Michuano
ya kombe la Mabara imemalizika na Hatimaye
Timu ya Soka ya Taifa ya Ujerumani imeibuka Bingwa mara baada ya kumtandika bao
Moja kwa Sufuli timu ya Taifa ya Chile ambaye katika mchezo wao uliopita Chile
vs Ujerumani walitoka sare ya bao moja kwa moja uliochezwa kwenye uwanja wa Kazan Arena
huko Kazan, Urusi.
Jumapili
usiku, Julai 2, kumefanyika mtanange wa mechi moja ya fainali, ambapo timu ya
taifa ya Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia lililopita nchini Brazil ambapo kwa sasa chini ya Mwalimu Joachim Löw ambaye amekiandaa kikosi cha
Ujerumani na kurudisha heshimaya Soka nchini Ujerumani.
Ujerumani
iliingia uwanjani kwenye mchezo huo, ikiwa na historia nzuri ya kuanza vyema
michuano ya mwaka huu mpaka kwenye hatua waliyofikia baada ya kutopoteza mchezo
hata mmoja.
Ujerumani imetengeneza
Historia ya kuwa timu nyingine itakayofanikiwa kutwaa taji la michuano ya Ulaya
baada ya lile la kombe la dunia kama ilivyowahi kufanya timu ya taifa ya
Hispania, iliyotwaa kombe la dunia mwaka 2010 na kushinda taji la Ulaya mwaka
2012.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni