Jumapili, 2 Julai 2017

TANZANI 1-AFRICA KUSINI 0 KIPINDI CHA KWANZA KATIKA MICHUANO YA COSAFA



Nahodha wa Taifa Stars Himid Mao amesema kufikia hatua ya robo fainali michuano ya Baraza la Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) kumewapa imani kubwa dhidi ya safari yao kuelekea mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Mao ameiambia Sayari ya Habari,  kama wataendeleza morali walionayo sasa wanaweza kufika mbali ikiwemo kuwatoa wenyeji Afrika Kusini leo.

Amesema kikubwa ni wachezaji kuendelea kujituma na kuisaidia timu kufikia malengo yake.

“Tunashukuru Mungu kwa kufikia hatua muhimu kama hii ya robo fainali, nategemea tukiendeleza juhudi tutafika mahali pazuri kuelekea safari yetu ya kutafuta nafasi ya kufuzu CHAN na ikiwezekana Afcon,”amesema.

Mao amesema kikubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri mchezo wa leo dhidi ya Afrika Kusini na kutoa picha kamili.

Amesema Afrika Kusini ni timu iliyoendelea na itawapa changamoto na kutoa tathmini juu ya safari yao ya Chan na Afcon.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni