MAHAMUDU MADENGE ACHANGIA MILIONI MOJA KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YA MWIMBAJI YUSUFU NGALOWOKA.
| MNEC MAHAMUDU MADENGE |
| Akiimba pamoja na waumini wa kanisa hilo |
| Akipongezwa kwa nasaha nzuri |
| Pongezei ziliendelea |
| Akipewa zawadi ya CD moja baada ya kuzindua albamu ya mwimbaji huyo |
| Baadhi ya waumini waliokuwepo |
| wengine walikaa upande huu |
| Hapa akiagwa kwa shamrashamra kubwa |
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi (NEC-CCM), Mahamudu Madenge amewaambiwa wakristo wenye nia ya
kushiriki maandamano yanayoitishwa na wanasiasa kwa nia mbaya kwamba yanawaweka
jirani na dhambi.
Hivi karibuni Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kilitangaza kuitisha
maandamano yasio na ukomo nchini nzima kwa lengo la kushinikiza kusitishwa kwa
Bunge la Katiba.
Wakati baadhi ya wanasiasa na wafuasi wa
chama hicho wakiyaunga mkono maandamano hayo ambayo hata hivyo yamedhibitiwa na
Polisi, wananchi wengi wamenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari wakiyaponda
kwa kile walichosema yanalenga kuvuruga amani ya nchi na kuchochea uhalifu.
“Tuache kufuata mikumbo ya siasa, kama
tunataka maandamano, tuandamane kuelekea makanisani na kufanya kazi inayompendeza
Mungu, tuishi kama alivyoishi Yesu” alisema Madenge anayeshikilia nafasi hiyo
nyeti kupitia manispaa ya Iringa.
Aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa albamu
ya injili ya muimbaji Yusuph Ngaluoka wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)
la mjini Iringa, uliofanyika jana katika ukumbi wa Highlands mjini hapa.
Akiunga mkono kazi inayofanywa na
muimbaji huyo, Madenge alitoa mchango wa Sh Milioni moja na kuwataka watanzania
wengine kuunga mkono kazi za wasanii wa injili kama wanavyofanya kwa wasanii
wengine.
“Wasanii wa injili wanahubiri upendo,
amani na utulivu. Na sisi wote tunataka kuishi katika hali ya upendo, amani na
utulivu; ni muhimu tukawaogopa wanaotoka kutuingiza kwenye machafuko,” alisema
huku akishangiliwa na mamia ya waumini wa dini hiyo waliojitokeza katika
uzinduzi huo.
Alisema kama ilivyoandikwa katika kitabu
kitakatifu cha Biblia kwamba wenye moyo safi ndio watakaomuona Mungu ni muhimu
wanadamu wakatafakari na kuzipuuza kauli za wanasiasa zinazoweza kuwaondoa
katika sifa hiyo.
Wakati akichangia kiasi hicho cha fedha,
Madenge aliimba pamoja na waumini hao wimbo maarufu unaotumiwa na wakristo
kwenye shughuli mbalimbali wa “Mungu ni Pendo, apenda watu, Mungu ni Pendo
anipenda.”
Wakati wimbo huo ukiendelea kuimbwa,
Madenge alisema alichagua kufanya kazi ya jamii hivyo haoni sababu ya kuogopa
kushirikiana na watu wa makundi mbalimbali pale anapohitajika au kuombwa
kufanya hivyo.
Akishukuru kwa mchango wa Madenge na
nasaha zake, muimbaji huyo alimtaja kiongozi huyo kama mmoja wa viongozi wa
mfano mwenye moyo wa kusaidia jamii kila anapoombwa kufanya hivyo.
“Mungu akubariki ; nitalia kwa Mungu ili
akupe zaidi na zaidi na afanye kitu juu yako utakachokikumbuka katika maisha
yako yote,” alisema mbele ya mamia ya waumini wa kanisa hilo waliofurika katika
ukumbi huo.
ZAIDI YA WASICHANA MILIONI 58 DUNIANI WAMEOLEWA WAKIWA NA UMRI WA CHINI YA MIAKA 18.
Zaidi ya wasichana
milioni 58 Duniani wameolewa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 kati
ya hao milioni 15 wana umri wa kati ya miaka 10 hadi 14 jambo
linalowasababisha kupata maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi na kufanyiwa
ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wa Tanzania takwimu
zinaonyesha kuwa wasichana wanajihusisha mapema zaidi katika mapenzi
ukilinganisha na watoto wa kiume kwani asilimia 13 ya wasichana wanaanza
kufanya mapenzi wakiwa na umri wa chini ya miaka 15 wakati kwa upande
wa wavulana ni asilimia saba.
Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akifungua mkutano
uliojadili elimu ya afya ya uzazi na jinsia kwa vijana ulioandaliwa na
Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani Gerd Mueller
na kufanyika katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo uliopo mjini New York
nchini Marekani.
Mama Kikwete ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kutokana
na kitendo cha wasichana kujihusisha na mapenzi wakiwa na umri mdogo
wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la mimba za utotoni na hivyo wengi wao
kushindwa kupata elimu.
“Nchini Tanzania kati ya msichana
mmoja hadi wanne wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wana mimba au
watoto , takwimu hizi ni kubwa zaidi katika nchi zingine za kanda ya
Afrika ya Mashariki na Kusini”.
Idadi hii inaonyesha wasichana
wataendelea kuwa kundi lililoathirika kwa kukosa haki zao za kupata
afya, watakabiliana na unyanyasaji na maisha yao yataisha mapema.
Tukichukua hatua ya kuwasaidia sasa tutaokoa wasichana wengi na
kuwasaidia kuwa na maisha mazuri hapo baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema
vijana wa Afrika wanatakiwa kupewa elimu ya maisha, afya ya uzazi na
usawa wa jinsia ambayo itaendana na mila na desturi zao ili waweze kuwa
na uchaguzi mzuri wa maisha yao kwani theluthi ya idadi ya watu
wanaoishi nchi zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara ni vijana wa kati ya
miaka 20 na 24.
Mama Kikwete alisema, “Afrika ya
baadaye na ukubwa wa Dunia inategemea na jinsi tutakavyowaandaa vijana
kujenga maisha yao ya baadaye. Hii itawezekana kama tutawasaidia
kuchagua njia nzuri kuhusu afya yao na kuwaokoa kutoka katika tabia
hatarishi”.
Kutimiza hili tunahitaji kuwa na
elimu bora ili mambo ya afya ya uzazi na stadi za maisha yapewe
kipaumbele na uangalizi mkubwa unatakiwa kwa watoto wa kike”.
Akiwakaribisha wadau wa elimu na
afya waliohudhuria mkutano huo Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo wa Ujerumani Gerd Mueller alisema kwa zaidi ya miaka 20
Serikali yake imekuwa ikifanya kazi ya kuhakikisha vifo vya kina mama
wajawazito na watoto vinapungua na upatikanaji wa huduma ya uzazi wa
mpango inaimarika.
“Jambo la ziada linatakiwa
kufanyika hasa katika Bara la Afrika lenye matumaini tutaongeza
ushirikiano tukilenga zaidi katika elimu hasa elimu ya ufundi kwa
wasichana na wavulana”.
Tunahitaji kufanya jambo la ziada
kama tunataka kufanikiwa katika afya na elimu kwa vijana hasa wasichana.
Wasichana wengi wenye umri wa chini ya miaka 18 katika nchi
zinazoendelea wanapata mimba zinazowaletea matatizo yanayopelekea vifo
vyao”, alisema Mueller.
Alisema Serikali ya Ujerumani
itatoa fedha zingine Euro milioni 3 kwa ajili ya na kuandaa programu za
pamoja ambazo zitaongeza elimu ya afya ya ujinsia na huduma za afya ya
uzazi kwa vijana katika nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kusini.
Akichangia mada katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kupamba na Ukimwi (UNAIDS) Prof. Sheila Tlou
alisema vijana wanahitaji kupata elimu ya afya ya uzazi na jinsia ili
waweze kujikinga na ndoa za utotoni na Ugonjwa wa Ukimwi.
Takwimu zinaonyesha kwa kila saa
moja kuna maambukizi mapya 50 ya HIV kwa vijana hii ina maana kuwa kwa
mwaka kuna maambukizi mapya 430000. Kwa sasa kuna vijana milioni 2.6
wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Prof. Tlou alisema mwaka mmoja
umepita tangu Mawaziri wa Afya na Elimu kutoka nchi 21 za Mashariki na
Kusini mwa Afrika wakubaliane maazimio ya kuongoza juhudi za kuandaa
mazingira salama na wezeshi kwa makuzi ya vijana katika nchi zao.
“Ni muhimu kuyafanyia kazi
maazimio hayo ambayo yatawasaidia vijana kupata elimu kuhusiana na afya
ya uzazi na jinsia jambo ambalo litawasaidia kufahamu zaidi ugonjwa
Ukimwi”, alisema Prof. Tlou.
Mkutano huo ambao pia
ulihudhuriwa na Mke wa Rais wa Malawi Gertrude Mutharika ni moja ya
maandalizi ya Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa (UN) utaofanyika hivi
karibuni mjini humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni