MBUNGE KIJANA JIMBO LA KALENGA GODFREY MGIMWA AWAFURAHISHA WANACHAMA WA VICOBA KATA YA KIWERE WAMPONGEZA KWA KUWAONGEZEA NGUVU
| Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kushoto akipongezwa na mmoja kati ya wapiga kura wa kijiji cha Kiwere |
| Mfanyabiashara wa nyama choma Kiwere kulia akimweleza mbunge Mgimwa jambo baada ya kutembelea vijana na wananchi wanaojishughulisha na biashara eneo la magenge ya Kiwere |
| Wanakikundi cha uoteshaji miti Kiwere wakimweleza mikakati yao mbunge Mgimwa katikati |
| Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akipita kwa shida katika vichaka baada ya kwenda kuwatembelea wapiga kura wake kijiji cha Kiwere |
| Kama anazungumza vile “lazima nimefike kuona kazi za wapiga kura wangu “ |
| Mbunge wa Kalenga Bw Mgimwa katikati akiruka maji ili kwenda kuona mto ambao unatumika kuwapa huduma ya maji wakazi wa Kiwere |
| Wanachama wa VICOBA Kiwere wakiimba shairi mbele ya mbunge Mgimwa |
| Diwani wa kata ya Kiwere Pachal Mwano akizungumza kabla ya kumpongeza mbunge Mgimwa kwa kazi nzuri |
| Mbunge Mgimwa akizungumza na wanachama wa Vicoba Kiwere |
Wanachama wa Vicoba Kiwere wakifuatilia hotuba ya mbunge Mgimwa
Na Matukiodaima.co.tz
WANACHAMA
wa vikundi vya VICOBA kata ya Kiwele katika jimbo la Kalenga
mkoani Iringa wapongeza jitihada za mbunge wao Godfrey Mgimwa kwa
kuwachangia kiasi cha Tsh milioni 3 ili kukuza mfuko wa vikundi
hivyo kata ya Kiwele.
Akitoa
pongezi hizo jana kwa niaba ya wanachama wa VICOBA kata ya
Kiwele diwani wa kata hiyo Paschal Mwano alisema kuwa kata hiyo
ni miongoni mwa kata zenye ndoto kubwa ya kuanzisha benki ya
wananchi wa kata ya Kiwele hivyo kutokana na jitihada mbali mbali
mbali zinazofanywa na wananchi hao kwa kuungana katika vikundi hivyo
ipo siku watafikia hatua ya kuwa na benki
Kwani
alisema kuwa fedha hizo kiasi cha Tsh milioni 3 zilizotolewa na
mbunge huyo zitasaidia kukuza mtaji wa vikundi hivyo 22
zilivyopo katika kata hiyo yenye vijiji vitano kikiwemo cha Kiwere ,
Mgera, Mfyome ,kitapilimwa na Itagutwa .
Alisema
kuwa vikundi hivyo hivyo vina jumla ya wanachama 464 wakiwemo
wanawake 386 na wanaume 78 na hadi sasa wana jumla ya Tsh 33835000
na kuwa kutokana na na faida mbali mbali wanazozipata katika
vikundi hivyo wanachama wameweza kuanzisha miradi mbali mbali
ikiwemo ya ufugaji kuku ,bata nyuki na miradi mingine mingi ambayo
imewasaidia kukuza uchumi wa mwanachama mmoja mmoja.
Mbali
ya kujiwezesha kwa mikopo bado wanahitaji kusaidiwa mitaji zaidi
ili kuanzisha miradi ya ufugaji ng’ombe wa maziwa na kuku wa nyama na
mayai kama njia ya kuongeza miradi zaidi.
Kwa
upande wake mbunge Mgimwa pamoja na kuwapongeza kwa kuanzisha
vikundi hivyo 22 vya vicoba bado alisema kuwa kasi kubwa ya
wananchi kuendelea kujiunga na vikundi hivyo vya Vicoba ndio
itakayopelekea jimbo la Kalenga kuja kuwa na benki ya wananchi wa
Kalenga jambo ambalo linawezekana.
”
Nawapongeza sana wananchi wa kata ya Kiwere kwa kuendelea
kujiunga na Vicoba kwani naamini njia pekee ya kujikomboa kiuchumi ni
pamoja na hii ya kujiunga pamoja ……kwa hatua ambayo mmefikia
tunaweza kufanya jambo kubwa zaidi ya hili mimi leo nitawachangia
kiasi cha Tsh milioni 3 ili kukuza mtaji zaidi ” alisema mbunge
Mgimwa
Aidha
alisema kuwa tatizo kubwa katika vikundi hivyo vya kifedha ni
pale ambapo wanachama wanakopa na kushindwa kurejesha mikopo kwa
wakati na hivyo kukwamisha wanachama wengine kukopa .
Kuwa
iwapo wanachama watashindwa kurejesha mikopo kikundi ama vikundi
hivyo havitaendelea na badala yake vitakufa mapema hivyo kuwataka
wakopaji kulipa mikopo kwa wakati kama njia ya kuviendeleza vikundi
hivyo.
Mbunge
Mgimwa alisema kuwa kitaalum yenye ni mtaalam wa fedha hivyo
kwa kupitia uwezo wake ndio sababu ya bunge kumteua kuwa mjumbe
wa kamati ya bunge ya bajeti ya serikali na wana kalenga wazidi
kujivunia kumpata mbunge mwenye ndoto ya kuona jimbo hilo
linakuwa na benki ya wananchi wa Kalenga jambo ambalo linawezekana
kufanyika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni