Jumanne, 11 Novemba 2014



MADIWANI MANISPAA YA IRINGA WAANZA KUTAKELEZA KAULI YA KATIBU MKUU WA CCM KWA VITENDO.

Baraza la Madiwani manispaa ya Iringa lakumbushwa umuhim wao katika kusimamia miradi ya Maendeleo ikiwa ni nguzo ya muhim katika kuendeleza uchumi wa familia,jamii na Taifa.

Hayo yamejili mwisho wa wiki katika kikao charobo ya mwaka wa fedha 2014/2015 cha  Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa mjini ambapo Meya ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo Aman Mwamwindi aliwambia madiwani kuwa nisehemu ya serikali hivyo wanaowajibu wa kusimamia miradi inayoanzishwa na serikali ikiwemo miradi ya Afya,elimu,miundombinu na shughuli za uchumi ili kuongeza upatikanaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
Alisema pamoja na kwamba madiwani hao wanashiriki kwa kiasi kikubwa katika usimamizi wa miradi hiyo lakini pia alipata fulsa ya kuwakumbusha kuwa usimamizi wa miradi hiyo unashirikisha viongozi wa ngazi ya kijiji hadi Taifa,wananchi wa maeneo husika pamoja na asasi za kiraia na kashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa na lengo la kuboresha maisha ya watanzani.

“Waheshimiwa madiwani tumekuwa mstari wa mbele kusimamia miradi inayoanzishwa katika kata zetu japo wapo wachache ambao kazi yao ni kuturudisha nyuma kwa makusudi maana tumekuwa na miradi mingi na inafanya vizuri kwaajili yetu sote na jamii zinazotuzunguka sasa unapoona mtu anaingiza kitu ambacho kinarudisha nyuma juhudi za serikali ukanyamaza manaake unashiriki mojakwamoja kuangamiza maisha ya watanzani”alisema meya

Hivyo amesema usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo mara nyingi inasababisha baadhi ya miradi kufanyika chini ya kiwango.
Baraza hilo pia lilipata nafasi ya kupata semina juu ya ushiriki wao katika mapambano dhidi ya rushwa ambalo limekuwa janga la dunia ambalo limekuwa likiwahusisha zaidi watendaji wa serikali.

Akitoa semina hiyo Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Bw Ismail Bukuku aliwambia madiwani kuwa lengo la semina hiyo ni kuwakumbusha uwajibikaji kwa kufuatamisingi ya sheria huku wakitambua usimamizi mzuri wa raslimali za umma kutasaidia kuziba mianya ya Rushwa,itasaidia fedha za miradi kutumika kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Huku akiwataka madiwani hao kuwaelimisha wananchi kutambua haki zao katika kupata huduma za msingi ikiwa nipamoja na matibabu,ajira,elimu bila kutoa wala kupokea rushwa vilevile  kuzijua sheria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni