HAWA NI VIJANA WATANZANIA WANAOLIA KILA SIKU KUDAI HAKI ZAO ZINAZOTUMIWA NA WAWEKEZAJI WANAOPEWA MAENEO KUWASAIDIA VIJANA FIKIRI KAMA UNGEKUWA WEWE.
Ikiwa wakazi wa Mtwara na Lindi wanalia na Bomba la Gesi linalo tolewa mkoani hapo na kwenda jijini Dar es salam na wameshindwa Iringa nako mwekezaji awanyanyasa wafanyakazi tazama Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Johnson Internation Group ambao wamefanya maandamano ya amani kudai haki zao kutoka kwa mwajili wao ambaye wamedai kuwa amekuwa akiwazungusha katika kuwalipa mishara yao.Wakizungumza na Mtandao huu vijana hao wamesema ni zaidi ya miezi minne wamesimamishwa kazi na mwajili wao kwa madai kuwa kazi za kufanya zimekwisha hivyo wanatakiwa kupumzika na pindi itakapo patikana kazi wataitwa kuifanya huku wakisubiri malipo yao,wamesema wamekuwa wavumilivu kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kupewa barua zao za kupumzishwa kazi huku wakiambiwa watapewa lakini haikuwa hivyo.
Wamesema kuwa wamekaa kwa zaidi ya miezi minne bila kuambiwa chochote kuhusu malipo yao huku wakipewa ahadi zisizokuwa na utekerezaji wowote,pamoja na vijana hao kutaabika na ugumu wa maisha unao wakabili kwa kuwa wametoka mikoa mbalimbali wameamua kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kupeleka kilio chao ili waweze kusaidiwa.
swali waliloliuliza nikwamba je,wawekezaji wapo ili watunyanyase wafanyakazi wa hali ya chini?



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni