutokana na hali hiyo ya kujisikitikia.

Usichukue maumivu yako kwa wengine. Unaporuhusu maumivu huumizi watu wengine bali unajiumiza wewe mwenyewe. Iambie nafsi yako kuwa unahusika na vitendo au tabia zako mwenyewe. Hakuna atakayeiumiza nafsi yako ila wewe mwenyewe.
Usifanye ukaidi. Kubaliana na ukweli. Si wakati wote maisha yanakuwa sawa na ya kuridhisha. Haijalishi hali inayokutokea katika maisha yako, hali ya kukata tamaa, ndoto zako hazikutimia bado kuna tumaini katika maisha yako.

Baada ya usiku inakuja siku mpya, baada ya kipindi cha baridi huja kipupwe, baada ya mvua kubwa huja jua, baada ya dhambi huja msamaha, baada ya maangamizo nafasi nyingine hutokea.
Tuangalie mfano wa kijana mmoja wa miaka 15 ambaye alidondoka kutoka juu ya mti na kuvunjika mgongo. Kwa bahati aliokolewa akiwa mzima, lakini tokea kipindi hicho hakuweza kutembea tena. Alitembelea kiti cha watu wenye ulemavu, katika maisha yake yote.
Katika kipindi kigumu kama hiki, inakuwa ni rahisi kujihurumia na kujiona huna thamani tena katika maisha yako. Lakini haikuwa hivyo wa kijana huyu ambaye alivunjika mgongo.

Kwani hakujiweka katika hali ya unyonge. Alitaka kuondoa hali aliyonayo na kuwa mtu mashuhuri. Kitu cha kwanza alicholenga kukifanya ni kumaliza masomo yake ya kidato cha sita. Alichohitaji ni kupata alama nzuri ili kufikia matarajio yake. Alimwambia mama yake anataka kuchukua masomo ya sanaa na uchoraji.
Kijana huyo ndoto yake ya maisha bora ilianza kung’aa tokea hapo na kufanikiwa katika maisha yake kutokana na kazi yake nzuri aliyoifanya. Kwani alikuwa mchoraji mzuri kiasi kwamba aliweza kupata mialiko mbalimbali kwenye vyuo vikuu vingine kutokana na bidii yake aliyoionyesha kwenye michoro aliyoichora. Baada ya masomo yake, kijana huyo alipata barua ambayo ilimtaka kwenda kufanya kazi ya kuchora katika kiwanda cha nguo.
Kazi hiyo imempatia pesa nzuri na kuweza kuisaidia familia yake. Kazi yake imempatia mahitaji yake yote ambayo alifikiri anahitaji. Anayapenda maisha katika hali ile aliyonayo. Kijana huyo ni mmoja wa watu wenye matarajio makubwa ukiachilia mbali hali aliyonayo ya kuwa mtu maarufu.

Kamwe usiishi maisha ya kushindwa. Unaona njia katika hali ya ugumu unayokabiliana nayo. Siri ya ushindi ni hii, usijione mshindwa, usikubali kushindwa kamwe usiishi katika hali ya kushindwa. Iambie akili yako kuwa hukuumbwa ili uwe mtu wa kushindwa.

Huwezi kuwa mtu wa kushindwa kama hujaruhusu hali hiyo katika maisha yako. Watu siku ya leo wanakata tamaa kutokana na sababu mbalimbali za maisha. Katika mtiririko wa mambo hayo, hakuna haja ya kukata tamaa katika maisha. Mtu ambaye hana kitu kinachofanya ajishughulishe anaona kuwa hana haja ya kuishi. Kila mtu anahitaji kitu cha kushikilia fikra zake na kumpa changamoto ili kufikia malengo anayotarajia.

Kumbuka, hakuna mafanikio pasipo kutaabika. Njia ya mapambano ni njia ambayo inamwezesha mtu binafsi kuongezeka, kukua, kuwa na maendeleo. Kila mtu anapitia maisha magumu kwa jinsi yake. Ni jinsi gani utakabiliana na hali hiyo ili uweze kuondokana nayo? Ni kwa kukataa hali hiyo na kusonga mbele.

Fanya jambo fulani kubwa ambalo hujawahi kulifanya kabla ya hapo. Unaweza kufanya mambo makubwa ambayo hukuwahi kuyafanya kabla ya hapo. Hiyo ni kwa sababu maumivu yako yamegeuka kuwa nyota ya mafanikio, tumia fikra zako, panua akili yako, jenga na tarajia. Uje na wazo kubwa, jambo fulani kubwa kuliko ilivyo kawaida yako. Songa mbele usikate tamaa mpaka pale matarajio yako yatakapotimia.

Jumapili, 14 Septemba 2014

TUMIA KINYWA CHAKO KUFANYA MABADILIKO YA MAISHA KIROHO

KUNA NGUVU YA MUNGU KATIKA KINYWA CHAKO ITUMIE ITAKUSAIDIA

 “Nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU, (Matendo 1: 8).
Je, tunatumia hii nguvu ya MUNGU?
Na je tunaitumia  mamlaka ya KRISTO tuliyopewa kama inavyotakiwa?
Haijalishi mwana wa MUNGU unapita katika magumu kiasi gani, Unachotakiwa ni kubadilisha kukiri kwako, na kadri unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana,elewa kuna jambo katika ulimwengu wa Roho linafanyika, hata kama huna shilingi mia mfukoni wewe sema pesa zipo,  hata kama wewe ni mgonjwa umelala kitandani Sema mimi ni mzima, maana Neno la MUNGU  linasema aliye dhaifu na aseme ana nguvu.
 Ezekieli alipoonyeshwa lile bonde la mifupa mikavu, kwa macho  ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi.
Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa unabii na kuitabiria ile mifupa, akaiambia  ’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi.’’  Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni jinsi gani Ezekiel ialivyoweza kutumia nguvu na uweza ulioko ndani ya kinywa chake na kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana wa MUNGU nini ni kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako?
-Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena,
-au ni uchumi wako,
- afya yako,
-watoto wako,
-hudumayako,
MUNGU anakuambia leo simama na uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.


Unakiri nini kushindwa au kushinda?
Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote yanayoonekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO mwenye nguvu zote.