Wakizungumza katika uzinduzi wa
Tamasha linalojulikana kwa Jina la JPM Starsuch lililoandaliwa na Umoja wa
Vijana wa CCM UVCCM Manispaa ya Iringa na kufanyika katika ukumbi wa Hall Fear
mkoani hapa kwa lengo la kibua vipaji mbalimbali kwa vijana walisema
kumekuwa na ugumu kwa wasanii wa kubwa kuonesha ushirikiano kwa wasanii
wachangajambo linalosababisha linayosababisha kushindwa kuwepo kwa ushindani
katika tasnia ya film na muziki na kuleta Tija kwa Taifa.
De Money ni miongoni mwa wasani
chipkizi wa Sanaa ya Muziki wa Bongo Freva aliiambia SAYARI YA HABARI kuwa
richa ya vijanawasanii kujiytuma lakini bado wanahitaji Sapoti kutoka kwa
wasanii wakubwa jambo ambalo lipo tofauti kwani baadhi ya wasnii wakubwa
wamekuwa wakihitaji fedha nyingi ili kufanya nao Korabo(kushirikisha)katika
nyimbo kwa kisisngizio kwamba wanawabeba
“tunatamani sana kufika mbali
kwasababu kama masinii unapofanyakazi unakuwa na maono ya wapi unataka kufika
lakini pia kama msanii unajaribu kuwatafuta wasanii waliotangulia angalau
wanamajina lakini changamoto kubwa hawaoneshi ushirikiano wa moja kwa moja
gharama inakuwa kubwa ukitaka umshirikishe katika nyimbo yako natamani
tusaidiane tuitangaze sanaa yetu ya Muziki”alisema De Msanii huyo
Merina Mlowe pia ni miongoni mwa
waigizaji walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha Hilo ambapo alisema kama wasanii
wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa fedha kama mitaji kwaajili ya kufanyia kazi
zao jambo linalokwamisha jitahada wanazozifanya katika kutengeneza Tamthilia
zenye Ubora hivyo aliiomba serikali iwasaidie waweze kupata mitaji ili
iwasaidie kuandaa kazi bora.
“kwa kweli tunatamani sana kufanya
kazi kwa kiwango kikubwa lakini tunashindwa kutokana na uhaba wa fedha ila
tunawapongeza UVCCM kwa kuona waanze kuuanda mikakati ya kuibua vipaji na
kuikumbusha serikali wajibu wake katika kutuwezesha vijana tuweze kujiari”alisema
Merina
Kwa upande wake rais wa
shirikisho la film Tanzania Simon Mwakifamba alisema wasanii wakubwa ili
kuiinua sanaa Tanzania ni lazima wasanii wakubwa watumie nafasi zao kuwainua
wasanii chipkizi kwani ili sanaa iwe na Tija kwa Taifa ni lazima watu
wengi wawekeze katika shughuli hiyo badala ya kuwakatisha tama na kushindwa
kufanya kazi pamoja na wasanii hao wachanga.
“hii ni kiongoni mwa changamoto
ambazo zipo pengine mi mi nisema ni vema sasa wasanii wakubwa wanajitambua tena
kwa majina ifike wakati tuwaone wasanii wadogo ni sehemu yetu hawa wakikua
watatusadai lakini pia niwatie shime hilo lisiwakatishe tamaa kuweni wabunifu
fanyeni kazi”alisema
Alphonce Myinga ni Katibu wa UVCCM
Manispaa ya Iringa alisema Mashindano hayo richa ya kuibua vipaji lakini
pia yalilenga kuwakutanisha vijana pamoja ili kuoneshana wapi zinapopatikana
Fursa ili vijana waweze kuwa na mambo ya kufanya badala ya kubaki wakilalamika
kuwa hakuna ajira ipo haja kwa vijana kuanzisha miradi yao ikiwa nai pamoja na
kujiingiza kwenye sanaa ili waweze kuonesha vipaji vyao na kuitangaza nchi.
“kanuni za umoja wa vijana
zinaniongoza mimi hasa nikiwa natekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini
nimeandaa tamasha hili ili kuhakikisha tunawaunganisha vijana ili waepukane na
matendo mabaya wawe na jambo la kufanya kwa sababu sanaa ni ajira wajibu wangu
ni kuwa linda vijana ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.”alisema katibu
UVCCM
Naye mkuu wa wilaya ya iringa Richard
kasesela alisema ipo changamoto kwa baadhi ya wasanii ambao hutumia nafasi zao kwa
kudharau wengine na kuona wamefanikiwa jambo linalorudisha Nyuma maendeleo
hivyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza baadhi ya wasanii wenye nia ya kuwainua
vijana wenzao ambapo kwa kwakufanya hivyo kunawafanya na wao kufanikiwa zaidi.
“niwakumbushe wasanii nchini upo
ukomo wa kuwa msanii hebu tumieni nafasi zenu kuwainua wasanii wenzenu kwani
njia hiyo ndiyo hutumiwa na nchi zilizoendelea wale waliofanikiwa wanatumia
nafasi zao kuwasadia waliochini ili kuweka Chain ya Wasanii mmoja anaposhindwa Yule
aliyeibuliwa anaendeleza pale pongezi nyingi kwa Diamond kwa kusaidia vijana
wenzake.”alisema kasesela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni