Timu ya Soka ya Tanzania Taifa Stars imeibuka
na ushindi wa goli 1-0 thidi ya Afrika Kusini katika michuano ya Balaza la Soka
katika nchi za kusini Mwa Africa COSAFA ambapo katika dk 18 mchezaji wa Timu ya
Taifa ya Tanzania Elius Mguli jezi nambali 12 mgongoni aliwainua mashabiki kwa
kupachika Bao la kwanza na la Ushindi.
Taifa Stars ilifuzu kuingia katika hatua ya
robo fainali ya mashindano ya michuano ya COSAFA inayo endelea huko nchini
Afrika Kusini baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Mauritius.
Huko Afrika kusini Timu yua Tanzania ikicheza
na Wenyeji wa Mashindano hayo Afrika Kusini imekuwa ilicheza mchezo wa kuvutia
kuonesha ukomavu wa soka huku timu ya wenyeji wakidharu mchezo huo ambapo
imewagharimu na sasa watabaki kuwa watazamaji wa wa Mashindano hayo baada ya
kutolewa kwa Goli moja kwa sufuli.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Mcheza Mhimu
katika mchezo huo(MAN OF THE MARCH)Elius Maguli amesema walipata nafasi na
wameitumia na kupata goal lililowapeleka kwenye Nusu Fainali
“tunashukuru tumetumia nafasi tuliyoipata
tumeshinda cha msingi ni kujiandaa katika michezo mingine”alisema mchezaji huyo
Katika michuano hiyo Taifa Stars imekuwa
ikionesha tofauti na Timu zingine kwani Hadi leo imepata nafasi ya kutoa Man Of
The March kwa mara ya Nne mfurulizo
Sayari ya Habari inaitakia Taifa Stars
Ushindi katika mechi zijazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni