KUNA NGUVU YA MUNGU KATIKA KINYWA CHAKO ITUMIE ITAKUSAIDIA
“Nanyi mtapokea nguvu akiisha
kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU, (Matendo 1: 8).
Je, tunatumia hii nguvu ya
MUNGU?
Na je tunaitumia mamlaka ya
KRISTO tuliyopewa kama inavyotakiwa?
Haijalishi mwana wa MUNGU unapita
katika magumu kiasi gani, Unachotakiwa ni kubadilisha kukiri kwako, na kadri
unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana,elewa kuna jambo katika
ulimwengu wa Roho linafanyika, hata kama huna shilingi mia mfukoni wewe sema
pesa zipo, hata kama wewe ni mgonjwa umelala kitandani Sema mimi ni mzima,
maana Neno la MUNGU linasema aliye dhaifu na aseme ana nguvu.
Ezekieli alipoonyeshwa lile bonde
la mifupa mikavu, kwa macho ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile
mifupa mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia itabirie hii mifupa
mikavu ipate kuishi.
Ndipo Ezekieli akatambua nguvu
iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa unabii na kuitabiria ile mifupa,
akaiambia ’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; BWANA MUNGU
aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi
.Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika
ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi.’’ Maneno haya tunayapata
katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni
jinsi gani Ezekiel ialivyoweza kutumia nguvu na uweza ulioko ndani ya kinywa
chake na kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana wa MUNGU nini ni kimekuwa
mifupa mikavu katika maisha yako?
-Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa
mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena,
-au ni uchumi wako,
- afya yako,
-watoto wako,
-hudumayako,
MUNGU anakuambia leo simama na
uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.
Unakiri nini kushindwa au kushinda?
Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote
yanayoonekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika
Jina la YESU KRISTO mwenye nguvu zote.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni