TASAF KUWANUFAISHA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU
NA AGUSTINO KIHOMBO IRINGA
Zaidi ya kaya elfu sita zinazoishi katika mazingira
magumu za manispaa ya Iringa zinatarajia kunufaika na mfuko wa maendeleo ya
jamii TASAF katika awamu ya tatu ya mpango wa kupunguza umasikini kwa jamii.
Akizungumza na mtanandao huu Mratibu wa Mfuko huo
Manispaa ya Iringa Bi Lucy Mtafya alisema kuwa mpango wa matumizi ya mufuko huo
umegawanyika katika awamu tatu ambapo katika awmu ya Kwanza mfiko huo wa
maendeleo ulijikita zaidi katika kusaidi katika uboreshaji wa huduma za Elimu
na Afya hususani ujenzi wa shule na Zahanati.
Akielezea juu ya Awamu ya kwanza ya TASAF alisema wamefanikiwa
kwa kiasi kikubwa katika kusaidia shughuli za maendeleo ambapo mfuko huo
ulikuwa ukichangia kwa asilimia 80% ya ujenzi na wananchi 20% hivyo hadi awamu
hizo mbili zimesaidi kujenga zaidi ya Shule tano na zahanati Tatu katika
manisipaa ya Iringa.
“Kwa ujumla Mfuko huu wa Maendeleo ya jamii TASAF
tumefanikiwa vizuri sana kuwasaidia wananchi katika shughuli zao za maendeleo
mfuko huu kila mahali ulipofanya kazi ulichangia aslimia 80% na wananchi walichangia
asilimia zinazo baki hiyo katika awamu hizo mbili” alisema
Akizungumzia kuhusiana na awamu hii ya Tatu ambayo
imezinduliwa rasmi Jan 6 2015 Bi Mtafya
alisema tayari wamekwisha anza kushughulikia masuala ya kuzitambua kaya za watu
wasio jiweza ambao ndiyo wanaolengwa na awamu hii ambapo wanalenga kuzifikia
kaya zaidi ya 6000 ili kuwawezesha kiuchumi.
Mratibu huyo alisema wamejipanga kuhakikisha
wanaolengwa na Mfuko huo kwa awamu hii ya tatu wananufaika na fedha
zitakazotolewa na mfuko huo alisema katika manispaa wanafanya kazi na kata zote
za manispaa ya iringa.
“katika awamu hii ya tatu ya Mfuko wa maendeleo ya
jamii TASAF imelenga kuwafikia wote wanaohusika hasa wale ambao mitaa yao
itakubaliana kuwa ndiyo watakao nufaika zaidi kwani katika siku za nyuma baadhi
ya watu walikuwa wanajaribu kutumia ujanja kuwandika watoto wao wasaidiwe na
kuwfanya walengwa wakose” alisema
Hivyo amewataka wananchi kusaidiana na serikali
katika kuwasaidia waishio katika mazingira magumu ili kuwawezesha kumudu maisha
pindi awamu hiyo itakapopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni