Jumapili, 22 Februari 2015

WAZIRI MKUU AWATAKA WATENDAJI KUFANYAKAZI KWA WELEDI ILI KULILETEA TAIFA MAENDELEO.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akisalimiana na Watumishi wa Hospitali ya Wilaya Iringa Mijini.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watendaji wa Halmashari za mkoa wa Iringa kufanya kazi kwa Weledi ili kuongeza ufanisi katika kuleta maendeleo.
Agizo hilo lilitowa na Waziri Mkuu  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ipogolo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano ya kiserikali katika mkoa wa Iringa.
Waziri mkuu Pinda alifanya ziara katika halmashauri zote za mkoa wa Iringa na kukagua miladi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Umwagiliaji na katika halmashauri ya Manispaa ya iringa  amekagua ujenzi wa Maabara katika shule ya sekondari kihesa na kuupongeza ungozi wa kata hiyo kwa kuwa shule ya mfano kwa ufanisi.
“katika shule shule zote nilizopita kukagua ujenzi wa maabara shule yenu ya sekondari Kihesa nimerishwa na ni shule ya kuigwa kwa kazi nzuri inayoendana na matakwa ya serikali imejengwa kwa ufanisi mkubwa”alisema Pinda
Akizungumzia ujenzi wa maabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Waziri mkuu alisema hakfurahishwa na miundombinu iliyotumika katika ujenzi huo kutokana na kutumiwa kwa majengo ya zamani na ambayo hayana Ubora na kwakiwango cha Chini bali alisema amewaagiza viongozi wa halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuyaweka katika hali nzuri.
“Nimetembelea shule ya sekondari pale Ilula ili kukagua agizo la Rais la ujenzi wa maabara linavyoenda siku ridhishwa sana kwani wamechukua maabara za miaka 20 iliyopita na kuzifanya zitumike sasahivi kitu ambacho hakiwezi kufanya vizuri kama ilivyokusudiwa”alieleza
Pia amefungua kituo cha polisi Kiheza kilichojengwa kwa ufadhiri wa Mbunge wa viti maalum mkoani hapa Ritta Kabati ambapo kimetumia zaidi ya Milion 40.
Katika sekta ya Afya Waziri Pinda baada ya kukagua na kuzindua kituo cha Afya Mlowa kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Hospitali ya Wilaya iringa Mjini alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni