Jumanne, 26 Mei 2015

Unaweza kuwasiliana na Mwimbaji kwa 0757 322 501 kwa mialiko mbalimbali



JE UNAMJUA MICHAEL KOMBA? MWIMBAJI NA MUHUBIRI WA INJIRI TANZANIA?


Moja kati ya Majukumu niliyonayo ni kuhakikisha unapata habari za waimbaji wa Nyimbo za Injiri Tanzania kupita mtandao na OVERCOMERS FM 98.6 IRINGA.
 
Mtumishi wa Mungu Michael Komba akiwa katika huduma ya Maombezi katika ibada
Mtumishi wa Mungu Michael Komba akiwa katika Mkutano wa Nje.

Waimbaji waliotikisa katika Mkutano huo wa Mtumishi Komba
Mtumishi wa Mungu Michael Komba akiwa na Mkewe (TUPONILE KOMBA)
 Leo napenda uweze kumfahamu Michael Komba Mwimbaji wa nyimbo za Injiri na Muhubiri wa neno la Mungu huyu ni miongoni mwa waimbaji wanaoendelea kufanikiwa kupitia utumishi wa mungu ambapo Mungu amekuwa akimtumia kwa namna ya kipekee nay a tofauti ambapo amekuwa akitumika katika maeneo mengi ya ndani na nje ya nchi kwa njia ya uimbaji na Kuhubiri Neno la Mungu katika mikutano mbalimbali.

Tukataka kufahamu historia ya uimbaji wake Komba anasema anamshukuru Mungu kwa Neema aliyompa hadi alipofikia kwani ameanza kitambo uimbaji wake tangu akiwa mdogo mpaka kufikia alipofikia nabado anakaza moyo kusonga mbele.

“ni kweli nimeanza kitambo kweli sana mnamo mwaka 1987 baada ya kuokoka na ndipo nilipopata kibali cha kumtumikia mungu kwa njia ya uimbaji” alisema Komba

Pia hatukusita kutaka kujua komba ikiwa amfanikiwa kuwa na albamu ya nyimbo za Injiri ambayo tayari iko sokoni kwa sasa tangu alipoanza uimbaji ma mafanikio yake yakoje alisema

“nimefanikiwa kurekodi nyimbo ambazo ni albamu tangu 2009 inayofahamika kwa jina la MUNGU HALI UGALI ambayo inatamba sasa katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na nje nchi na Mungu amenibariki nimeshaitengenezea video ambayo inatarajia kutoka siyo muda mrefu ambayo itakuwa yenye ubora wa kiwango cha kiutumishi hivyo mashabiki wangu na wadau wa muziki wa Injiri watarajie kitu kupitia DvD hiyo” alisema

Akizungumza namna mungu alivyo muinua katika kuhubiri neno la mungu katika mikoa mbalimbali na nje nchi komba amesema tangu mwaka 2012 amekuwa akitumika kuhubiri injiri na amemuona mungu kupitia huduma hiyo.

“Mungu amenipaka mafuta ya kunena Neno lake kwa Ufunuo usio wa kawaida mikoa mbalimbali ya Tanzania na nje ya nchi kama Jijini Nairobi Kenya na kwingineko,ninaujumbe mzito kwa kanisa naipenda sana huduma hii ninafundisha katika makongamano na semina makanisani”alisema komba

Akizungumzia Baraka ya kumpata mke wa kufanana naye komba amesema anamshukuru mungu kwaajili ya mke wake kwani amekuwa Baraka kubwa kwake kutokana na namna alivyowainua katika huduma hii alisema

“naimba na kuhubiri pamoja na mke wangu Tuponile Komba Bwana anatutumia kwa namna ya kipekee nimemuona Mungu kupitia mke wangu hususani uvumilivu wake na maombi juu ya familia yetu tuliyo nayo hii ni Baraka”alisema komba

Hivyo amesema kuwa yuko tayari kwa mialiko mbalimbali iwe uimbaji ama Kuhubiri katika mikutano mbalimbali na semina.
Unaweza kuwasiliana nae kwa Namba  0757 322 501
 

Jumatatu, 25 Mei 2015

CAROLINE ACHERY MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJIRI MWENYE MALENGO NA MTAZAMO WA MBELE KATIKA HUDUMA NA KATIKA JAMII

Caroline katika Ubora wake
Ni mwimbaji wa nyimbo za Injiri jijini Dar es salam ambaye amekuwa na malengo ya kufika mbali pia kupitia huduma yake ya Uimbaji amepanga malengo makubwa ya kuisaidia jamii
"mimi katika huduma ya uimbaji nilianza kitambo kidogo toka nikiwa mtoto nilikuwa naimba Sunday School nimekuwa hivo nikaingia katika kwaya ambako hadi sasa ni kiongozi wa Kuabudu kanisani na mshukuru Mungu ananitumia katika kuabudu na nitaendelea kumuabu siku zote" alisema Caroline

Ni miongoni mwa waimbaji wachache ambao tayari pamoja na shughuli zao binafsi amefanikiwa kuwa na kituo kidogo cha kulea watoto yatima kilichopo mkoani Arusha akiwa na malengo ya kuwa mlezi wa watoto yatima na Wajane  kituo hicho kipo Umasaini huko na Kinafahamika kwa Jina la LOBOSIRETI naamini kwa wakazi wa Arusha wanalijua maana ya jina hilo. ''mimi napenda kwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo namshukuru Mungu nimefanikiwa kuanzisha kituo cha watoto yatima na wajane ambacho kimsingi bado kichanga kutokana na uhaba wa fedha za kukiendesha bali namwamini mungu atanipa kwasababu nimaombi yangu kituo kile kifanikiwe kiwe msaada wawatu wasiojiweza" alisema

Pia kuhusu kutoa albamu zake za nyimbo alisema yeye amefanikiwa kuwa na albam Moja haya ni maneno yake"albam yangu ya kwanza Inaitwa 'MWANGALIE MUNGU' niliitoa mwaka 2008 na kuiweka wakfu mwaka 2009 katika kanisa la maranatha Arusha ambako ndiko ninakolelewa kiroho toka nina umri wa miaka nne mpaka leo" alisema


Akizungumzia Ujio wa Albam yake mpya ya Audio Caroline amesema anatajia kuitoa siyo muda mrefu kuanzia sasa na kuwataka mashabiki wake wa muziki wa Injiri kukaa mkao wa Burudani kwani itakuwa ya Viwango hivyo wamsapot kwa mawazo hata kwa kuitafuta kwani anasema"namshukuru mungu ameniwezesha baada ya ile albamu yangu ya kwanza sasa natarajia kuitoa albamu ya pili ambayo itatoka mwezi wa sita na inatwa 'SUBIRI WAKATI WA BWANA' na ninaamini itawabariki sana" alisema hayo katika Hot Interview tuliyoifanya na mwimbaji huyu

Pia alizungumzia mpango wake wa kuzifanya albamu zake za sauti kuwa katika mfumo wa Picha anasema hiyo ni hatua ambayo anaiendea kwa sasa kwa hiyo anatarajia kuzirekodi nyimbo hizo kwa mfumo wa Video hivi karibuni " Mpango wangu ninatarajia kuja kufanya video ya Live yenye nyimbo za kuabudu na pia kutengeneza  kundi la wamwabuduo halisi ambalo litakuwa likifanya uimbaji wa Live ndani na Nje ya nchi kwa nyimbo za kuabudu na kusifu"alisema Caro

Moja kati ya mambo ya kujifunza kwa Caroline ni pamoja na kuwa na malengo pamoja na kujituma kwa mwimbaji itakuwa sehemu ya kukutoa mahali ulipo kwenda katika hatua nyingine maana unaweza kuwa ni mwimbaji mzuri kama hutakuwa na malengo katika uimbaji wako wala bidii hakika kuzifikia ndoto ni vigumu. Tunakutakia safari njema katika huduma na malengo uliyo jiwekea