Alhamisi, 4 Juni 2015

WANANCHI WA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI WAMPOKEA EXAUD KIGAHE KUWA MGOMBEA UBUNGE ENDAPO ATAPITISHWA KUGOMBEA

EXAUD KIGAHE AGOMBEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI.
Exaud Kigahe Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini
Ikiwa mchakato wa kutangaza nia ya kugombea Ubunge na Urais hapa nchini unaendelea jamii imetakiwa kuwachagua watu wenye nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo chanya katika maeneo husika.

 Hayo yamesemwa na Mdau wa maendeleo wilayani Mufindi Bw Exaud Kigahe wakati akizungumza na wandishi wa habari Mjini mafinga wailayani Mufindi Mkoani Iringa wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mufindi kasikazini ambapo amesema ni vyema na wakati umefika kwa wananchi kuwachagua viongozi wenye uwezo na uzalendo wanaoweza kushirikiana nao katika kuleta maendelaeo.

“ni ukweli usiopingika kwamba wakati wa viongozi kuwarubuni wananchi umekwisha ninahakika kwamba Mufindi ninaijua vizuri sana yale maisha wanayaishi wananchi wale siyo ndiyo waliyotakiwa kuishi nimekuja kushirikiana nao tuondoe tatizo la umaskini kikubwa nikipewa ridhaa kwangu wajibu wangu ni kuwaletea maendeleo wananchi” alisema Kigahe

Bw Kigahe amesema mtazamo wa sasa katika kusimamia shughuli za maendeleo zinatazamwa zaidi kwa viongozi ambapo anapotokea kiongozi ambaye hana uwezo hakuna maendeleo yatakayopatikana kwa wakati hivyo amesema endapo atapata nafasi ya kuongoza jimbo hilo kuna mambo lukuki anayoyaona yakitumika kama furusa kwa wananchi wa Mufindi yatawapa maendeleo kwa kasi wananchi hao.

Amesema wilaya ya Mufindi ni miongoni mwa wilaya zenye raslimali za kutosha ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikituwa na wageni huku wazawa wakibaki kuwa walinzi jambo ambalo amesema kusingekuwa na maendeleo hata kwa miaka ijayo bali kwa kutumia rasilimali hizo atahakikisha anawaunganisha wananchi kwa ushirikishaji wa mambo yote ya maendeleo kwa faida ya wanamufindi wenyewe.

“rasirimali zilizopo ninaamini zinatosha sana kutuletea maendeleo wanamufindi ninachokifahamu kwa mufindi na kwamba tuna misitu lakini kutokana na uongozi kutotujali wamekuwa wakitumia watu wa maeneo mengine nadhani muda wa wananchi kutumia misitu yao umewadia nitafurahi nao na kulia nao” alisema

Pia Kigahe amesema inasikitisha kuona rasirimali kama misitu inavunwa na watu wa nje na wenyeji wakibaki maskini jambo ambalo haliwezi kuvumilika,amesema wilaya ya Mufindi ina ardhi ya kutosha ambayo kwa kiasi kikubwa haiwanufaishi wanamufindi.

Hivyo amewataka wananchi kwasasa wasidanganyika na watu wanakuja wakiwa hawana malengo mema na wananchi bali wanahitaji kujinufaisha wenyewe bali sasa amekuja kwaajili ya kushirikiana nao kuiondoa hali hiyo.

“kwa upande wangu ninaamini kwamba wanamufindi wanahitaji mambo makubwa machache tu ambayo nikipata ridhaa na wakati maalumu ukifika nitawaeleza na namna tutakavyo weka mikakati ya maendeleo mimi ninauchungu na maisha yale wanayoishi mama zetu,baba zetu hata wadogo zetu naomba wanipokee tuyamalize hayo” ni maneno ya Kigahe

Jimbo la Mufindi Kaskazini lenye kata 11 za Ikweha, Sadani, Igombavanu, Ifwagi, Mdabulo, Ihalimba, Kibengu, Mapanda, Mpanga Tazara, Ihanu na Ikongosi, Jimbo la Mufindi Kusini litakuwa na kata 14 za Kiyowela, Makungu, Mninga, Kasanga, Igowole, Mtambula, Itandula, Mbalamaziwa, Idunda, Mlangali, Nyololo, Ihowanza, Mtwango na Luhunga:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni