KIJANA AMKA UKAWAJIBIKE
Elani : Kundi la vijana kutoka nchini Kenya linalotumia vizuri lugha ya kiswahili
Tukiongelea Elani kama kundi la vijana linalohit nchini Kenya tutaweza kulifananisha na kundi la Shosteez ambalo linaudwa na three fresh young talented girls japo tofauti na Shosteez , Elani ni kundi lililosimama na ambalo bado lipo hai katika kuwapa burudani wapenzi wake hasa ukizingatia wanaimba nyimbo zao kwa lugha ya kiswahili kwa sana. Nyimbo yao ya kwanza inaitwa “Jana Usiku”.
Wambui Ngugi, Maureen Kunga and Bryan Chweya ni marafiki wa muda mrefu waliokutana kwa mara ya kwanza huko Alliance Française nchini Kenya mwaka 2008 na kuamua kuanzisha kundi la Elani kutokana na kua wote ni wapenzi wa muziki.Tokea waanze kuimba Elani wameweza kupata show za kutosha jijini Nairobi na nje yake na waliachia album yao ya kwanza inayoitwa “Barua ya Dunia” tarehe 6 December mwaka jana..
Maana halisi ya “Elani” ni Mwanga huku neno hili likiwa ni neno la ki-giriama. Hivi sasa Elani wanajiandaa kuachia video yao ya tatu..

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni