WAFANYABIASHARA IRINGA WATAKIWA KUJIUNGA TANZANIA CHEMBER OF COMMERCE
Wafanyabiashara Mkoa Iringa wametakiwa kujiunga na
Chama cha wafanyabiashara Tanzania Chember Of Commers ili kiwasaidie kutatua
baadhi changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na wandishi wa habari Ofisini kwake
Katibu wa chama hicho Bw James Siziya alisema kumekuwa na matatizo mbalimbali
yanayowakabili wafanyabiashara yanayosababisha kusimama kwa shughuli zao jambo
ambalo amesema linaweza kushughulikiwa na na chama hicho.
"nimeona niwakumbushe wafanyabiashara wajiunge na Chember hii hapa ndipo wataleta malalamiko yao na hapa ndipo watapata majibu ya maswali yao wanayojiuliza juu ya mambo yanayowatatiza" alisema Siziya
Bwana Siziya Alisema ni vyema wafanyabiashara
wakajiunga katika chama hicho ni maalum kwaajili ya kutetea masilahi ya
wafanyabiashara hususani wale waliojiunga nacho ambapo chama hicho ndicho
chenye dhamana ya kushughulikia migogolo na malalamiko yao kwa kufikisha mahali
panapo husika na kuhakikisha yanashughulikiwa.
Alisema miongoni mwa changamoto zinazo wakabili wafanyabiashara ni pamoja na uelewa mdogo juu
ya mambo ya kisheria,Kodi na matumizi ya mashine za kielectronic pamoja na
kutojua sheria ya vipimo na mizani jambo ambalo amelitaja kuchangia ongezeko la
kodiya usafirishaji bidhaa.
Aidha aliwataka wafanyabiashara kujisajili na Tanzania Chember Of Commers kwa kuwa
kitawasaidia kutambua sheria mbalimbali na kuepukana na usumbufu utakao
wacheleweshea utendaji wao wa kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni