Jumanne, 2 Septemba 2014

KALAMU YAKO IFICHUE MAOVU.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFUATA MAADLI YA UANDISHI ILI KUISAIDIA JAMII YA WASIYO WASEMEMAJI.


Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari mkoani Iringa(IPC) Bw Frank Leonard wakati akizungumza na wandishi katika siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho na mwandishi wa habari wa kituo cha Televition cha Cha Chanel Ten Daudi Mwangosi kilichotoke 2/9/2012 katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa ambapo hapo jana imetimia miaka miwili tangu kufariki kwake.

Mwenyekiti huyo amesema kifo cha Mwangosi nipengo katika tasnia ya habari hivyo amesema ni vema kufuata yale mema aliyoyaacha ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii ili kumuenzi kwake kuwe na tija,Amesema Chama cha wandishi wa habari mkoani Iringa kimeona ni vema kuweka jambo la kumuenzi mwandishi huyo ikiwemo michezo.

Aidha amewataka wandishi kufanya kazi ya kuandika habari zitakazoleta mabadiliko na kuwa wasemaji wa watu wasio na mahali pakusema badala ya kuwasemea wenye uwezo ameenda mbali zaidi na kutaja makundi ya watu hao kuwa na pamoja na wale wanaohitaji pembejeo,barabara,Afya na wanakosa huduma hizo,pia ni wale wanaohitaji maji hawayapati,wanahitaji umeme hawapati,na ni wale wanaohitaji kusomesha watoto lakini inashindikana,

Hivyo amesema wandishi ndiyo kioo cha mwananchi wa hali ya chini katika kumuinua ajue mambo yaliyojificha na hivyo ndivyo tutamuenzi Daudi Mwangosi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni