Jumatano, 12 Novemba 2014



MUCOBA BENKI YAWA CHACHU YA MAENDELEO KWA WAKULIMA MKOANI IRINGA

Meneja wa Benki ya Wananchi MUCOBA Bw Beny Mahenge akielezea utendaji wa Benki hiyo
Wadau wa Benki ya wananchi MUCOBA
Wakulima wa mkoa wa Iringa wameanza kunufaika na ruzuku za pembejeo kupitia Benki ya wananchi Mufindi(MUCOBA) ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la MUCOBA Bank PLC ikijumuisha wananchi wote wa mkoani wa Iringa imeanza kutoa mikopo ya pembejeo kwa vikudi vya wakulima.

Akielezea juu ya namna mwananchi atakavyonufaika na ruzuku hiyo Meneja wa Benki hiyo Bw Ben Mahenge amesema serikali imeamua kutoa ruzuku kwa mkulima kupitia Benki ya wananchi kutokana na ukaribu wa Benki hiyo kwa wananchi wa maeneo yote ya mkoa wa Iringa ili kulinda usalama wa chakula kwa mkulima.

Amesema kuwa walengwa wakuu ni wananchi wa kipato cha chini ili wawe na uhakika wa kupata chakula cha kutosha hususani kwa wale waliolima ukubwa wa shamba la kuanzia ekali moja ambao watasaidiwa kupatiwa ruzuku ya mifuko mitatu ya mbolea na mfuko mmoja wa mbegu kwa mazao ya Mpunga na Mahindi ikiwa ndiyo mazao pekee yanayopendelewa na wananchi wa mkoa wa Iringa.

Bw Mahenge ameendelea kufafanua juu ya ruzuku hizo kuwa itatolewa kwa wakulima watakaojiunga katika vikundi mbalimbali vitakavyojumuisha wanakikundi wasiopungua 10 ambao kila mmoja atapatiwa mkopo wa pembejeo zenye ruzuku ya serikali.

Ameelezea kuwa ruzuku hiyo itatokana na riba ya mkopo atakaoupa kutoka benki ambayo ghalama yake ya ni 18% ambapo serikali inalipa riba ya asilimia 14% ya riba ikiwa kwa upande wa mkulima atalipa riba ya asilimia 4% kutoka kwenye riba ya asilimia 18% ya mkopo wote.

Aidha amesema kupitia benki hiyo ya MUCOBA wananchi watajipatia pembejeo wanazozihitaji badala ya kupangiwa aina ya pembejeo za kilimo ili kuboresha zaidi kipato na mazao ya mkulima ambapo amesema mkopo huo utalipwa baada ya mavuno pamoja na kwa kabla ya mkulima kupewa mkopo huo atatakiwa kulipa asilimia 20 ya kianzio kuonesha nia ya kuhitaji ruzuku.

Hivyo amewataka wananchi kushiriki katika vikundi mbalimbali ili wawe sehemu rahisi ya kupata pembejeo zenye ruzuku ya serikali kwa urahisi zaidi pia amewataka wakulima kumchangua wakala wa pembejeo atakayeshirikiana katika kuzipata zenye viwango vya hali ya juu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni