ZAIDI YA MIL 400 KUTOKA HIFADHI YA RUAHA ZATUMIAKA KATIKA KUJENGA MIRADI YA UJIRANI MWEMA IRINGA VIJIJINI.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisaini baada ya kuwasili ktk shule ya Sekondari Willium Lukuvi kupokea jengo jipya la Bweni la wasichana. |
![]() |
| Dk Christopher David Timbuka Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Nation Park akiwasilisha ripoti ya Ujenzi wa Bweni Pawaga mbaele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza. |
![]() |
| Viongozi mbalimbali walioongozana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakikagua Jengo la Bweni katika shule ya Sekondari ya Willium Lukuvi lililoteketea kwa moto hivi karibuni. |
![]() |
| Bweni jipya la wasichana Shule ya sekondari Willium Lukuvi baada ya moja kuteketea kwa Moto hivi karibuni. |
![]() |
| Baadhi ya Wananchi waliohudhulia Katika makabidhiano ya Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Idodi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk Christopher Timbuka leo. |
![]() |
| Makabidhiano Baina ya Mkuu wa Mkoa na uongozi wa Tanapa na Serikali. |
![]() |
| Picha ya Pamoja |

![]() |
| Wanafunzi wa Shule ya Msingi Malengamakali wakishuhudia makabidhiano ya Nyumba ya walimu wa shule hiyo. |
![]() |
| Mh.Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha DK Christopher Timbuka wa fungua nyumba ya walimu Malengamakali. |
![]() |
| Hii ni Nyumba ya Polisi Idodi i;iyojengwa Kupitia Mradi wa Ujirani Mwema kupitia TANAPA |
“Wote tuhifadhi na tulinde hifadhi yetu ya Taifa ya
Ruaha kwani ni fahari na Urithi wetu wa watoto na watoto wetu”ni kauli
iliyotolewa na wananchi wa wilaya ya Iringa kuonesha furaha yao Baadha ya
Shirika la Hfadhi ya Taifa TANAPA kupitia mradi wake wa Ujirani mwema na vijiji
vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya kuujenga Bweni la wasichana
Katika shule ya Sekondari Willium Lukuvi iliyopo pawaga,Nyumba ya Polisi
iliyopo kata ya idodi na shule za walimu mbili ambazo zamejengwa na mradi huo
kwa kuthamini jitihada za wananchi Katika kulinda Hifadhi ya Ruaha.
Nyumba hizo mbili za Walimu moja imejengwa Katika kijiji
cha Malenga makali kata ya Idodi na nyingine imejengwa Katika kijiji cha Kipera
iliyopo kata ya Nzihi-kipera jimbo la Kalenga ambapo zaidi ya mil 420
zimetumika Katika shughuli hiyo.
Akizungumza wakatika wa kukabidhi nyumba hizo Mkuu
wa Hifadhi ya Ruaha kwaniaaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA,Dk Christopher David
Timbuka amesema Tanapa kwa kutambua mchango wa wananchi Katika kulinda na kutetea
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha walionana ni vyema kurudisha fadhira kwa kuchangia
badhii ya shughuli za maendeleo hivo wameona na vyema kujenga nyumba za walimu Katika
maeneo hayo ili kuwapunguzia mzigo wa michango ambapo amesema TANAPA ilikuwa
ikichangia kiasi 70% ya mradi na wananchi
% zinazosalia.
“Hifadhi ya Ruaha kupita mradi wake wa Ujirani mwema
tumewazesha ufanikishaji wa ujenzi wa nyumba hizi kwa kushirikiana na wananchi
wa maeneo husika ambapo hifadhi tulitumia asilimia 70% na wananchi
zilizosalia,tumetumia zaidi ya mil 400 katika miradi yote”alisema Timbika
Dk Timbuka Amesema ushirikiano huo uliopo baina ya
wananchi na Hifadhi hiyo ndiyo uliosababisha kufanikiwa kwa miradi hiyo mikubwa
ambayo imekuja kwaajili ya kuwanufaisha wananchi hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuunga
mkono juhudi wanazozifanya kwa maendeleo yao na vizazi vijavyo.
Dk Timbuka alisema “tunawaomba wananchi kuendelea
kusaidiana na Hifadhi ya Ruaha Katika ulinzi wa hifadhi dhidi ya majangili ili
iendelee kuwanufaisha Katika masuala ya kimaendeleo”
Akipokea na Kusaini hati ya makabdhiano ya miradi
hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina masenza ameipongeza Hifadhi hiyo kwa kuona
umuhim wa kujihusisha na masuala ya kijamii hususani Katika kuwasaidia wananchi
suala la michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ambapo pia itasaidia kupunguza
kero za walimu vijijini.“niseme jambo moja nimekubalikupokea miradi hii
ikiwa imekamilika Katika ubora wake ambapo nimeona nyumba za walimu za kisasa
zaidi sana mmenisaidia kupunguza kero kwa wanafunzi wa kike Katika shule ya
sekondari ya Willium Lukuvi pale pawaga baada ya bweni lao kuungua kwa moto hivyo
leo mkaona mtukabidhi baada ya kukamilisha ujenzi,”alisema mkuu wa Mkoa
Aidha Mh.Masenza amewataka wananchi wa wanaoishi
kuzunguka hifadhi au maeneo yaliyohifadhiwa badala ya kukaa kimya mnapoona kuna
uharibifu unatokea kwani kwa kufanya hivyo majangili watabeba rasilimali
zilizopo ambazo zingewasaidia Katika shughuli za mendeleo pia amewataka kutunza
miradi hiyo ya majengo ili yaweze kudumu hivyo ameziagiza kamati za shule
kuwaondoa wale wote wasio na mapenzi mema ili na miradi hiyo ili kuwapawengine
watakaoweza kusimamia ipasavyo kwa faida ya wengine wao.
Akishukuru kwa niaba ya viongozi wa vijiji
vilivyonufaika na miradi hiyo mwenyekiti wa kijiji cha kipera Bw Francis Yangi
ameupongeza uongozi mzima wa hifadhi ya Ruaha kwa mchango walioutoa kupitia
Ujirani mwema hivyo ameahidi kusimamia ushirikiano zaidi hususani Katika ulinzi
wa hifadhi na uhifadhi.























Hakuna maoni:
Chapisha Maoni