UVCCM IRINGA KUSAIDIA JITIHADA ZA SERIKALI KUHAMASISHA VIJANA KUJIARI NA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.
katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi wa pili kulia akiwa na katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw Sixtus Mapunda.
|
Vijana nchini
hususani mkoani Iringa wameshauriwa kujiandaa na kujiweka sawa katika kupambana
na changamoto za ugumu wa maisha kwa kuchangamkia furusa mbalimbali
zinazojitokeza na kujiajiri wenyewe.
Kauli hiyo imekuja
baada ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na kuonesha kuwa vijana wengi wamekuwa
na mitazamo ya kusubiri serikali iwaletee badala ya kufikiri zaidi namna ya
kujitengenezea ajira zitakazo waletea kipato na kuboresha maisha yao hali
ambayo imeendelea kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Akitoa tathimini ya
kikao cha Baraza la vijana mkoa wa
Iringa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Bw Elisha
Mwampashe amewataka vijana wafanye kazi ili wasiendelee kuilamu serikali.
“ninawaomba vijana
ifike wakati tujitambue na tuone jukumu la kujiletea maendeleo katika familia
zetu tusiwe watu wa kulaumu tu badala kuwa na mawazo chanya kujishughulisha na
shughuli zitakazotuletea maendeleo ili hata kama kuna mkono wa serikali kusaidia
jitihada zetu utukute tukiwa tayari tuna mambo tunafanya” alisema mwampashe
Aidha alisema maadhimio ya vijana wa chama cha
mapinduzi katika kikao hicho ni kutoa
elimu kwa vijana itakayowasaidia kutumia changamoto zilizopo kuwa fulsa
zitakazo waingizia kipato pia ameeleza maadhimio mengine kuwa ni kuwatembelea
vijana na kubaini changamoto zinazowakabili na kutafuta namna ya kuzimaliza
mengine ni kusaidia katika shughuli za kijamii ambapo mapema mwezi huu
wanatarajia kuweka kambi ya pamoja kwaajili ya kufyatua tofari na kuanza ujenzi
wa Bweni la shule ya sekondari Idodi lililoteketea kwa moto hivi karibuni kama
vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa iringa ili kupunguza nguvu ya wananchi
katika kuchangia ujenzi huo.
“tumefanya kikao
cha baraza la vijana wa Chama Cha Mapinduzi na tumejadili na kuadhimia mambo
mengi ambayo tunaamini tutayasimamia na kuyatekereza kama vijana tumeadhimia
kuwafikia vijana wengi ili kuangaliachangamoto zinazowakabili na tuone namna ya
kuzitatua na vijana wenyewe kuhakikisha tunatengeneza vikundi vya
kiujasiliamali vitakavyotuwezesha kupata wafadhiri”.alisema
Hivyo Mwampashe amesema
wao kama vijana watahakikisha wanawafikia vijana wote wa mkoa wa iringa ili
kukumbushana wajibu wao katika kujiletea maendeleo na kutambua kuwa vijana
ndiyo nguvu kazi ya Taifa.
Mwampashe amesema
sio jambo jema kwa vijana wenye nguvu kushinda vijiweni wakizungumza siasa na
kucheza bao wakati wenzao wakiwa katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
“tumepita katika vikundi kadhaa hapa
mkoani na tayari tumekutana na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na
ujasiliamali tumezungumza nao tumewapa elimu na baadhi ya vitendea kazi kama
mashine ya ufyatuaji tofari na kuwahamasisha umoja kwa mustakabari wa maisha
yao kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya vijana wanaokaa vijiweni bila kazi yoyote
na kuilamu serikali jambo ambalo halina
manufaa yoyote kwao”.alisema mwampashe katibu wa vijana
Alisema duniani
kote hakuna serikali inayoweza kuajiri kila mtu mwenye uwezo na sifa za kufanya
kazi na akazungumzia umuhimu wa sekta binafsi katika kushughulikia changamoto
ya ajira kwa vijana.
Akizungumzia
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka hu, Mwampashe amewataka wanawake kuondoa hofu na
kujitokeza kwa wingi kushindana na wanaume katika nafasi mbalimbali za uongozi
zinazogombewa.
Pamoja na wanawake,
amewasishi vijana wenye sifa kutupa karata zao katika uchaguzi huo huku
akiwataka wajiandikishe kwa wingi na kushiriki kikamilifu kuchagua viongozi
bora wanaojali matatizo yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni